20 Apr 2012




Ray amtia mbaroni Mange Kimambi
•  KUHUSISHWA KIFO CHA KANUMBA

na Irene Mark
JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam, limekiri kumshikilia kwa saa kadhaa kwa mahojiano mmiliki wa ‘blog ya Uturn’, Mange Kimambi, kwa madai ya kumhusisha muigizaji maarufu nchini, Vicent Kigosi au Ray, na kifo cha nguli wa tasnia hiyo, Steven Kanumba, ‘The Great’.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella, alisema Ray alikwenda kulalamika kwenye kituo hicho, kuhusu maneno yaliyoandikwa kwenye mtandao huo akiomba msaada wa jeshi hilo.

“Ninathibitisha kwamba huyo dada tulimshikilia hapa kwetu tangu jana (juzi), tumemwachia leo (jana), kwa sababu dhamana ni haki yake, ila tunaendelea na upelelezi, maana anadaiwa kutuma taarifa kwenye mtandao akimhusisha Ray na kifo cha Kanumba.

“Hiyo blog haijahalalishwa kutoa taarifa za kukashifu na kuwadhalilisha watu… ameandika skandali kwa Ray, tukiiachia hii, maneno hayo yanaweza kuonekana halali na kuleta maafa katika jamii, hasa kwa huyo anayetajwa,” alisema Kamanda Kenyella na kuongeza kwamba kesi iko mahakamani, hivyo si vema kuingilia upelelezi.

Kwa upande wake, Ray aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu Kanumba, alisema kitendo hicho kinahatarisha maisha yake, hivyo ameapa kulishughulikia suala hilo, huku akisisitiza kwamba suala hilo linamvunjia heshima na kumharibia kazi yake.

“Hiki sio kitu cha kweli, Kanumba ni mdogo wangu na tumetoka mbali kimaisha, huyu dada Mange Kimambi simjui… ameandika uongo, sijajua hizi habari amezipata wapi hii ni kutaka kunishushia heshima katika jamii.

“Uigizaji ndiyo kazi yangu, kwa hiyo anapoandika na kuweka kwenye intaneti inayosomwa dunia nzima, anataka kuniharibia kazi yangu? Anataka kuniharibia maisha? Anataka kunipotezea mashabiki?

“…Unategemea watu wanioneje? Hili sitaliacha, nitalifanyia kazi na kulifikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa wanaotumia kalamu zao kutaka kuwaharibia wengine, chochote kitakachonikuta nitadili na huyo mama... haya ni maisha, nitaendelea kuvumilia Mungu yupo,” alisema Ray anayetamba kwenye medani ya filamu ndani na nje ya nchi.

Juhudi za kumpata Mange, aliyewahi kuandaa shindano la urembo la Dar Indian Ocean 2006 na kumwibua Wema Sepetu, hazikufanikiwa baada ya simu yake kutopatikana.
CHANZO: Tanzania Daima

3 comments:

  1. Niliiona post hiyo na nikawasiliana na WAANDISHI WENZANGU kuwaeleza namna ambavyo ETHICS IN MEDIA inavyoingiliwa.
    Niliandika kukumbusha kile nilichofundishwa punde nilipofika Times FM kuwa NO RESEARCH, NO RIGHT TO SAY.

    Tuwe tunakumbushana kuwa SIO VEMA KUHISI, KISHA UKAANDIKA.
    Tusubiri tuwe na hakika

    ReplyDelete
  2. Nilifikiria ana lawyer. Keeping that kind of bog you need Mark Geragos behind you...still her blog has poor taste in all ways. Umbea umejaa sana kule. Wacha wamfundishe adabu..

    ReplyDelete
  3. Ray, grow up men. Do you know something called freedom of speech??? There's no way you can mute ppl because you are bongo celebrity. Even, the hollywood most notable supreme world celebrity they got no power to stop ppl from talking. Let me see how you gonna go about it.Get a life.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.