12 Aug 2010

Baada ya kimya cha miaka miwili na mwezi mmoja hatimaye nimerejea katika ulingo wa uandishi wa makala zangu za Raia Mwema Ughaibuni katika jarida maridhawa la Raia Mwema.Haikuwa rahisi kwangu kukaa kimya huku nchi yetu ikiteketezwa na mafisadi lakini ililazimu kuwa hivyo ili kujipanga upya.

Katika makala ya wiki hii nimeelezea kwa kifupi kilichonisibu hadi nikafikia uamuzi wa kusitisha uandishi wa makala hizo.Basi nisikupunguzie uhondo bali bonyeza kiunganishi kifuatacho usome habari na makala nyingine motomoto katika jarida makini la Raia Mwema pamoja na makala ya wiki hii yenye kichwa MASLAHI YA UMMA NI ZAIDI YA VYOTE.

5 comments:

  1. Kwanza nakupa pole kwa maswahibu hayo yaliyokupata Dr Chahali.

    Pili nakupongeza kwa kutumia fursa yako vizuri kwa kupata elimu kwa gharama za fedha za walipa Kodi wa Tanzania.

    Tatu tunahitaji watu kama wewe wanaofahamu jinsi ya kutoa shukrani ya kulipiwa gharama za elimu yao, kutokana na fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa vitendo tena halali.

    Nne Kutumia taaluma yako kwa njia mhafaka na sahihi kama hitaji la watanzania kwa sasa kuelewa elimu ya siasa na pilika pilika za shughuli za kiraia kwa kina.

    Tano kumbuka kuwa kwa kipindi hicho chote ulichokaa kimya na kuwapa ushindi wanaoshabikia shughuli za kiahalifu kimewagharimu walipa kodi wa Tanzania mambo mengi...vifo, majeraha ya kudumu kama vile ulemavu, raia wasiokuwa na hati kupelekwa gerezani na mengine mengi yenye matokeo sifa za tawala zisizozingatia utawala wa sheria.

    Na mwisho kwa maoni haya ni kwamba umehamua jambo sahihi kabisa kutusaidia sisi watanzania wenye kuhitaji mchango wako katika Taifa hili kabla halijaangamia katika vurugu na vita.

    Kimsingi, unapozungumzia nchi zilizowahi kuwa na amani, utulivu hali ya juu kabisa na uchumi imara katika bara la Afrika ni Ivory Coast ambayo Tanzania haijafikia kiwango hicho hata chembe.

    Siasa zinazoshabikiwa sasa hapa Nyumbani Tanzania ndiyo ilipofikisha Ivory Coast leo kuwa nchi yenye amani tata na uchumi mmbovu.

    Kwa hiyo uchofanya hivi sasa Dr, ni sahihi kabisa kabla mambo kuwa mabaya zaidi. Okoa Tanzania yetu tunayoipenda kabla ya kuangukia kwenye vurugu na vita.

    God Bless

    ReplyDelete
  2. Asanteni sana La Princessa,Reverend Kitururu na Anonymous wa 17:43.

    ReplyDelete
  3. jus dropping by to show some love.usisahau kupitiapitia laprincessaworld.blogspot.com!!!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.