13 May 2012


MSANII mahiri katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini Abbas Hamisi ‘20 Pacent’ ameamua kujikita kwenye ujasiriamali ambapo sasa amejikita kwenye kilimo huko mkoani Morogoro.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, 20 Percent ambaye alitamba kwa kuzoa tuzo tano kwa mpigo za Wimbo Bora wa Afro-pop, Mtunzi bora wa nyimbo, Mwimbaji bora wa kiume, Wimbo Bora wa Mwaka na Msanii Bora wa Muziki wa Kiume, katika tuzo za Kili Music Awards kwa mwaka 2010 alisema ameamua kuanza kujipanga kwa maisha ya baadaye.

Nyota huyo aliyetamba na nyimbo kama vile ‘Money Money’, ‘Yanini Malumbano’ na nyinginezo kibao alisema kuwa amehamasika kujikita katika kilimo kama ilivyo kwa mkongwe wa muziki huo nchini Selemani Msindi ‘Afande Sele’.

“Kaka hivi sasa mimi nimeamua kujikita pia kwenye kilimo kwa sababu huwezi kutegemea kazi za muziki tu, kuna kila sababu za kuwa mjasiriamali,” alisema 20 Percent.

CHANZO: Tanzania Daima




1 comment:

  1. Hongera sana 20% kwa uamuzi wa Busara...
    Kwa ushauri wa uchumi wa Kilimo pamoja na Biashara usisite kunitafuta..

    @kaka Chahali...
    nimeupenda huu mwonekano mpya.. keep the good work on.

    peace, love & blessings

    www.eastafricaherald.com

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.