20 Feb 2011


Tunaendelea kuwaletea updates za tukio la milipuko ya mabomu jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,hadi sasa inakadiriwa zaidi ya watu 20 wamepoteza maisha katika tukio hilo.

Tovuti ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC) Idhaa ya Kiswahili inaripoti:
Hali ya taharuki imetanda mji wa Dar Es Salaam, nchini Tanzania, huku wakaazi wakiamka kuomboleza vifo vya zaidi ya watu kumi na zaidi ya wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea kwenye ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi, lililo karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege.

Wakaazi wa eneo la Gongo la Mboto lililo karibu na ghala hilo wamekesha nje baada ya makaazi yao kubomoka kutokana na mtikisiko wa milipuko hiyo iliyodumu kwa saa kadhaa. Milipuko hiyo ilisikika kwa umbali wa zaidi ya kilomita ishirini kutoka kituo hicho cha kijeshi.

Inaarifiwa kuwa milipuko hiyo ilianza mwendo wa saa mbili usiku.

Msemaji mmoja wa jeshi amesema kuwa kuna watu wengi ambao wamepoteza maisha yao lakini idadi kamili haijajulikana.

Kamanda wa polisi jijini Dar-es-Salaam, Suleiman Kova, ametoa wito kwa raia wa mji kuwa huo watulivu huku maafisa wa ulinzi wakiendelea na mikakati ya kurejesha hali ya uthabiti.

Kova amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mlipuko huo ni ajali na wala sio shambulio la kigaidi.

Ni hii mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita mwaka wa 2009 zaidi ya watu ishirini waliuawa na wengine 300 kujerihiwa

Kadhalika,Rais Jakaya Kikwete amewaasa wananchi kuepuka maelezo ya "redio mbao" na badala yake wasubiri taarifa rasmi kutoka serikalini na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).Hata hivyo inawezekana Kikwete hajajiuliza kwanini wananchi wanategemea taarifa za "radio mbao" kwani ni dhahiri kuwa penye ombwe la taarifa rasmi,wananchi wanalazimika kugeukia vyanzo vya habari visivyo rasmi.



Hadi muda huu,hakuna kiongozi yeyote aliyewajibika au kuwajibishwa.Watanzania wanatarajia kuona Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo,Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo,wakiwajibishwa mara moja.Lakini kwa namna tunavyofahamu udhaifu wa Rais Kikwete katika kuwashughulikia watendaji wake,kuna uwezekano mkubwa wa Dkt Mwinyi,Mwamunyange na Shimbo kuendelea na madaraka yao

Kilicho wazi ni kuwa serikali itapoteza fedha za walipa kodi kuunda tume kama ile ya milipuko ya Mbagala mwaka 2009,na kisha ripoti ya tume hiyo kuishia kuwa karatasi za kufungia vitafunio.

Japo hakuna anayetaka kutumia janga hili la milipuko kama mtaji wa kuwahukumu watawala wetu,lakini kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha matukio yaliyopita na tukio hili na uwajibikaji duni wa serikali iliyopo madarakani.

Ni muhimu pia kutafakari dhamira ya serikali kuilipa kampuni ya kitapeli ya Dowans,sambamba na mpango wa kuwapatia wabunge shilingi bilioni 90 kila mmoja,huku mipango endelevu ya kuepusha na kukabiliana na majanga ikipuuzwa.

Ukweli ulio bayana ni kwamba serikali ya Kikwete na CCM yake haisumbuliwi na hali ya kutokuwa na uhakika na usalama wa wananchi.

Endelea kutembelea tovuti hii kwa habari na uchambuzi zaidi kuhusu tukio hili la kusikitisha.

4 comments:

  1. Vipi kulikoni ni vidole vimeteleza au kwani tarehe zinanyesha za mwaka jana wakati tukio ni la leo,

    ReplyDelete
  2. saw kaka ila tufahamu kuwa swala la kufanya maamuzi au kutoa taarifa na kuwawajibisha wahusika huwa kwa tanzania hii ni ngumu saana,
    hebu fikri wazungu na watalii qwangapi yaliwakuta haya au kushudia milipuko au matetemeko haya??
    je wataenda kueleza nn nnchini kwao kuhusu amani ya Tanzania??
    Je waliokuwepo jana uwanja wa ndege bila kuwepo taarifa zozote za safar je unaona wamekwazika kiasi gani???
    m,mmmhh je mabomu yaNGELIPUKA WAKATI klm INAtua ingekuwaje???

    naona kikwete ana PLANT THE SEED OF HIS OWN DESTRUCTION

    ReplyDelete
  3. Kwa mara ya kwanza nimepata fursa ya kutoa maoni kwenye UWANJA MPYA.
    Na nimetoa maoni baada ya KUWA KIMYA KWA MUDA MREFU kwani niliamini kuwa kusema kitu huku nikiwa na hisia kungeniumiza ama kuwaghafilisha wasomaji wangu.
    Kinachotakiwa kubadilika ni MFUMO kwani ndio unaotupa viongozi wasiojali.
    Kama nilivyonukuu kwenye Blogu yangu "If we don't change our values and re-arrange our systems, we'll always gonna be another victims......"

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.