26 Sept 2011


Wajuzi wa mambo wanadai kuwa moja ya mambo yanayopunguza ufanisi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni tabia iliyoota mizizi ambapo kila kigogo anataka kumpatia mwanae,mpwae,mtoto wa rafiki yake,nk katika ajira ya taasisi hiyo nyeti.Haina ubaya kutoa ajira iwapo mwajiriwa mtarajiwa atakuwa na sifa husika.Lakini uzoefu umeonyesha kuwa kanuni na taratibu zinabemendwa makusudi ili ajira hizo ziende kwa watu wa karibu wa vigogo hao.

Kibaya zaidi ni ukweli kwamba wengi wa watoto wa vigogo wanapopata ajira kwenye taasisi kama hii ambayo msingi wake mkubwa ni uzalendo wa mtumishi husika hujiona kama 'untouchables' flani,wanafanya mambo wapendavyo,usumbufu mtaani kwa zile 'unajua mimi ni nani/nafanya kazi wapi' huku bastola zikiachwa zionekane waziwazi kama Aden Rage.Wengi wa hawa vijana hawafahamu jukumu kubwa walilonalo kwenye kila sekunde ya uhai wa Mtanzania.Don't get me wrong kuwa ninajifanya kuelewa sana mambo haya lakini ukweli ni kwamba taaluma ya ushushushu ni uti wa mgongo wa uhai wa taifa lolote lile duniani.Idara ya Usalama ya nchi ikiyumba,nchi nayo inayumba.Watu wengi hawaelewi umuhimu wa chombo hiki kwa vile kimaadili kinapaswa kufanya kazi zake kwa siri,japo watoto wa vigogo wanaona usiri huo kama kero.

Anyway,nimekutana na tangazo la ajira za ushushusu katika 'Idara ya Usalama' (wa ndani-yaani ya kuzuia ujasusi) ya Uingereza-MI5 au kwa kirefu Military Inteligence,Section 5)-ambalo limewekwa kwenye gazeti la bure la kila siku la METRO.Utaratibu huu ambao sitarajii kuuona ukiigwa na taasisi nyingi za usalama duniani,achilia mbali yetu,unaweza kusaidia sana kufanya zoezi zima la kuajiri (recruitment process) kuwa ya huru,wazi na inayowekea mkazo uwezo,ujuzi na sifa za mwombaji kazi (based on merit(s)).

Hii ni mada nyeti kwahiyo naomba niishie hapa.Ukiwa na swali,usisite kuniuliza (majibu yatategemea swali limeulizwaje).

4 comments:

  1. Mr. Evarist: its true kutokana na yote uliyoyasema... lakini kwa Tanzania taifa letu, nahisi hawapo kwaajili ya Usalama wa taifa ama Usalama wa nchi....... labda ni kwa faida zao binafsi. na je kuna vigozo gani unapotaka kuomba nafasi ktk usalama wa taifa.....??? samahani ningeppenda unijibu inbox kwa E-mail [email protected]

    ReplyDelete
  2. vigezo gani vinahitajika kujiunga na TISS na hata gani [email protected] naomba majibu

    ReplyDelete
  3. jamani mi naomba kujua taratibu za kujiunga na jwtz na sio JKT kwani sasa tayari nimamaliza masomo yangu ya mambo ya securities katika nyanja ya IT AU ICT (TEHAMA) Hivo naomba mwenye uwelewa na hili anaisaidie kwani watu kama sisi tunahitajika sana katika kulinda amani katika TANZANIA yetu hivo tunomba kama kuna mtu anaejua utaratibu juu ya hayo mambo naomba ajitaidi anaiunganishe na hao watu hivo ningependa kusaidiwa na hao watu na niko tayari kwa ataew2eza kunisaidia nami nika mssaidia hata kimawazo.
    NIMESOMA HAYA MAMBO
    NETWORK AND SYSTEM ADMINISTRATION NA PIA NIMESOMA ETHICAL HACKING NA INFORMATION SYSTEM MANAGEMENT.

    ReplyDelete
  4. News nzuri zenye kujenga na mafundisho mazuri ktk kuiletea nchi Amani ya kweli

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.