11 May 2009


Na Frederick Katulanda, Busanda

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzongwa na kundi la wananchi waliomuhoji juu ya ahadi zake za umeme alipowasili katika mji wa Katoro wilayani Geita.

Tukio hilo mithili ya mdahalo lilitokea kati ya majira ya ya saa 9:30 hadi saa 10:15 muda mfupi tu baada ya Ngeleja kuwasili Busanda akitokea Mwanza.

Maswali yalianza baada ya Waziri Ngeleja kusalimiana na wananchi hao na akajibiwa kwa kuonyeshwa alama za vidole viwili.

Hali hiyo ilimfanya waziri huyo kuwauliza wananchi hao sababu za kuichukia CCM wakati imekuwa ikijitahidi kuwaletea maendeleo na ndipo walipoanza kumuuliza maswali huku akiyajibu wakati fulani kugeuka mabishano.

"Hatuwezi kuwashangilia nyinyi... mmetuahidi umeme siku nyingi na hatuuoni, leo mnakuja kutuambia nini. Alikuja hapa sijui (Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam) Malima akasema umeme utakuja, lakini wapi hatujaona lolote mpaka leo," alisema mwananchi mmoja.

Ngeleja alipotaka kujibu, mwananchi mwingine alidakia kusema: "Hata kwenye machimbo mmekuwa mkitunyang'anya maeneo yetu na kuwapa wawekezaji. Sisi mnatuona hatufai kama vile ni wakimbizi ndani ya nchi yetu."

Ngeleja alilazimika kuwatuliza na kuwaomba wapunguze maswali ili ajibu swali moja baada ya jingine, lakini kila mtu akataka kumuuliza swali na kukawa na msuguano kati yake na wananchi.

Alianza kujibu kwa kusema kuwa serikali ipo mbioni na kwamba kinachofanyika sasa ni kufuata taratibu kwa sababu mchakato wa suala hilo hauwezi kumalizika siku moja, hivyo akawaomba wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea.

Ngeleja alidai kuwa suala lao kuhusu umeme liko katika hatua ya kuridhisha na kwamba wanapaswa kutambua utaratibu wa kushughulikia miradi ya serikali umekuwa ukifanyika kwa hatua.

Majibu hayo yalipingwa na wananchi ambao walimwambia wamekuwa wakidanganywa kama watoto kwa sababu ya kutaka kura na wakishapata, hutoweka.

"Sikiliza basi nikujibu, wewe naona umetanguliza ushabiki tuu. Naomba unisikilize. Ni kweli tulipowaahidi umeme tulidhani mchakato ungekamilika mapema, lakini kuna mambo yametukwamisha, tunaomba mtuvumulie," alisema huku wananchi hao wakiendeleza maswali.

Wakati wakiendelea na mjadala huo, lilipita gari la mgombea CCM wa kiti cha ubunge cha Busanda, Lolensia Bukwimba na mara moja wananchi hao wakageuka na kuanza kuzomea msafara.

Wakati wakiendelea kuzomea ndipo Ngeleja alipopata mwanya na dereva wake akawasha gari na kuondoka.

Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited.

CCM imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na Faustin Kabuzi Rwilomba ambaye alifariki akiwa nchini India alikoenda kutibiwa
.

CHANZO: Mwananchi

IWAPO KUNA LOLOTE LA KUJIFUNZA KATIKA KAMPENI HIZI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUSANDA BASI NI NAMNA CCM ILIVYO KICHWA NGUMU KUELEWA SOMO.THING IS,WAMESHAHADAA WAPIGA KURA KIASI CHA KUTOSHA KWA AHADI HEWA,HIVYO KUREJEA TENA AHADI HIZOHIZO AMBAZO HAWAJAZITEKELEZA NI MITHILI YA,ASHAKUM SI MATUSI,KUMTONGOZA MTALAKA WAKO.

PENGINE JINGINE NI NAMNA CHAMA HIVYO KISIVYO SERIOUS NA USTAWI WA WANANCHI.WHY?BADALA YA KUREJEA AHADI HIZO AMBAZO HAZIJATEKELEZWA,CHAMA HICHO KWANZA KILIPASWA KUWAOMBA RADHI WAPIGA KURA KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA AHADI HIZO HADI SASA,NA ANGALAU BAADA YA HAPO KINGEWEZA KUJARIBU KETE YA KUREJEA AHADI HIZO.NASEMA THAT IS INDICATIVE OF LACK OF SERIOUSNESS KWA VILE CCM INAAMINI KUWA KAMA ILIKUWA IKITOA LOTS OF EMPTY PROMISES FOR AGES NA WAGOMBEA WAKE WAMEENDELEA KUCHAGULIWA,BADO KUNA IMANI KUWA SUCH A RISKY STRATEGY COULD WORK AGAIN AND AGAIN.

CCM HAIDHANI KUWA IMAGE YAKE IKO SEVERELY TARNISHED NA USWAHIBA WAKE NA UFISADI/MAFISADI.INAENDELEA KUAMINI KUWA SHUTUMA DHIDI YAKE KWAMBA NI KICHAKA NA HIFADHI YA MAFISADI NA ZA WATOVU WA NIDHAMU WACHACHE KAMA SIE LAKINI SIO KWAMBA KELELE ZETU NI UWAKILISHI TU WA VILIO VYA MAMILIONI YA WATANZANIA WALIOCHOKA KUFANYWA WAJINGA.

HIVI KIONGOZI MWENYE BUSARA ANAWEZA KUDIRIKI KU-BRING UP ISHU ZA DOWANS KWENYE BY-ELECTION KAMA YA BUSANDA?CAN'T BLAME NGELEJA KWA KUWA KWA YEYE NA VIGOGO WENZIE WA CCM,EQUATION YA DOWANS=RICHMOND HAIJAMWINGIA KICHWANI.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.