19 Dec 2009


Ahadi za urais 2005 zamtesa Kikwete uchaguzi wa mwakani

Rais Jakaya Kikwet, mzigo mzito wa ahadi zake za mwaka 2005 unamkabili uchaguzi ujao 2010.
Na Mwandishi Wetu
MIEZI michache ikiwa imebaki kabla ya kuanza kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano, Rais Jakaya Kikwete anaonekana kukabiliwa na mzigo mzito wa kutekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za mwaka 2005.

Kikwete alipata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 baada ya kunyakua takriban asilimia 80 ya kura, akiwa pia ameshinda kwa kishindo dhidi ya wapinzani wake kwenye uteuzi wa mgombea wa CCM.

Lakini kadri muda unavyokwenda ndivyo umaarufu wake unaonekana kupungua huku tafiti mbalimbali zikionyesha kuwa umaarufu aliokuwa nao wakati akiingia madarakani unaendelea kuporomoka, ikiwa ni miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Wakati akizunguka sehemu mbalimbali nchini kuomba kura za wananchi, Kikwete alikuwa akitoa ahadi kem kem ambazo alizielezea kwa kifupi kwenye kauli mbiu yake ya “Naisha Bora kwa Kila Mtanzania” ambayo mkakati wake wa kuitekeleza ulikuwa ni “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya”.

Mbali na ahadi ambazo alikuwa akizitoa kwa wananchi kila sehemu alipoelezwa tatizo, ikiwa ni pamoja na matatizo sugu ya maji, miundombinu, huduma za afya na pembejeo, Rais Kikwete pia alitoa ahadi za ujumla kabla na baada ya kushinda uchaguzi kumrithi Benjamin Mkapa.

Baadhi ya ahadi hizo za Rais Kikwete kabla na baada ya kuingia madarakani ni pamoja na kuweka kipaumbele katika kilimo, akitumia kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, kupitia upya mikataba ya madini ili inufaishe nchi na wawekezaji, na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi wa elimu ya juu anayekosa masomo kwa kukosa karo.

Ahadi nyingine ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za umma, kuumaliza mgogoro wa Zanzibar, kuimarisha uhusiano wa kimataifa, kukomesha tatizo la ufisadi, kupambana na tatizo la uhalifu, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya na ujambazi, kuandaa mdahalo wa kitaifa wa michezo kwa lengo la kuinua michezo na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma....INAENDELEA HAPA

1 comment:

  1. Kaka Evarist
    Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
    Baraka kwako

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.