Showing posts with label AL-QAEDA. Show all posts
Showing posts with label AL-QAEDA. Show all posts

25 Mar 2015


Wiki mbili zilizopita niliandika makala iliyoonya tabia iliyoanza kuzoeleka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kufanya mzaha kuhusu ugaidi. Kwa muda mrefu sasa, viongozi wa chama hicho hususan Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba wamekuwa wakiihusisha Chadema na ugaidi. Lakini tabia hiyo haikuanzia kwa Chadema pekee kwani huko nyumaCUF nayo ilikumbwa na tuhuma kama hizo kutoka kwa CCM.

Katika makala hiyo ambapo nileleza kwa kirefu kiasi kuhusu hatari inayoikabili dunia hivi sasa kutoka kwa vikundi vinavyoongoza kwa ugaidi kwa muda huu, yaani ISIS, Al-Qaeda, Boko Haram na Al-Shabaab, nilitahadharisha kwamba tabia ya CCM kuufanyia mzaha ugaidi, kwa maana ya kuzusha tu 'Chadema ni magaidi au CUF ni magaidi', inaweza kutugharimu huko mbeleni. Nilibainisha kuwa mzaha huo unaweza kuwarahisishia magaidi halisi dhima ya kushambulia nchi yetu, kwani 'tayari tuna magaidi wa ndani- kwa maana ya tuhuma za CCM dhidi ya Chadema na CUF.

Vilevile nilitanabaisha kwamba kuufanyia mzaha ugaidi kunaufanya uzoeleke, uonekane ni kama jambo la kawaida tu ambalo halikauki midomoni mwa akina Nape na Mwigulu.Lakini pengine baya zaidi ni vyombo vyetu vya dola kuwekeza nguvu kubwa kudhibiti 'magaidi hewa' hali inayoweza kuwapa upenyo magaidi halisi.

Kwa bahati mbaya, tahadhari niliyoitoa kwenye makala hiyo inelekea kubeba uzito, baada ya kupatikana taarifa kwamba kikundi hatari kabisa cha magaidi cha ISIS kina mpango wa kujienga na hatimaye kufanya mashambulizi katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa za kituo cha televisheni cha Aljaazera, mawasiliano ya hivi karibuni ya kikundi hicho cha kigaidi yanaonyesha kuwa kinajaribu kujijenga Afrika Mashariki, eneo ambalo limekuwa likisumbuliwa na magaidi wa Al-Shabaab na Al-Qaeda kwa vipindi tofauti.

Hivi karibuni, kikundi cha kigaidi cha Boko Haram cha Nigeria kimetoa ahadi ya utiifu kwa ISIS, hatua iiliyotafsiriwa na wachunguzi wa masuala ya ugaidi kuwa inaweza kuongeza nguvu za ISIS katika maeneo mbalimbali ya bara la Afrika.

Hata hivyo, kitu ambacho hakikufahamika kwa wengi ni kwamba tukio hilo la Boko Haram kuonyesha utii wa ISIS lilitanguliwa wiki chache kabla ya ujumbe uliotumwa kwa kiongozi wa Al-Shabaab , Abu Ubaidah, kumwomba afanye kama walivyofanya Boko Haram (kutangaza utii kwa ISIS)

Ujumbe huo uliwasilishwa na  Hamil al-Bushra, jina linaloaminika kutumiwa na vyanzo viwili vya habari vinavyohusishwa na ISIS.

Katika ujumbe huo, Bushra aliwapongeza Al-Shabaab na kuwahamasisha wafanya mashambulizi Kenya, Ethiopia na TANZANIA.

Soma habari kamili HAPA

9 May 2011


Baada ya kifo cha Osama bin Laden,nani anaweza kuchukua nafasi yake?Tuangalie historia na tabia za warithi watarajiwa wa uongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda



big-fat-aman-nb04-inline
AFP-Getty Images
Ayman al-Zawahiri
Cheo: "Naibu" wa Osama
Wasifu: Daktari wa macho
Sifa Maalum: Msemaji mahiri wa Al-Qaeda
Maficho: Mara ya mwisho alionekana Khost, Afghanistan, mwaka 2001
Wasifu: "Kichwa" kilichoandaa Mashambulizi ya September 11,2001 nchini Marekani
Anafahamika zaidi kwa: Ushiriki wake katika mashambulizi ya mabomu kwa balozi za Marekani mwaka 1998
"Nembo" (trademark): Miwani ya njano


big-fat-aladel-nb04-inline
FBI-Getty Images
Saif al-Adel
Cheo: Mwandaaji wa operesheni za kigaidi kimataifa
Asili: Vikosi Maalum (special forces) vya Jeshi la Misri
Sifa maalum: "Bwana mipango"
Maficho: Waziristan, kwa mujibu wa ripoti
Wasifu: Aliwekwa kizuizini kwa miaka minane nchini Iran
Anafahamika kwa: Mashambulizi ya mabomu mwaka 1998
"Nembo": Vijinywele kwenye kidevu


big-fat-nb04-allibi-inline
Intel Center
Abu Yahya al-Libi
Cheo: Mwanateolojia
Asili: Mshairi na mwanazuoni
Sifa Maalum: Mwanapropaganda wa Al Qaeda
Maficho: Afghanistan au Pakistan
Wasifu: Alitoroka jula ya Wamarekani huko Bagram, Afghanistan
Anafahamika kwa: kujaribu kumuua Muammar Gaddafi
"Nembo": Hotuba kali


big-fat-nassar-nb04-inline
Intel Center / Polaris
Nasser al-Wuhayshi
Cheo: Kiongozi Peninsula ya Rabia
Asili: Katibu muhtasi wa Osama
Sifa maalum: Alitoroka gerezani Sanaa, Yemen, mwaka 2006
Maficho: Yemen
Wasifu: Alishirikiana bega kwa bega na Osama katika mapambano huko Tora Bora, Afghanistan
Anafahamika zaidi kwa: Kutoroka jela huko Yemen
"Nembo": "Andunje": ni mfupi wa chini ya futi tano



big-fat-adam-nb04-inline
Intel Center / AFP-Getty Images
Adam Gadahn
Cheo: Msemaji
Asili: Anapenda miziki ya sauti kali  yenye ujumbe wa kifo
Sifa maalum: Anamudu kiingereza vizuri,mjuzi wa teknolojia
Maficho: Alihamia Pakistan mwaka 1998, ameoa mkimbizi wa Kiafghanistani
Wasifu: Aliwahi kufungwa kwa kumpa kipigo mwenyekiti wa msikiti aliokuwa akiswali
Anafahamika zaidi kwa: Kumpa elimu Osama kuhusu mtikisiko kwenye sekta ya dhamana ya majengo (mortgage crisis)
"Nembo": Mjukuu wa mtaalam wa Kiyahudi wa elimu ya mkojo (urology)


big-fat-adnan-nb04-inline
FBI-Getty Images
Adnan el-Shukrijumah
Cheo: Afisa mipango ya nje
Asili: alisoma Kemia
Sifa maalum: Aliishi Marekani kwa miaka 15
Maficho: inadhaniwa kuwa Pakistan
Wasifu: Mrithi wa Khalid Sheikh Mohammed
Anafahamika zaidi kwa: Kupanga shambulio lililofeli la mabomu kwenye mfumo wa reli ya chini ya ardhi nchini Marekani mwaka 2009
"Nembo": Kushirikiana na magenge ya majahili wa Honduras


big-fat-nb04-alquso-inline
Fahd al-Quso
Cheo: Kamanda wa operesheni za mashambulizi
Asili: Mbeba mabegi ya bin Laden
Sifa maalum: Kulala fofofo: "alilewa" usingizi hadi akachelewa kazi ya kurekodi shambulio la kigaidi kwa manowari ya  USS Cole.
Maficho: Kaskazini mwa Waziristan
Wasifu: Kuandaa shambulizi la mabomu kwa manowari ya USS Cole.
Anafahamika zaidi kwa : Aliwatambua kwa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) magaidi wawili waliohusika na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11,2001 nchini Marekani
"Nembo": Nywele zake kwenye paji lake zimekaa kama herufi V iliyogeuzwa


big-fat-nb04-Droukdel-inline-tease
Sifaouoi Mohamed / SIPA
Abdelmalek Droukdel
Cheo: Kiongozi wa  Islamic Maghreb
Asili: mwanafunzi wa sayansi
Sifa maalum: Mtaalam wa milipuko
Maficho: Aljeria
Wasifu: Idara ya Hazina ya Marekani ilitaifisha mali zake mwaka 2007
Anafahamika zaidi kwa: Kuua watu 70 kwenye kwa shambulizi za bomu jijini Algiers,Aljeria
Trademark: Tambara la kijana kama yale ya mabaniani
Imetafsiriwa (isivyo rasmi) kutoka jarida la Newsweek


Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.