8 Jun 2009


WHY SHOULD WE ALWAYS LESS,IF NOT NOTHING AT ALL?HIVI TUNGEKUWA NA WAWEKEZAJI NCHINI INDIA (WANAKOTOKA WABABAISHAJI WA TRL) HALAFU WASHINDWE KUKIDHI MATARAJIO YA WAHINDI,UNADHANI WASINGETIMULIWA?POROJO KWAMBA PASIPO TRL HUDUMA ZA RELI YA KATI NDIO KWISHNE HAZIINGII AKILINI HATA KIDOGO.KAMA TUNAWEZA KUWALIPA WABUNGE WETU MAMILIONI YA SHILINGI KILA MWEZI PASIPO KUHITAJI MSAADA WA WAWEKEZAJI,SIONI KWANINI TUSHINDWE KUMUDU UENDESHAJI WA HUDUMA YA TRENI RELI YA KATI.




Abiria 552 waliotakiwa kusafiri na treni ya kati juzi, wamekwama jijini Dar es Salaam baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya ReliTanzania (TRL), kugoma kwa lengo la kushinikiza uongozi wa shirika hilo, kusaini mkataba wa Maisha Bora unaojulikana kwa jina la Mkataba wa Hiyari.

Wakizungumza na 'HabariLeo Jumapili' katika nyakati tofauti, baadhi ya abiria waliokuwa wakitarajia kwenda Tabora, Mwanza na Kigoma, walisema walipaswa kusafiri juzi lakini ilipofika saa mbili usiku, walitangaziwa kuwa safari hiyo haipo na kutakiwa kusubiri hadi kesho yake (jana) kujua hatma ya safari hiyo.

“Kweli tulisubiri na ilipofika leo (jana) saa tano, tulitangaziwa kuwa safari haitakuwapo hivyo tujipange kwenye mstari ili turudishiwe nauli zetu. “Sisi tumefedheheshwa sana na kitendo hiki hivyo tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti ili abiria wanaotegemea usafiri wa treni wasiendelee kuumia,” alisema abiria aliyejitambulisha kwa jina la Masanja Said.

HabariLeo Jumapili imeshuhudia abiria wakiwa katika mistari mirefu wakisubiri kurejeshewa fedha za nauli wakati watoto na wazee walikuwa wamelala sakafuni kwenye jengo la kampuni hiyo. Meneja Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez, alisema mgomo huo hautambuliki kisheria kwa kuwa viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) wanasema hawajatangaza mgomo.

“Baada ya wafanyakazi kugoma, uongozi uliwasiliana na viongozi wa Trawu lakini viongozi hao walisema hawajatangaza mgomo kwani kisheria tangazo la mgomo linatolewa saa 48 kabla ya kuanzamgomo. Hata hivyo hakuna tangazo lolote wala kiongozi wa mgomo hajulikani,” alisema Meaz.

Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao waligoma baada ya viongozi wa Trawu kuwapatia ripoti kwamba uongozi wa kampuni umegoma kusaini mkataba wahiyari na kwamba uongozi umeondoa kipengele kinachomtaka mwajiri kuwalipa wafanyakazi wanaopunguzwa kazi mishahara ya miezi 20 hadi 40 kama mkono wa heri.

Meaz alisema, uongozi wa TRL uliamua kurejeshea abiria fedha zao baada ya juhudi za kuwataka wafanyakazi hao kusitisha mgomo kutozaa matunda. Alisema uongozi umejaribu kuwasiliana na TRAWU Taifa na kujibiwa kuwa hakuna mgomo ila ni shinikizo.

“Tatizo haijulikani nani kiongozi wa mgomo, kila anayeulizwa anasema hajui lolote. Kisheria hakuna mgomo lakini katika hali halisi wafanyakazi wamegoma na ndio maana abiria wamerudishiwa fedha zao za nauli,” alisema Meaz. Juhudi za kuwapata viongozi wa Trawu haikuzaa matundakwa kuwa ofisi zao zilikuwa zimefungwa pia simu za mkononi zilikuwa zimefungwa.

CHANZO: Habari Leo


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.