30 Oct 2011




BLOGU HII INAPENDA KUTOA SALAMU ZA HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA JARIDA MWANANA LA RAIA MWEMA AMBALO LILIZALIWA SIKU KAMA YA LEO MIAKA MINNE ILIYOPITA.

BINAFSI,JARIDA HILI NI KAMA SEHEMU YA MAISHA YANGU.TANGU WAHUSIKA WANIPATIE NAFASI YA KUANDIKA KATIKA JARIDA HILO KWWENYE SAFU YA TAIA MWEMA UGHAIBUNI NIMEKUWA NIKISHIRIKIANA NAO HATA NJE YA FANI YA UANDISHI.NILIPOUGULIWA NA MAREHEMU MAMA MWAKA 2008 NA HATIMAYE ALIPOFARIKI,WAHUSIKA WA JARIDA HILI WALIKUWA NAMI BEGA KWA BEGA.

NAKUMBUKA VIZURI SIKU NILIPOZURU OFISI ZAO KWA MARA YA KWANZA NA JINSI NILIVYOPOKELEWA KANA KWAMBA SOTE TULIKUWA TUKITANA HAPO OFINI KILA SIKU YA WIKI.

LAKINI KUBWA ZAIDI NI MCHANGO WA JARIDA HILI KWA JAMII.LICHA YA HABARI ZAKE MAKINI JARIDA LA RAIA MWEMA LIMEJIJENGEA SIFA KUBWA KWA KUWA NA MAKALA ZINAZOANDIKWA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU NA LIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA 100 KUTOELEMEA UPANDE WOWOTE ZAIDI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA SAUTI YA WASIO NA SAUTI.

NAJISIKIA FAHARI KUBWA KUWA MIONGONI MWA WANA-TIMU WA JARADA HILI,NA NI FURAHA KUBWA KUONA RAIA MWEMA LIKITIMIZA MIAKA MINNE HUKO LIKIZIDI KUPAA KWA KUAMINIKA KATIKA JAMII NA KUENDELEA KUUTUMIKIA UMMA KWA UADILIFU.

KWA MARA NYINGINE TENA,NA KWA NIABA YA WASOMAJI WA BLOGU HII,NAOMBA KUSEMA TENA HAPPY BIRTHDAY RAIA MWEMA

2 comments:

  1. Happy Birthday to Raia Mwema!!!! Wishing you many more years to come!! Thanks for keeping it real......Your aunthenticity is refreshing ...,

    ReplyDelete
  2. nimejifunza mambo mengi sana mazuri katika jarida hili. Siku chache zilizopita, nililikosa mtandaoni, nilipungukiwa kitu kwa kweli.
    Niwawapongezeni sana wote mnaotufanya tukapata mengi ya kuyasoma ktk jarida hili. Msichoke kuendelea kuifundisha na kuiburudisha jamii. La msingi ni kuzidi kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya haki na Usawa. Hongereni wanajopo, hongera Raia mwema (www.raiamwema.co.tz)

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.