22 Mar 2010


Kiongozi shurti awe na msimamo na kisha asimamie kile anachoamini.Kwa mara nyingine,Rais Barak Obama ameithibitishia dunia kuwa ni 'mwanaume wa shoka' linapokuja sula la kuamini anachosimamia.Hatimaye jana Obama alifanikiwa kupitisha sera yake ya mabadiliko katika mfumo wa afya ya jamii nchini Marekani.Hiyo ni baada ya safari ndefu na ngumu pengine zaidi ya kampeni yake ya kuingia Jumbe Jeupe (White House).Pamoja na kuhatarisha nafasi yake na ya chama chake kisiasa,Obama alipigana kiume kuhakikisha kuwa lazima mabadiliko hayo yafanyike,kwa gharama yoyote ile.Na kama inavyofahamika,mara nyingi maamuzi ya kihistoria huwa na tabia ya kutokuwa maarufu. Ushindi wa Obama katika suala hili unapaswa kuwa fundisho muhimu kwa Rais wetu Jakaya Kikwete ambaye miezi michache ijayo atahitimisha miaka yake mitano tangu aingie madarakani.Sote tunafahamu,with exception ya wale wanaopenda habari nzuri tu hata kama ni za uongo,kwamba kwa kiasi kikubwa ahadi za Kikwete kuikomboa Tanzania kutoka kwenye lindi na umasikini imebaki kuwa hadithi tu huku ufisadi ukishamiri na kuitafuna Tanzania kwa kasi ya ajabu.Yayumkinika kusema kwamba utawala wa Kikwete utakumbukwa zaidi kwa skandali kuliko ufanisi wa kuwatumikia Watanzania.Kibaya zaidi,Kikwete alitoa lundo la ahadi kuhusu namna atakavyoboresha maisha ya Watanzania,hence kauli-mbiu MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Kuna wanaodhani kuwa kilichomsukuma Kikwete kuogmbea urais mwaka 2005 ni kukamilisha ndoto yake ya mwaka 1995 'iliyokwazwa' na Baba wa Tiafa Mwalimu Julius Nyerere.Wenye mtizamo huo wanaamini kuwa Kikwete alitumia miaka 10 iliyofuata akikusanya nguvu,sio katika namna gani atawatumikia Watanzania,bali atakavyoweza kuingia Ikulu.Ni katika 'piga ua' hii ndipo alijikuta akishirikiana na 'viumbe hatari' waliojipenyeza kwa kivuli cha 'wanamtandao' wakiwa na matarajio makubwa kuwa Kikwete akiingia Ikulu basi nao 'wameula'And they were not wrong.Kusuasua kwa Rais wetu katika kuchukua maamuzi mazito kumechangiwa zaidi na ushirika wake na watu hao.Na hii haiwezi kuwa excuse kwake kwa sababu alikuwa na kila sababu na uwezo wa 'kuwasaliti' laiti angekuwa na nia.Angeweza kabisa kuwaita Ikulu na kuwaambia 'nathamini sana mchango wenu kuniingiza madarakani,lakini mimi sasa ni Rais wa Watanzania wote ninayeongozwa kwa misingi ya Katiba.I'm sorry,atakayekwenda kinyume na sheria na taratibu za nchi basi sheria itachukua mkondo wake.Tubaki marafiki lakini sio kwa urafiki wa kukwamisha utawala wangu'.Simple and clear!

Tupo wengine tunaoamini kuwa licha ya ndoto hiyo iliyoanza 1995,Kikwete pia alisukumwa na dhamira ya kuwatumikia Watanzania.Na kututhibitishia kuwa tuko sahihi,alipoingia tu madarakani alitoa hotuba zilizoonyesha kuwa anafahamu kwa kina vikwazo vya maendeleo ya taifa letu.Aliweka wazi kuwa rushwa ni tatizo kubwa na angefanya kila awezalo kupambana nayo.Kama ilivyokuwa kwenye hotuba zake za wakati wa kampeni,Kikwete alipoingia madarakani alirejea kuahidi makubwa kwa Watanzania,na wengi tulimwamini kwa vile alikuwa akiongea lugha tunayoielewa (tofauti na Mkapa aliyezowea kutoa hotuba 'ngumu' kana kwamba ni mihadhara ya kitaaluma chuo kikuu).

Dalili ya kwanza kuwa Kikwete 'hana jipya' ni kauli yake kuwa 'anawafahamu wala rushwa bali anawapa muda wa kujirekebisha'.Nadhani kauli hiyo itaingia kwenye vitabu vya historia kama ya aina yake kwa mkuu wa nchi kutoa deadline kwa wahalifu.Lakini baadhi yetu tulijipa matumaini kwamba labda Rais alikuwa serious katika kauli hiyo,na kwamba baada ya deadline hiyo ku-expire angechukua hatua flani.Miaka mitano baadaye,sote tunafahamu sasa kuwa kauli hiyo ilikuwa mithili ya 'kumtishia mtu mzima nyau'.Na si kwenye kauli hiyo tu,bali tuliambiwa wakati flani kuwa amekabidhiwa orodha ya wauza madawa ya kulevya (na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Bakari Mwapachu) na baadaye tena akatuambia kuwa anawafahamu wala rushwa pale Bandari Dar es Salaam,na majina anayo.So far,hajachukua hatua kwa wauza madawa ya kulevya (wa orodha ya Mwapachu) na hajawasilisha majina ya wala rushwa wa Bandari!Sasa kama Rais hataki kutoa majina ya wala rushwa anaodai anawafahamu,tutegemee nini kutoka kwa mwananchi wa kawaida?

Kama nilivyosema mwanzoni mwa makala hii,uongozi ni kusimamia katika kile unachomini hata kama kitakupunguzia umaarufu.Kikwete alipaswa kufahamu kuwa ili urais wake uwe na manufaa kwa Watanzania ni lazima 'akosane' na baadhi ya marafiki zake.Na kwa hakika hilo lingekuwa na maana zaidi kwani ni bora zaidi mara milioni kupendwa na Watanzania walio wengi na 'kuchukiwa na mafisadi wachache' kuliko kupendwa na 'kigenge kidogo cha mafisadi' na kulaumiwa na mamilioni ya Watanzania.Kama Kikwete alikuwa na dhamira ya dhati ya kuwaletea Watanzania maisha bora alipaswa asimame kidete kuhakikisha hilo linatimia kwa udi na uvumba.

Lakini kwa vile bado kuna miezi kadhaa kabla ya uchaguzi,na kwa vile Obama ametioa darasa zuri kwa viongozi ya type ya Kikwete,basi tunabaki with our fingers crossed kuwa huenda rais wetu nae akajitutumua na kurekebisha mambo katika muda huu uliosalia.Uzuri ni kwamba hata kama ufisadi umetuumiza kwa muda wote huu,uamuzi wa kuukalia kooni katika dakika hizi za majeruhi utafanikiwa kufuta machungu yote tuliyopitia.Ni kama katika fainali ya soka ambapo bao la ushindi linapatikana katika dakika za majeruhi.Shamrashamra zitakazoambatana na ushindi huo hazitajali kuwa bao la ushindi limepatikana dakika za lala salama.What matters ni ushindi.

Basi Rais Kikwete tunatarajia sasa utafanya kweli.Utatamka bayana kuwa ile deadline uliyotoa kwa wala rushwa unaowafahamu ime-expire na kuamuru vyombo vya dola viingie ulingoni (yes,vimekuwa vikiwajibika baada ya ruhusa yako).Utakabidhi ile orodha ya mafisadi ya pale Bandarini ambayo watendaji wanaisubiri ili wachukue hatua zinazostahili.Utaifanyia kazi pia ile orodha ya 'wauza unga' ulokabidhiwa na Mwapachu.Utaamuru wamiliki wa Kagoda wawekwe hadharani na kuchukuliwa hatua zinazostahili.Ukiwa mwenyekiti wa CCM,utatambua kuwa uwepo wa Mzee wa Vijisenti kwenye Kamati ya Maadili ya chama hicho licha ya tuhuma zinazomkabili ni mzaha usiokubalika,na utashauri awekwe kando hadi taratibu za kisheria zitapochukua mkondo wake.Utaamua kuwa suala la Richmond haliwezi kumalizwa 'kishkaji' bali wahusika wote watachukuliwa hatua ili iwe funzo kwa wanaotumia madaraka yao vibaya.Na mwisho,utaanza kutafsiri kwa vitendo ahadi zako lukuki ulizotoa wakati wa uchaguzi na kuendelea kuzitoa kwa muda wote uliokuwa madarakani.Rejesha ari,kasi na nguvu mpya katika kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Kama Obama ameweza,wewe unaweza pia.It's all about kuamini unachosimamia na kusimamia unachoamini.

2 comments:

  1. Binafsi, napenda tupanue uigo wa suala na kuongelea ushindi wa Obama na fundisho kwa waTanzania. Ni kweli kuwa Obama anaweza kutoa fundisho kwa JK, lakini naamini fundisho kubwa zaidi ni kwa waTanzania.

    JK amekuwepo madarakani miaka kadhaa tu, na akipata kipindi cha pili atamaliza na kurudi uraiani. Wananchi walikuwepo kabla ya JK, wako wakati huu wa JK, na wataendelea kuwepo baada ya JK. Kwa hivi jukumu zito la kujifunza kutoka kwa Obama lazima liwe mabegani mwa wananchi.

    Ni yepi hayo ambayo waTanzania wanapaswa kujifunza kutoka kwa Obama?

    Kwanza tukumbuke kuwa Obama alikulia katika mazingira magumu, bila baba. Alifanya bidii kukabiliana na hali, akafanya bidii shuleni, na akaingia Harvard, ambako alipata heshima ya kuteuliwa mhariri wa jumuia ya wanafunzi wa sheria wa pale.

    Obama hakukaa akilalamikia hali ngumu, bali alikula kitabu. Hakukaa akingojea sera ya serikali, bali alijituma. Hakukaa akimlaumu rais wa Marekani, bali alijituma.

    Sasa fananisha na uzembe wa wa-Tanzania, ambao hawathamini elimu bali wanatafuta njia za mkato au dezo ili wapate vyeti. Wakishapata vyeti, na wazo la kusoma linaisha kabisa.

    Watanzania hawaoni sababu ya kujielimisha baada ya kupata vyeti. Wenyewe wanaita "kumaliza masomo," ambayo ni dhana ya ajabu, kwani masomo hayamaliziki.

    Watanzania wakisha "maliza masomo" hawako tayari kununua kitabu, labda kiwe cha udaku. Pesa wanazitwanga baa na kwenye sherehe. Huko hata malaki wanatumia.

    Obama ni nyota inayong'ara duniani kote, kwa jinsi alivyo na fikra, busara, na uwezo wa kujieleza. Watanzania hata kuongea na kuandika ki-Swahili wanashindwa, achilia mbali ki-Ingereza, amnbayo ndio lugha inayohitajika zaidi katika mapambano ya ulimwengu huu wa utandawazi.

    Leo hii, katika dunia hii ya utandawazi, wa-Kenya wanazidi kuingia Tanzania, na kujipatia ajira, kwa sababu wanao uwezo wa kujieleza. Ajabu ni kuwa hata kwenye kazi za kufundisha ki-Swahili huku ughaibuni, utaona wa-Kenya ndio wanazichukua zaidi.

    Kwa uvivu walio nao wa-Tanzania, hata kibarua cha kuhudumia vyumba katika hoteli kubwa pale pale Tanzania hawatapata. Kazi hizi watazipata wa-Kenya na wa-Ganda, wakati wa-Tanzania wanaendelea kukaa vijiweni, wakilumbana kuhusu Yanga na Simba, au wako kwenye vikao vya sherehe.

    Obama alijikwamua kutoka maisha ya utotoni ya kutokuwa na baba hadi amekuwa rais wa Marekani. Alitumia juhudi na maarifa. Watanzania hawana mpango wa kujikwamua. Muda wote wako vijiweni wanamnyooshea vidole JK.

    ReplyDelete
  2. Mzazi naona upo poa kabisa,,
    Mie ni mdau wako kutoka A town,comment yangu ni kuhusu hiyo post ya hapo juu wakati JK Akipokea hundi ya malipo....
    CQ Kwenye maneno imeandikwa TWO HUNRED THOUSAND Lakini kwenye Tarakimu ineandikwa 300,000.....
    jAMANI TUTAFIKA TUSIPOKUWA MAKINI NA VITU Vidogo vidogo kama hivyo..

    Asante sana Great S..

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.