22 Dec 2010



Picha kwa Hisani ya Mjengwa

Japo haipendezi kuona jeshi la polisi likitumia nguvu kubwa kuzuwia haki ya kikatiba ya wananchi kuandamana au kugoma kwa amani,lakini nashawishika kutowaonea huruma wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kufuatia kichapo walichopewa na askari wa FFU.Hivi sio hawa wana UDOM waliochangisha fedha kwa ajili ya kampeni za Jakaya Kikwete?Na sio hawa waliotoa tamko la kukemea haki ya kikatiba ya wabunge wa Chadema kususisa hotuba ya Kikwete huko Bungeni?

Najua si vyema kutoa lawama za jumla kwani si kila mwana-UDOM aliafiki wazo la kujikomba kwa Kikwete lililopelekea wanafunzi hao kuchangia fedha zao za ngama ili kumwezesha mwanasiasa huyo aliyekuwa mgombea wa CCM arejee madarakani.

Na kama tulivyoandika baadhi yetu wakati wa kampeni za uchaguzi wakati tunaonya madhara ya kuirejesha CCM madarakani,haijachukua muda kwa  Kikwete na serikali yake kuwalipa fadhila wasomi hao wa Dodoma.

Majuzi nilimsuta mwanahabari mkongwe Dunstan Tido Mhando baada ya kupata taarifa kuwa serikali imemtosa ubosi wa TBC.Nilimsuta kwa vile naamini wakati Tido anaombwa na WALIOMUOMBA kuja kuendesha TBC alikuwa anafahamu fika kuwa aidha anapanda mchicha au bangi,na mavuno yangekuwa mchicha au bangi,respectively.Ukikubali kutumiwa lazima ukubali kitachotekea itapojiri "expiry date" yako.

Sasa tunashuhudia kundi jingine la walioingizwa mkenge.Hawa wasomi watarajiwa wa UDOM walijikomba kwa Kikwete na CCM na kuchangia kampeni zake,sijui wakitarajia kuwa pindi mwanasiasa huyo akirejea Ikulu angewapatia muujiza gani sijui!

MLIPANDA BANGI SASA MNATARAJIA KUVUNA MPUNGA?

5 comments:

  1. Mr Evarist, I have been a keen reader of your blog and used to agree with you with most of the views you expressed. However, since the election it seems you have lost your way. Firstly, your piece about church burning in Zanzibar, I don’t agree with any of the actions by the people but reading from it you seem to lay blame on the religion and not the people, and the picture before the story was of people praying, you accepted it was wrong that the picture is not related to the piece and you will remove it but you did not. Secondly, this story about Udom strike, my sister is studying there and she has no political affiliation with any party apart from concentrating with her studies, am worried about the violence and what will happen to her as she spend most of the time locked in her room to avoid the troubles. And opening your blog what I see, blaming all students that they are CCM followers, it really made me sick. You admit not all students were involved in the donation but you still support FFU actions. So what do you want, because some students favoured CCM during elections, some of them should not fight for their rights to express their views? No matter what happen before election, no matter who they supported, everyone has a right to demonstrate peacefully. I know you did not support JK for presidency but I was surprised when you applaud when one of your Tabora Boys buddies who got deputy minister job, this was one of the signals that you are deluded. I know you hate JK because whatever happens to him you have a negative view, even a tyre puncture, but you were happy about his decision to appoint one your school mates. What is it then, are you expecting he is going to slot you in one of the departments.
    Am using Anonymous because I dont have time to register for all the option.

    Mohammed,Glasgow

    ReplyDelete
  2. Japo in uvunjaji wa haki za binadamu, kichapo cha UDOM big up. Maana ni jana tu hawa jamaa wa UDOM walifikia kiwewe hadi kumchangia JK achukue fomu za kugombea urais ili awapige na wasijue. Tuliwaonya kwa usomi nepi upogo na kujipendekeza wakatuona wabaya. Sasa wanalia na nani? Hiyo ndiyo CCM na huyo ndiye kipenzi chao waliompenda hadi kumchangia pesa ya kuchukulia fomu. Amewapenda sana hadi akawashushia kichapo cha mwizi. Asiyejua maana haambiwi maana na akiambiwa maana hajui maana.UDOM hayo ndiyo malipo ya usaliti na kutumia matumbo kufikiri badala ya vichwa. HONGERENI kwa kupata kichapo na bado. Wakati mnachapwa kwa kudai pesa wenzenu wanauziana mashangingi yatokanayo na pesa ya kodi ya wazazi wenu kwa laki tatu tu!Jifunzeni kufikiri na msome na kuelemika na si kupoteza muda madarasani.

    ReplyDelete
  3. Mkuu Mhango,you said it all.

    Mr Mohamed,I must admit my wrong doing.I had promised earlier that I would have changed the picture that accompanied my post on church building burning in Zanzibar,but I'm yet to fulfill the promise.Rest be assured that I will.

    As to my blanket finger pointing to UDOM student,I must again admit that there was a sentence missing,unintentionally,in which I intended to single out those who didn't support what I still regard as acts of political naivety by some UDOM students to raise funds for JK.

    However,I do not see myself as being deluded after supporting my ex-Tabora Boys' classmate who was recently appointed a Deputy Minister.If you read the congratulatory message objectively,you surely would have noticed that I was focusing on my classmate and not the person who appointed him.A dictator appointing a family member to hold some high profile post does not make them a good dictator.In similar way,my friend being appointed a deputy minister has not in anyway whatsoever changed my stance on JK as a president.Let me be very clear.I have nothing personal against Jakaya Kikwete the person but I have serious reservations about Jakaya Kikwete the president.I believe any sensible Tanzanian should too ( and the recently published WikiLeaks report in The Guardian only helps to cement such reservations).

    I take it your assumption that I might be expecting an appointment by JK as a bad joke.I dont have any political ambitions as I'm quite content with what I'm currently doing.

    ReplyDelete
  4. LEAVE DE PLANT ALONE MAN, AFADHALI WANGEPANDA BANGI HAPO BONGO, AKILI ZIMELALA INABIDI ZIAMSHWE, LET THE PLANT GROW MAN.

    ReplyDelete
  5. (Mohamed Glasgow) water hell on earth that you are living.....Kuona siyo kutambua....This is a major issue facing majority of black people as whole....

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.