27 Apr 2009

MOJA YA MAENEO KOROFI KATIKA BARABARA KUU WILAYANI KILOMBERO.UNGETEGEMEA VIONGOZI WA WILAYA HIYO WAELEKEZE NGUVU ZAO KWENYE KU-ADDRESS SHIDA ZA WANANCHI (KAMA HIYO YA BARABARA) BADALA YA KUTAKA KUUZA ARDHI YAO.HUU NI UNYAMA USIOKUBALIKA HATA CHEMBE.ANYWAY,2010 IS COMING.I HOPE UKATILI HUU WA VIONGOZI WABABAISHAJI UTAKUWA SABABU TOSHA YA KUWAPIGA CHINI KWENYE UCHAGUZI.

na Mwandishi Wetu, Kilombero

KIJIJI cha Namwawala, kilichopo Kata ya Idete, Tarafa ya Ifakara, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, kiko hatarini kuuzwa kwa mwekezaji, huku viongozi wanaosimamia mpango huo wakidai ni agizo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka katika kijiji hicho, zilidai kuwa baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa, wanasimamia uuzaji wa ekari zaidi ya 3,384, sawa na asilimia 95 ya ardhi ya kijiji chote, kwa ajili ya mwekezaji anayetarajia kuanzisha mashamba ya miwa na kiwanda cha sukari.

Hivi sasa, kijiji hicho kimeunda kamati kufuatilia mambo manne ya msingi ambayo ni kuthibitisha kauli ya viongozi wao kwamba Rais Kikwete ameamuakuchukua ardhi hiyo, na kama ardhi inayochukuliwa ni asilimia 95 ya eneo lote la
kijiji.

Mambo mengine ni, Mkurugenzi Mtendaji Kilombero kuanza kuthaminisha mali zao bila taarifa rasmi na kutaka wasomewe waraka unaoelekeza Rais Kikwete kutoa agizo la kuchukua ardhi na kumpa mwekezaji.

Kamati hiyo ambayo inadaiwa kuishi kwa kutishiwa na baadhi ya viongozi wilayani humo, inaundwa na Mwenyekiti Zuberi Kapindijega, Kenani Haule (Katibu), wakati wajumbe ni Johson Msuya na Godfrey Lwema.

Akizungumza na Tanzania Daima kutoka mjini Ifakara jana, Kapindijega, alisema baada ya viongozi wa wilaya na kata kupita kwa wananchi na kuwataka waanze kufanya tathimini ya mali zao na kujiandaa kuhama, walifikisha barua yao kwa Rais Kikwete jijini Dar es Salaam wakitaka ufafanuzi wa mpango huo.

“Januari 31 kwenye mkutano wa mapato na matumizi ya kijiji, iliibuka hoja ya wanakijiji kutaka kujua hatma ya ardhi yetu, ndipo mwenyekiti wa kijiji alitusomea waraka aliodai wa rais, ambao umetumika katika kuchukua asilimi 95 ya ardhi hiyo. Kutokana na mazingira na mfumo uliotumika kufikisha waraka huo wa rais kwetu, tunahisi kuna mchezo
mchafu.

“Kwa hofu hiyo na kwa kuwa kila tunaloliuliza jibu ni moja tu la rais kaamua kuchukua ardhi yake, ndiyo maana tumeamua kuja kuonana na wewe mwenyewe Mheshimiwa Rais,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo kwenda kwa rais iliyoandikwa Februari 13 na Tanzania Daima kupata nakala yake.

Hata hivyo, katika majibu ya rais kwa viongozi hao wa tume yalitolewa kwa barua iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, F. Mwaipaja, Februari 16, viongozi hao walitakiwa kuwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, na Mkuu wa Mkoa na kama hawataridhishwa, wanaweza kuonana na rais.

Kutokana na barua hiyo kutoka kwa rais, viongozi wa tume hiyo walibisha hodi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa barua waliyoiandika Februari 20 nakufuatiwa na nyingine ya Februari 27, ambazo pia Tanzania Daima nakala zake inazo.

Hata hivyo, ofisi hiyo ya mkuu wa wilaya, ilijibu barua hiyo kupitia kwa Katibu Tawala, E Mmbaga, akidai kuwa ameagizwa na DC Evarist Evarist Ndikilo awajulishe wajumbe hao wa tume kwamba amepokea barua hizo.

“Aidha mnafahamishwa kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itawasiliana na SUDECO, Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Serikali ya Kijiji (Namwawala) pamoja na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), wanafanya tathmini ya fidia. Mnaombwa mvute subira kwani matokeo ya mawasiliano hayo, mtajulishwa,” ilisema barua hiyo.

Baada ya majibu hayo, tume hiyo pia ilifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, na kuwasilisha barua yao Machi 6, mwaka huu kutaka kupata ufafanuzi wa kuuzwa kwa ardhi ya kijiji chao.

Ofisi ya mkoa kupitia kwa Kaimu Katibu Tawala, L. Msuya, iliahidi katika barua yenye kumb namba CD/148/06/87, kwamba italishughulikia suala hili kwa makini.

“Kumbukeni kwamba mmeshafikisha malalamiko yenu kwenye ofisi ya rais na sasa mmerudishwa kwa Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo suala hili linatakiwa lishughulikiwe kwa umakini sana.
Mnatakiwa mvute subira wakati mkuu wa mkoa anafanya uchunguzi wa kina ili kupata ufumbuzi wa kudumu,” ilisema barua hiyo.

Hata hivyo, akizungumzia malalamiko ya tume hiyo, DC wa Kilombero, jana alikaririwa na moja ya vyombo vya habari vya kila siku kwamba wajumbe wa tume hiyo ni wachochezi na kutoa amri wakamatwe mara moja.

Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini kuwa, hali ya kijiji hicho si shwari kwani wananchi wanashindwa kuendelea kufanya shughuli za maendeleo kwa hofu ya kuhamishwa, huku baadhi ya viongozi wakitofautiana kuhusu mpango huo unaodaiwa kuendeshwa kiujanja ujanja kwa kutumia jina la rais.


THIS IS BECOMING PERSONAL!TATIZO LA WILAYA YETU (NA JIMBO LA KILOMBERO KWA UJUMLA) NI KAMA HATUNA MBUNGE.KUNA JAMAA ANAITWA LIGALAMA.I JUST CANT UNDERSTAND WHAT THIS GUY HAS BEEN DOING!BADALA YA VIONGOZI KUWEKEZA NGUVU ZAO KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO WAO WANAENDEKEZA USHKAJI NA WAWEKEZAJI....NA HAIHITAJI UTAFITI KUFAHAMU KUWA KICHOCHEO KIKUBWA HAPO NI RUSHWA NA UFISADI KWA UJUMLA.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.