25 Aug 2010


Hongera nyingi kwako Mzee wa Changamoto Yetu kwa blogu yako kutimiza umri wa miaka miwili.Ama kwa hakika blogu yako ni miongoni mwa sehemu zinazofanya kuweko mtandaoni kuwa ni jambo la muhimu katika maisha yetu ya kila siku.Hekima na filosofia zako zinaamsha tafakuru kubwa,huku ukihakikisha tunamwayamwaya na burudani ya miziki mbalimbali.Kwa hakika,Changamoto Yetu ni miongoni mwa sababu zinazonifanya niendelee kupenda fani ya kublogu.

Kila andiko lililowekwa kwenye blogu yako katka kipindi hiki cha miaka miwili kimekuwa na manufaa makubwa kwa jamii.Ni dhahiri kuwa kila unapoandaa andiko la kuweka bloguni hapo unakuwa na picha ya sie wasomaji wako akilini na hivyo kufahamu maswali,kiu,mshawasha,na matamanio au mahitaji yetu mengine.

Kukupa sifa unazostahili inahitaji chapisho kubwa zaidi ya thesis ya PhD.Naomba pongezi hizi fupi ziwakilishe stahili zako zote kutokana na kazi mwanana unayoifanya kwa jamii.

Again,Hongera Sana na Happy Birthday.

1 comment:

  1. Kaka.
    Sina ninaloweza kusema juu ya UWEPO WENU katika harakati hizi.
    Kama unakumbuka tuliwahi jadili namna ambavyo MAONI hayana maana kwetu tuandikapo YAIFAAYO JAMII
    Na hili naliona hata hapa. Mara zote unaandika na bado hujali wamesema nini. Kwani wajua TUNASOMA NA KUELIMIKA.
    Tambua kuwa CHANGAMOTO YETU ipo na INASIMAMA IMARA KWA KUWA KUNA CHAMBUZI ZILIZOJAA HAPA ZIONGEZAZO UCHAJI WA FIKRA.
    Ninaheshimu, Ninapenda na Ninathamini saaana kazi zako.
    SHUKRANI SAANA KAKANGU NA HESHIMA KWAKO

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.