22 Aug 2010

Blogu hii ya KULIKONI UGHAIBUNI inafungua ukurasa mpya na kuweka historia ya kipekee katika fani ya habari nchini Tanzania kwa kutangaza hadharani kuwa inam-endorse mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

Kuna sababu lukuki za kufanya hivyo lakini hapa nitaziorodhesha chache.Kwanza,blogu hii inataka kuachana na unafiki unaojidhihirisha katika baadhi ya vyombo vya habari vyetu ambapo wahusika wanadai hawafungamani na upande wowote lakini matendo yao yanawasuta kwa kupendelea chama tawala huku wakivibinya kwa nguvu baadhi ya vyama vya upinzani.Hapa simsimangi mtu bali nadhani ni vema kuweka msimamo wazi ili kama chombo cha habari ni wakala wa CCM na JK basi ni vema wasomaji wakafahamishwa bayana.

Pili,blogu hii inaamini kuwa kila Mtanzania mwenye uchungu wa dhati kwa nchi yetu anapaswa kumsapoti Dkt Slaa.Katika utumishi wake kwa umma,mgombea huyo wa Chadema ametuthibitishia kuwa ni mtetezi halisi wa haki za wanyonge na ustawi wa taifa letu.Ni nani asiyefahamu namna Dkt Slaa alivyohatarisha maisha yake kwa “kuwavua nguo mafisadi hadharani” alipotangaza ile “list of shame”?Walitishia kumpeleka mahakamani lakini hakuna mmoja wao aliyediriki kufanya hivyo,na sanasana baadhi yao wakaishia kuburuzwa mahakamani na serikali katika “kujikosha”.Blogu hii inaamini kuwa Dokta Slaa ni mkombozi na suluhisho mwafaka la matatizo lukuki yanayotukabili.

Tatu,binafsi naamini kuwa mgombea wa CCM,Jakaya Mrisho Kikwete,ameshindwa kabisa kutimiza matarajio ya Watanzania licha ya ahadi lukuki alizozitoa wakati wa kampeni zake mwaka 2005 na anazoendelea kuzitoa hadi leo.Ungetegemea kuwa mwezi huu wa toba Kikwete angemwogopa Mola wake na kutubu kwa Watanzania kwamba kuna maeneo mengi tu ambapo yeye na chama chake wamewaangusha Watanzania.Lakini kama ilivyo jeuri ya wanasiasa wengi wa Kiafrika,JK ameendeleza wimbo wa “mafanikio ya Awamu ya Nne”.Yani hata kushamiri kwa ufisadi na “uchakachuaji” wa kura za maoni ndani ya CCM ni mafanikio!

Sababu ya nne inashabihiana na hiyo ya tatu.Naamini kuwa afya ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,inapaswa kuwekwa kwenye darubini na wapiga kura wanapofanya maamuzi ya kumchagua rais wa awamu ya tano.JK ameshaanguka hadharani mara tatu na kila mara tunapewa excuse moja baada ya nyingine.Mwaka 2005 tuliambiwa “swaumu na uchovu wa kampeni”.Alipoanguka Mwanza tuliambiwa uchovu wa safari (kana kwamba safari hizo ni zile za Wamachinga wanaotembea juani kwa mguu!).Na jana kaanguka tena jukwaani halafu tunaambiwa sababu ni swaumu.Kwani Makamba hajafunga?Au Rais Karume naye “kobe”?Kuna tatizo zaidi ya swaumu au uchovu lakini kwa vile viongozi wetu wamezowea sifa na sio kasoro basi kuweka hadharani kinachomsibu kiongozi huyo inaonekana ni sawa na uhaini.Blogu hii imaanimi kuwa ili Tanzania ijikwamue katika lindi la umasikini wa kutupwa,sambamba na kukabiliana na janga la ufisadi,tunahitaji kiongozi mwenye afya timilifu,kimwili na kiakili.Hatujui JK ameshaanguka matra ngapi asipokuwa hadharani lakini haihitaji hata cheti cha short course ya utabibu kumaizi kuwa JK ana matatizo ya kiafya yanayofichwa,aidha kutokana na uoga wa wanaopaswa kuujulisha umma kuhusu hilo au maagizo yake mwenyewe kuwa “yuko fiti”.All in all,uzito wa matatizo yanayoikabili Tanzania unahitaji mtu aliye fiti kweli,na sio kwa anavyodhani yeye au anavyotaka umma uamini hivyo ilhali ni kinyume na hali halisi.

Kama nilivyoandika mwanzoni,kuna sababu nyingi zilizopelekea blogu hii kuamua kum-endorse Dkt Slaa lakini chache zilizotajwa hapo juu zinawakilisha hizo nyingine.Nawakaribisha ndugu zangu wa Chadema kuitumia blogu hii kufikisha habari kwa Watanzania pasipo hofu ya kuwa habari hizo zitachujwa,kuminywa au “kuchakachuliwa”.

Natambua bayana kuwa baadhi ya wasomaji wa blogu hii sio wafuasi wa Dkt Slaa au Chadema lakini napenda kuwakikishia kuwa endorsement hii haimaanishi kashfa,matusi,dharau au mambo yasiyofaa dhidi ya wagombea wa vyama vingine.Kuweka wazi msimamo wangu haimaanishi chuki dhidi ya vyama hivyo na wagombea wake bali ni imani yangu kuhusu nani anayeweza kuipatia Tanzania “uhuru wa pili” (mapambano dhidi ya Watanzania wenzetu wanaotafuna raslimali zetu zaidi ya alivyofanya mkoloni).

Mwisho,nawahamasisha bloga wenzangu na vyombo vingine vya habari kwa ujumla kuweka bayana misimamo yao ili kuepuka lawama zinazoweza kujitokeza pale habari za vyama flani zinaponyimwa fursa katika vyombo hivyo.Endorsement ya mgombea au chama ni jambo la kawaida katika nchi za Magharibi lakini hii ni mara ya kwanza kwa chombo cha habari cha Kitanzania kufanya hivyo,na kwa hakika najivunia kuweka historia hiyo.

13 comments:

  1. Hawa watu wa CCM hawataki kukiri kuwa safari hii wamemsimamisha mgombea mabaye afya yake inatia mashaka. Kama hawapo makini inaweza kuwapotezea watanzania imani.

    Matukio ya kuanguka kwa Kiongozi wetu, Mkuu wa Nchi yanatisha na kila mara sababu ni kama zinafanafa (Sukari kushika, swaumu, BP) nk. Huyu mtu ambae ana madaktari wake wa karibu (tofauti na watanzania wa kawaida) wanashindwaje kumpima kabla hajasimama jukwaani?. Hii ni fedheha kwa mataifa kuwa na kiongozi ambae hapatiwi huduma za afya za kiuchunguzi wa kina. Ni fedheha kuwa na wana usalama ambao wanashindwa hata kubaini afya ya Rais na kumsaidia mapema.

    SEHEMU YA PILI(Wakati anaanguka)

    http://www.youtube.com/v/0S2AE3xXR-Q..._embedded&fs=1

    SEHEMU YA MWISHO(Baada ya kuanguka)

    http://www.youtube.com/v/dJIemqlBK4Q..._embedded&fs=1

    ReplyDelete
  2. Afadhali angekufa si kuanguka. Ni ushirikina na madhambi yake ya kuwachuuza watanzania yanayomrudi. Malipo ni hapa hapa duniani. Namuombea afe haraka ili nchi yetu ikombolewe.

    ReplyDelete
  3. Inawezekana ameshachunguzwa sana nakupewa taarifa kamili ya afya yake lakini daktari hawezi kumlazimisha mgonjwa kupumzika. Mimi binafsi sina chama lakini nitampigia kura mgombea yule anayeonyesha uwezo na si vinginevyo. Nilimpigia kura Mkapa sababu niliamini aliosimamishwa nao wote hawakuwa wanampita kiwango cha uongozi. Na sasa nampigia Dr. Slaa kwasababu amenidhibitishia ana uwezo wakupewa mzigo wa uongozi kipindi chote alichokua mbunge. Hakuwa mtawala bali mtumishi wa wananchi. Amekuwa anapigania maslahi ya wananchi nakuweka maisha yake hatarini kwaajili ya Tanzania. Who else anaweza akainyooshea kidole CCM akiwa na evidence bila kuogopa? Asingekua Dr. Slaa nani angejua EPA na utajiri waliojilimbikizia wachache Tanzania? Nchi imeoza na nchi imeuzwa lakini Raisi bado anazungumzia mafanikio asioweza kuyataja takwimu zake. Amekua very general kama mtu asiyekuwa na taaluma yeyote. Viongozi wake wanafoji vyeti yeye anafumbia macho swala hilo. Hivi mtu atakua na cheti cha darasa la saba na cha computer alafu anakua mbunge. Mtu huyu anaweza kugundua mikataba halali na mibovu? Mtu huyu anaweza akachambua bajeti kweli? Mtuhumiwa wa mauaji ya albino kweli anapitishwa kwenye kura za maoni? Mtuumiwa wa ufujaji wa mali ya umma anapitishwa kwenye kura za maoni? Ukishatuhumiwa wewe haustahili uongozi wowote mpaka kesi yako imalizike vyombo husika vikusafishe. Huu ni uozo uliokithiri kwenye uongozi wa Raisi Kikwete. Raisi anachokizungumza hakiendani na anachokitenda. Ukiangalia viti maalum hakuna mwakilishi wa mkulima wala mfanyakazi. Nalazimika kusema viti maalum vimewekwa kwaajili yakutoa fadhila wanazozijua wao. Kama wanawake wengine kama Anna Tibaijuka wanaweza kugombania wakapata kura then viti maalum vinakazi hipi hasa???

    ReplyDelete
  4. Una mawazo mazuri,lakini hayana impact kwa kuwa wengi wa hao wanaosoma hizi habari kwenye mitandao si wapiga kura. Wapiga kura wapo vijijini. Tafuteni namna ya kuwafikia hao.

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa 16:47....
    Kuna redio stesheni nyingi tuu za masafa ya fm. Kimsingi zinaweza kuwafikia wananchi waliopo vijini hata sehemu zisizofikika kwa urahisi, kwa kuandaa vipindi maalum, kutoa maelezo na habari zilizojiri kwenye hizi blogu kama hii hapa ya ughaibuni kilichomo ndani yake, isipokuwa serikali iliyopo madarakani ukifanya hivyo kuna nafasi kubwa sana ya kituo hicho redio kuwekewa zengwe kwa namna nyingine ili kifungiwe...

    Mfano angalia gazeti la kulikoni lipo wapi sasa hata tovuti mwanakijiji hatujui ipo wapi sasa....eti sababu habari iliyoandikwa imeligusa jeshi la wananchi.

    Hivi jeshi la wananchi ndiyo chombo kilichoundwa na umma wa Tanzania. Hivyo kimsingi wananchi wana haki ya msingi kabisa kufahamishwa yanayotokea na kufnywa na jeshi hili yawe mazuri ama mabaya..

    ReplyDelete
  6. Mheshimiwa sana, Kulikoni Ughaibuni, nashukru kwa kujitolea katika hili la kum-support Dr. Slaa tuko pamoja, heshima mbele Mkuu. kama huoni shida badilisha hii background colour yako, rangi nyeusi haivutii na inaumiza macho. Natangulizua shukrani zangu. Tuko pamoja.

    ReplyDelete
  7. Rf anonymous 22:42....

    Additional point from that positive comment about the background display. Why don't you Ughaibuni blog come out with black fonts as well which will make much better and easier to read for us followers of your blog...Thanks

    ReplyDelete
  8. ok, umejitahidi kumpigia debe dk slaa. lakini unashindwa kufahamu kwamba jK Ameifanya tz kuwa nchi ya amani na utulivu.
    kumbuka kabla ya jk sasa hivi tulikuwa tukisia majibizano pamoja na kukimbizana kati ya polisi na wafuasi wa upinzani. lkn utwala wa jk mambo hayo hayapo kabisa.
    nakukaribisha kwenye
    www.jktu2010.blogspot.com

    ReplyDelete
  9. nchi ya amani na utulivu.
    kumbuka kabla ya jk sasa hivi tulikuwa tukisia majibizano pamoja na kukimbizana kati ya polisi na wafuasi wa upinzani. lkn utwala wa jk mambo hayo hayapo kabisa.
    nakukaribisha kwenye
    www.jktu2010.blogspot.com
    by malaria sugu wa jamiiforums

    ReplyDelete
  10. nchi ya amani na utulivu.
    kumbuka kabla ya jk sasa hivi tulikuwa tukisia majibizano pamoja na kukimbizana kati ya polisi na wafuasi wa upinzani. lkn utwala wa jk mambo hayo hayapo kabisa.
    nakukaribisha kwenye
    www.jktu2010.blogspot.com
    by malaria sugu wa jamiiforums

    ReplyDelete
  11. Reference anonymous 13:44 and 13:46.

    Sasa hapo ndiyo nimekubali kwamba tunasafari ndefu sana kupata maendeleo kwa maoni ya huyu mfuasi. Kimsingi mfuasi ina maana hata kitu ama jambo limekosewa wewe unalipaka rangi ya dhahabu.

    Kumjulisha tuu huyu bwana kwamba Tanzania hakuna amani ya ukweli isipokuwa wanasiasa wanaongea tuu majukwaani. Jambo linatokea ni kwamba wananchi wengi wananidhamu ya uwoga. Na uwoga huwa na kikomo chake. Nchi kama Somalia siyo kama iliandikiwa kufikia hapo ilipo.

    Narudia tena kama unaposoma vitu kwa vielelezo hakuna Nchi katika Africa iliyokuwa na Amani na uchumi imara zaidi ya nchi Ivory Coast. Hizi siasa ambazo wewe unazishabikia hivi sasa ndiyo ziliweza kuvunja amani katika nchi hizo. mwanamuziki wa muziki wa reggae anaitwa Alfa blondy alitengeneza album ya muziki ambayo ilikuwa inakemea hayo ambayo wewe unayoyashabikia.

    Wanasiasia wa dhalimu na mafisadi kma haw leo unaowashabikia wakazuia hiyo albamu kuingia sokoni na kuwekwa korokoroni, au kama leo Gazeti la kulikoni lilivyofungiwa au zito alipoitwa mwongo bungeni au kama vile Kampuni ya Kagoda inavyokkosa mmiliki au kama orodha aliyotoa Dr Slaa ya mafisadi ambayo wapo mtaani wanakula maisha kama wapo peponi.....

    Nimefikia mahali kuona kwamba ni kweli sisi tunaojiita watanzania hatuna utanzania ni dhahiri wananchi wa Taifa lingine. Nashindwa kuelewa neno uzalendo linamfahaa nani...huyu mtoa maoni amenichosha kabisa na uelewa wa watanzania ndiyo sababu leo rahisi anakutakana kesho anasema sikusema hivyo umeshindwa kunielewa.

    ReplyDelete
  12. lakini hata malaria sugu amefungiwa kwenye jamiiforums, media ya chadema huku wenyewe chadema wakijifanya ndio watetezi wakuu wa haki ya kutoa maoni

    ReplyDelete
  13. Anonymous 08:47......

    Vyama vingi vya siasa haina tofauti na mfumo huria wa biashara Mfano sekta ya biashara huduma ya simu, tulikuwa TTCL pekee siku za zamani na sasa tuna kampuni zaidi nne katika soko hili.

    Hivyo mfumo wa siasa wa wazalendo wa Tanzania hii ya leo inatakiwa pia huwe "fair and balance politcal opportunities" hii italeta ushindani katika utendaji wa vyama siasa. Tutaacha kuchagua viongozi wa serikalini wanaotokana na vyama vya siasa kwa sababu anatoka chama gani. Angalia hivi sasa inaonekana kwamba Dr Slaa ni tishio kwa Mgombea wa CCM.

    Sababu kubwa moja tuu binafsi inayompa DR Slaa fursa kubwa kutwaa kiti cha uraisi kwa sababu ya utendaji wake na uwajibikaji kamili bila ya porojo na siyo jina la chama chake cha Chadema, kama wagombea wengine wa kiti hicho cha urais.

    Maana yangu kwamba hata uwakilishi bungeni isiwe wa dominant kwa chama kimoja haitaleta tija na uwajibikaji kwa wabunge bungeni. Angalia wabunge wengine tangu bunge lianze kwa kipindi miaka zaidi kumi amekuwa mmbunge bila kuulizwa swali...Je hii kweli inaingia akili!!!!?. Hivyo zana domination wabunge kutoka chama kimoja tuu cha siasa inaharibu kabisa maana ya bunge.....

    Hivyo nategemea kama ni mtu mwenye akili timamu na pia iwapo Mzalendo wa Tanzania utakuwa umeelewa. La sivyo itakuthibitishia kwamba wewe ni mzalendo wa jina na siyo kutoka moyoni kwa sababu hupo tayari kusaliti wazalendo wenzako kwa sababu ya chama cha siasa

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.