25 Dec 2008


Serikali imeridhia Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA- JKT), liongezewe nguvu kiutendaji na kuwa kampuni ya ulinzi itakayotoa ushindani kwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayotoa huduma hiyo kwa kiwango kisichoridhisha. 

Kwa sasa SUMA, imejikita katika ujenzi wa nyumba za serikali, barabara na kutengeneza samani. 

Uamuzi wa JKT kuwa na kampuni ya ulinzi, una lengo la kuajiri vijana wanaohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi. 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Kanali Ayoub Mwakang’ata, alitoa taarifa hiyo jana wakati akihutubia katika kilele cha mafunzo ya Operesheni Uadilifu yaliyokuwa yakifanyika katika Kambi ya 835 JKT Mgambo wilayani Handeni. 

Katika taarifa yake alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi hilo wameridhia kampuni hiyo kuanza kazi rasmi mapema mwakani. 

Kampuni hiyo imepanga kuboresha huduma za ulinzi kwa kuajiri askari waliopitia Jeshi hilo pekee na kuwasambaza katika maeneo mbalimbali nchini kote wakichuana na makampuni mengine yaliyoko sasa, lakini bila ya kuathiri utendaji wao. 

``Suma JKT itakuwa kampuni ya ulinzi rasmi kuanzia mwakani na itachukua vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi na si askari wa akiba wa mgambo, mpango huu ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia vijana kama hawa kupata ajira za uhakika baada ya kuhitimu mafunzo haya… na ukweli ni kwamba hatua hii itakuwa ni changamoto kwa vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kujiunga JKT,``alisema. 

Awali Ofisa Utumishi wa JKT Makao Makuu, Meja Elvis Massawe alipohojiwa kuhusiana na hatua iliyofikiwa hadi sasa na Kitengo hicho cha SUMA alikiri kwamba Ofisi hiyo imeshapokea maombi zaidi ya robo tatu ya vijana waliohitimu katika Jeshi hilo nchi nzima wakisubiri kuajiriwa rasmi. 

Kwa mujibu wa Ofisa huyo ni kwamba Kampuni hiyo mbadala ya ulinzi itachukua askari wa rika mbalimbali bila kujali umri wao na kwamba bado jeshi hilo linapokea maombi ya yawanaotaka kujiunga na kampuni hiyo...

CHANZO: Nipashe

SINA HAKIKA KAMA UMEFANYIKA UTAFITI WA KUTOSHA KUHUSIANA NA MAAMUZI HAYA MAZITO (IT'S PERSONAL KWANI NAMI NI MMOJA KATI YA WALIOPITIA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MIAKA YA 90).NAAMINI TATIZO KUBWA LINALOKWAZWA KUIREJESHA JKT KUWA KAMA YA ENZI HIZO NI PAMOJA NA MIPANGO DHAIFU ISIYOANGALIA MBALI.SIJUI BABA WA TAIFA HUKO ALIKO AKISIKIA JKT INATAKA KUGEUZWA KAMPUNI YA ULINZI ATAJISIKIAJE LAKINI KWA HAKIKA NI JAMBO LINALOTIA SHAKA SANA HASA IKIAZINGATIWA KWAMBA JESHI SIO TAASISI YA BIASHARA.NI VIGUMU KUTUAMINISHA KWAMBA JKT ITAWEZA KUHIMILI USHINDANI WA KIBIASHARA KATIKA SEKTA YA ULINZI BINAFSI ILHALI UFANISI WA VITENGO VYA KIBIASHARA KATIKA JESHI HILO (KWA MFANO SUMA NA MRADI WA KOKOTO KUNDUCHI) WENYE MUSHKELI.

JKT INGEWEZA KUWA KITUO CHA KUZALISHA AJIRA KWENYE SEKTA YA KILIMO NA HATA UJASIRIAMALI IWAPO KUTAKUWA NA MAANDALIZI SAHIHI.MSISITIZO WA JKT NI KUWAANDAA VIJANA KULITUMIKIA TAIFA LAO KWA UZALENDO NA SIO KWENDA KULINDA MALI ZA WATU (INCLUDING MAFISADI).HATA KAMA WAZO LA BIASHARA YA ULINZI NI ZURI BADO KUNA WASIWASI KUHUSU MASLAHI YA VIJANA HAO,JAMBO AMBALO LISIPOANGALIWA KWA MAKINI LINAWEZA KUZAA MAJAMBAZI BADALA YA WALINZI BINAFSI.ULINZI NI TAALUMA NYETI NA ISIPOTENGENEZEWA SERA MAKINI INAWEZA KUZAA MAYHEM KATIKA JAMII.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.