20 Oct 2010


Baadhi ya wazazi wa watoto wanaugua ungonjwa wa malaria wakiwa nje ya Kituo cha Afya Nyamongo Wilayani Tarime

Anthony Mayunga, Tarime

KITUO cha Afya Nyamongo wilayani Tarime hakijapata dawa ya mseto inayotibu malaria kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sasa.

Tatizo hilo linakwenda kinyume na kampeni za kupambana na malaria kwa kuwatibu wagonjwa ambayo inasisitiza kwamba Watanzania watapata vyandarua na dawa sahihi za kutibu malaria.

Uchunguzi wa uliofanywa na Mwananchi katika kituo hicho kilichoko katikati ya eneo la mgodi wa dhahabu wa North Mara ,ulibaini ukubwa wa tatizo hilo na wananchi kuonyesha kukata tamaa juu ya
mikakati inayonadiwa na viongozi kutokomeza malaria nchini. Marwa Ryoba mkazi wa Nyangoto alisema wanalazimika kutumia dawa za krolokwini,metakefilini na SP ambazo zilikwishapigwa marufuku na serikali kwa kushindwa kutibu ugonjwa huo.

“Tunashangaa ahadi na tambo nyingi za serikali kuwa watatokomeza malaria wakati hatupati dawa , hivi kupewa vyandarua na Wamarekani bila dawa inatusaidia?”alihoji kwa uchungu.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dk George Marwa alikiri kuwa hawajapata
dawa mseto licha ya kutoa taarifa kwa zaidi ya miezi mitatu. “Hapa tunapambana na matatizo makubwa maana jamii haijui tatizo la Msd badala yake lawama zinaelekezwa kwetu,maana kama hakuna Alu unadhani huko wanatumia nini,”alisema. Kuhusu kadi za kiliniki hakuna na wajawazito na wenye watoto
wanalazimika kununua mitaani inadaiwa wananunua Sh2,000= maana hatuna,na hilo linawakatisha tamaa wasiokuwa na fedha kuhudhuria
kiliniki.
“Hapa tunahudumia zaidi ya watu laki moja kutoka kata zaidi ya nne za Tarime na Serengeti, glovu unapewa pc 50 kwa miezi mitatu ,wakati hizo ni kwa wiki moja,wanalazimika kununua, na ni tatizo la mfumo.

Awali mwanamke aliyekutwa katika kituo hicho akisubiri huduma jina tunao ,alisema kuwa wanachofanya ni kwenda kuandikiwa tu kisha wanakwenda kununua dawa kwenye maduka ya watu ambao pia si wataalam.
“Wengi tunatumia panadol wakati unaumwa malaria na hata kwa watoto
,matokeo yake panapotokea vifo inakuwa vigumu kujua nini tatizo ,maana wapo wanaoishiwa damu, lakini tunashindwa watibiwe na nini,”alisema.

Alikwenda mbali na kudai kuwa matatizo ya wananchi kwa huduma za afya yamegeuka kuwa mtaji kwa wanasiasa wanafiki,kwa kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki,”suala la dawa limeshindikana sasa wanadai malaria
itakuwa historia kwa kuua ama nini?”alihoji kwa masikitiko.Baadhi ya wajawazito na wenye watoto waliokuwa hapo kituo
cha afya walisema mbali na dawa ya malaria pia wanalazimika kununua kadi na glovu kwa kuwa hazipatikani hapo kituoni .

“Pembeni wanasema huduma kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano bure ,lakini hapa tunanunua dawa,mipira ya mikononi(Gloves)na kadi za kiliniki,wengi wanajifungulia majumbani na hawaleti watoto
kiliniki akiugua malaria wananunua panadol na dawa za kienyeji,”walisema.

CHANZO: Mwananchi

NAAMINI TATIZO LA KUDAIWA MALIPO KWA HUDUMA ZINAZOPASWA KUTOLEWA BURE NI KARIBU KILA MAHALI NCHINI.NDIO MAANA CCM HAWATAKI KUSIKIA AHADI YA CHADEMA KUHUSU  ELIMU BURE.

6 comments:

  1. Bila shaka umetumwa na akina Chahali wewe uichafue serikali yetu tukufu. Lakini unasahau au hujui kuwa zahanati za wilaani zinahudumiwa na halmashauri za wilaya na ndizo zinazotoa pesa kulipa kwa boharia mkuu wa madawa kuweza kupatiwa mgao wa dawa. Sasa kama halmashauri yenu ina daktari fisadi, yeye akipata mgao anaupeleka dukani kwake na hapo kunaonekana upungufu wa dawa au vitendea kazi. Amka anza kubanana nao huko wilayani kabla ya kulaumu serikali. ahadi zipo na zinatekelezeka nyie kama munawaachia mafisadi watafune kasma yenu ni juu yenu itakula kwenu

    ReplyDelete
  2. Laiza nenda darasani kajifunze vitu vinne ambavyo ni Management and leadership, na pia Accountability and Responsibility sijui tafsiri sahihi ya kiswahili katika haya mambo niliyotaja. Haya ni mambo ya msingi sana na makubwa katika kuelewa maana ya serikali na uongozi wa umma. Na hizi makala za Bwana Chahali...Utaposoma na kuelewa hayo mambo yalitajwa hapo juu. Nakupa ushauri uanze kusoma makala za Bwana Chahali...Kimsingi hivi sasa wewe unazielewa nyuma mbele, na siyo mbele nyuma

    ReplyDelete
  3. Pole anonymous...huenda mimi nazisoma kikuruani kulia kushoto...na siyo kushoto kulia. ati darasa la management and leadership ndiyo litaniconvince kuwa ahadi za serikali hazitekelezeki pale dawa zinapokosekana tarime.bwana mdogo, unakokwenda ndiko nilikotoka...nina umri wa miaka 53 sema hamsini na tatu...nimesoma na nina shahada ya pili ya sayansi ya fedha...rejea government gazette utaniona nimesajiliwa...naongea kwa takwimu na siyo kumfurahisha chahali na wewe....mnataka kutudanganya kuwa nabii amekuja tuwafuate jangwani mtuache bilka maji...hatudanganyiki...ngoja niendelee kuzisoma nyuma mbele nawe zisome mbele nyuma...tutafika tu,,,wewe mpinzani mimi mtetezi wa serikali na chama tawala...

    ReplyDelete
  4. Laiza, Inawezekana unavyo vyeti isipokuwa hauna uwezo wa kuelewa vitu kwa kina na hasa kama umepata hivyo vyeti kifisadi....Tena wewe ni miongoni waliosoma elimu ya bure mpaka chuo kikuu...Mimi elimu yangu ni ya juu zaidi yako. Mimi mtanzania kwa asili, nimesoma mpaka darasa tatu bure nikiwa bado Tanzania baada ya hapo nikaenda ughaibuni. Na hivi sasa nina Phd mbili hivyo nategemea nimekuacha nyuma sana kielemu na ubunifu. Nina miliki na kuendesha biashara binafsi kubwa tuu huku ulaya. Siwezi kutaja umri kwa sababu nitakuwa natoa identity yangu. Nadahni sasa utakuwaumelewa.

    ReplyDelete
  5. Kama unamiliki biashara ughaibuni na una PHd mbili kelele za nini huku kwetu? pilipili twala siye wewe zakuwashiani...Umeshindwa kutaja umri kwa kuelewa kuwa nakuacha mbali hivyo falsafa zako haziniikngii hata kwa robo thumni.Kizuri zaidi ni kuwa daima unakwenda kwa identity ya anonymous kwa sababu...unakaanga mbuyu ili wenye meno tutafune...tukivunja meno yetu...uko ughaibuni unamiliki biashara kuuuubwaaaa...big up

    ReplyDelete
  6. Laiza,Hii sababu tosha kwamba elimu yako uliyofuzu ni ya kifisadi animation,copy and paste style...Umeshindwa kuelewa kama nimeandika kiasili ni mtanzania ina maana gani!!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.