16 Nov 2016

Moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Magufuli ni ukusanyaji mapato, ikiwa ni pamoja na yale yatokanayo na madeni. Ni katika utekelezaji wa kipaumbele hicho, Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa taasisi za Elimu ya Juu (HESLB) imeanza 'msako mkali' dhidi ya 'wadaiwa sugu.' watu walionufaika na mikopo hiyo lakini hawajaanze kuirejesha.

Kwanza, nianze makala hii kwa kuipongeza serikali kwa hatua hii muhimu ambayo ikifanyika kw aufanisi, itasaidia ukusanyaji wa mapato makubwa yatakayowezesha udhamini wa serikali kwa wanafunzi wengi zaidi. Sote twatambua umasikini wa Tanzania yetu, na ni jukumu letu kuisaidia nchi yetu.

Binafsi, nilisoma kwa mkopo wa serikali kuanzia mwaka 1996 hadi nilipohitimu mwaka 1999. Wakati huo, na hadi ninaondokaTanzania mwaka 2002, hakukuwa na utaratibu wowote wa urejeshaji wa mkopo huo.

Hali hiyo imeendelea hadi mwaka huu 2016, ambapo ghafla serikali kupitia HESLB imeamka usingizini na kuanza kufuatilia fedha inayotudai, lakini sio kistaarabu (kwani sio kosa letu wadaiwa kutotengenezewa mfumo stahili wa kufanya marejesho ya mikopo tuliyopewa, bali kosa la serikali) na tunaitwa WADAIWA SUGU. Mdaiwa sugu ni mtu ambaye amedaiwa zaidi ya mara moja na hajalipa. Si sahihi kumwita mtu 'mdaiwa sugu' wakati hujamwelekeza jinsi ya kulipa deni unalomdai wala hujahangaika kumdai.



Sina hakika kama kuna watu walishawahi kupewa utaratibu wa kurejesha mikopo ya elimu waliyopewa, lakini kwa uelewa wangu na ufuatiliaji wa yanayojiri huko nyumbani, sijawahi kuona hilo.

Hata hivyo, kwa vile lawama hazijengi, na lengo la serikali 'kukurupuka' ni jema (kukusanya mapato), basi ni vema kuweka kando lawama na sote tunaodaiwa kuanza utaratibu wa malipo ya fedha tunazodaiwa.

Kwa upande wangu, nimetuma barua pepe kwa HESLB kuulizia kiwango ninachodaiwa na taratibu za malipo. 


Nimefainya hivyo ili, kwanza, kuunga mkono jitihada za serikali kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na malipo ya mikopo tuliyokopeshwa. Pili, dawa ya deni ni kulipa. Ninawahamasisha wadaiwa wenzangu kuhusu umuhimu wa kulipa fedha tunazodaiwa. Na, tatu, ku- preempty jitihada zozote za watakaotaka kutumia suala hili la 'udaiwa sugu' kuchafua jina langu. Ni matarajio yangu kuwa kwa hatua hizi za dhati nilizochukua hakutajitokeza 'mchawi' wa kusema "ah wewe Chahali unajifanya mzalendo kumbe fisadi unadaiwa..." haha. 

Anyway, nitatumia ukumbi wangu huu kuwafahamisha majipu nitakayoletewa na HESLB na mustakabali wa 'udaiwa sugu.' 

3 comments:

  1. Ahsante kwa kutushirikisha.

    ReplyDelete
  2. Safi, umekuwa muungwana, japo mikopo tunarudisha lakini wengne wadogo zetu na ndugu zetu ambao ni yatima na tunawasomesha wamekosa mikopo, hii inakatisha tamaa pia.

    Nadhani kila mtu ana nia ya kurudisha mkopo, lakini isiwe njia za kuumizana kama ya kusema unakata 18% ya mshahara hapo ndo watu watajificha zaidi na zaidi

    ReplyDelete
  3. Hongera san brother kwa uamuzi wa kuamua kuunga jitihada za urejeshaji wa deni hilo. Ni imani yangu wakijitokeza wengi na kukamilisha malipo basi ni ishara kuwa vijana wengi wanawezeshwa pia kupata elimu kwa kukopeshwa pia.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.