20 Aug 2009


Labda CCM imekaa madarakani kwa muda mrefu mno hadi imefikia hatua ya kusahau wajibu wake. Pengine ni matokeo ya mafisadi kushika hatamu ndani ya chama hicho, au pengine ni CCM imesharidhika kwamba Watanzania wamezowea kunyanyaswa, kupuuzwa na kuchezewa kama watoto wadogo pasipo kuchukua hatua yoyote.

Najiuliza hivyo baada ya kusoma habari kwamba chama hicho tawala “kimechimba mkwara mzito” kwa baadhi ya viongozi na wanachama wake wanaodiriki kunyooshea vidole ufisadi na mafisadi.Ungetegemea CCM ingekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mapambano dhidi ya ufisadi na mafisadi kwa vile so far ndio kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa kauli-mbiu Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Lakini kwa vile mafisadi ni watu muhimu sana kwa chama hicho, jaribio lolote la kuwakemea ni sawa na kusigina katiba ya CCM.

Kana kwamba kushindwa ku-meet matarajio ya wapigakura (waliokipa dhamana chama hicho mwaka 2005 kututawala tena) sio jambo linaloinyima CCM usingizi, chama hicho kimeanza kuonyesha dalili za udikteta tukirejea kauli zake nzito za hivi karibuni. Siku chache zilizopita, kiongozi mkongwe na miongoni mwa waasisi wa CCM,Kingunge Ngombale Mwiru,aliwakemea viongozi wa Kanisa katika lugha inayoweza kutafsiriwa kuwa ni ya kidikteta,alipoonyesha dhahiri kukerwa na kitendo cha viongozi wa dini kutumia uhuru wao wa kikatiba kutoa maoni yao kuhusu hatma ya taifa letu.Na sasa tunaambiwa kwamba chama hicho kimeamua kuwafunga midomo wabunge wake wanaojaribu kuwakemea mafisadi, sambamba na kunyamazisha kelele dhidi ya tuhuma zinazomwandama Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu.

CCM imefikia hatua ya kulitukana Bunge la Jamhuri ya Muungano na kulifananisha na kikundi cha vichekesho cha Ze Komedi.Jaribu ku-imagine kauli kama hiyo ingetoka kwa mtu kama Dkt Wilbroad Slaa au Zitto Kabwe! Ni dhahiri watu kama George Mkuchika, anayechanganya majukumu yake ya u-Katibu Mwenezi wa CCM na u-Waziri wa Habari, au Yusuph Makamba wangekurupuka na vitisho kuwa “wapinzani wanaikosea heshima Katiba ya Jamhuri.” Kulilinganisha Bunge na Ze Komedi kwa vile tu limejikongoja kuruhusu sauti zisizopendeza masikioni mwa mafisadi na watetezi wao ni kitendo kinachoashiria utovu wa nidhamu wa hali ya juu.

Bunge la Jamhuri ya Muungano ni taasisi nyeti na inayopaswa kuenziwa na kuheshimiwa na kila Mtanzania including hao wanaoifananisha na kikundi cha vichekesho. Kama unadhani kauli ya “Bunge ni mithili ya Ze Komedi” haina uzito, tafakari upya. Mtu anapokufananisha na mchekeshaji (comedian) anafikisha ujumbe kwamba hupaswi kuchukuliwa seriously. Kauli na matendo yake pia yanapaswa kuchukuliwa kama mambo yasiyopaswa kupewa umuhimu au kutekelezwa kwa vile ni ya “kusukuma muda” tu. Japo vichekesho vingi huwa na ujumbe uliofichika katika maneno au matendo ya kuchekesha, mara nyingi kauli au matendo hayo hayapaswi kuchuliwa seriously.

Kwa CCM kulifananisha Bunge na Ze Komedi inatueleza kwamba taasisi hiyo yenye jukumu la kutunga sheria za nchi haistahili kuchukuliwa serious katika kauli, maamuzi na matendo yake. Lakini hilo si geni kwa vile hata maamuzi ya baadhi ya kamati za Bunge, kama ile ya Mwakyembe, yameendelea kupuuzwa katika kile kinachothibitisha kuwa CCM imekuwa ikiliona Bunge kama genge la wachekeshaji,with exception of wabunge kama Kingunge,Serukamba,Mkuchika ,Lowassa,Rostam,Karamagi,Chenge na “wateule wengine wachache” wenye umuhimu wa kipekee kwa chama hicho.

La kusikitisha ni kwamba bado mamilioni ya Watanzania wenye akili zao timamu wataipigia kura CCM hapo mwakani irejee madarakani kuendeleza nyodo kama hizi.Na hicho ndicho kinawapa jeuri watu kama Mkuchika kusema lolote pasi hofu ya kukigharimu chama hicho ushindi hapo mwakani.CCM inajivunia knowledge yake kuhusu Watanzania kwamba ni kama wamezowea kupuuzwa (wao na baadhi ya wawakilishi wao wachache wanaopiga kelele Bungeni kutetea maslahi ya walalahoi),kunyanyaswa,kuburuzwa na kudanganywa kama watoto wadogo.

La kusikitisha zaidi ni namna uongozi wa juu (with exception of Makamba na Mkuchika wanaofahamika bayana wanaoelemea upande gani kati ya watetezi na wapinzani wa ufisadi) walivyo kimya japo kila siku wanasikika majukwaani wakiahidi Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Taarifa za vyombo vya habari kuhusu yaliyojiri kwenye vikao vya juu vya chama hicho zinatuthibitishia bayana kuwa uongozi wa juu wa CCM hauna dhamira ya dhati ya kukomesha ufisadi kwa vile badala ya kuwakemea wanaowakwaza wapambanaji dhidi ya ufisadi wanadaiwa kuleta ngonjera za “kujadili mambo ndani ya chama.”Yaani wanataka kutuambia hawajui kuwa ndani ya chama kuna watu kama Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo ambao kwa namna yoyote hawako tayari kuruhusu mjadala huru dhidi ya ufisadi kwa vile wao ni watuhumiwa?

Ungetarajia busara za watu kama Mzee Ali Hassan Mwinyi ziwafumbue macho CCM kwamba kuzuia demokrasia katika kujadili mambo yanayowakera na kuwaumiza Watanzania kutapelekea kifo cha mende kwa chama hicho. Lakini pengine wanafahamu nguvu za mafisadi ndani ya chama hicho, na hivyo kuhofia kuwaudhi katika kipindi hiki ambacho CCM inawahitaji mafisadi more than ever ili iendelee kututawala.Wanatupuuza kwa vile wanajua hatuna jeuri ya kuwaadhibu kwa madhambi yao.

They could be right, though! However, they fooled us in 2005.They possibly will fool us again in 2010, but let them rest assured that they will never fool us forever. They are simply buying time to finish digging their own graves.


1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.