Showing posts with label BUSANDA BY-ELECTION. Show all posts
Showing posts with label BUSANDA BY-ELECTION. Show all posts

17 May 2009


NIMEKUTANA NA HABARI ILIYONISHTUA KIDOGO,KWAMBA MMOJA WA WANA-CCM WALIOOMBA KUGOMBEA KITI CHA UBUNGE KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUSANDA,DONALD MAX, AMEREJESHEWA GHARAMA ALIZOTUMIA WAKATI WA KUJIPIGIA DEBE.INADAIWA HILO LIMEFANYIKA ILI AWEZE KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI ZA MGOMBEA ALIYEPITISHWA NA CCM,LORENCIA BUKWIMBA.

KWA MUJIBU WA GAZETI LA Mwananchi:


Taarifa...za ndani zilisema kukubali kwa Max kupanda jukwaani, kunatokana na makubaliano ya faragha baina yake na Malecela kwa niaba ya Kikwete ambaye aliagiza arejeshewe gharama zake za kampeni katika mchakato wa kura za maoni...Kutokana na makubaliano hayo CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye.

NASEMA HABARI HIYO IMENISHTUA "KIDOGO" KWA VILE CCM SI NGENI KATIKA ULIMWENGU WA MAIGIZO YA KISIASA.KWA MFANO,TUME YA MAADILI YA CHAMA HICHO BADO IKO CHINI YA UONGOZI WA MZEE WA VIJISENTI,MWANASIASA AMBAYE MAADILI YAKE YA UONGOZI NI QUESTIONABLE KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUJILIMBIZIA VIJISENTI HAPO JERSEY.

LAKINI INAPOFIKIA HATUA YA CHAMA HICHO KUREJESHA GHARAMA ZA MGOMBEA ALIYESHINDWA KWENYE NOMINATION PROCESS INAMWAGA ZEGE ZAIDI KWENYE UKWELI KWAMBA CHAMA HICHO TAWALA KINA UHABA MKUBWA ZA BUSARA ZA UONGOZI.HIVI KUREJESHA GHARAMA HIZO KUNA TOFAUTI GANI NA KUMHONGA MWANASIASA HUYO ILI APANDE JUKWAANI?HIVI,TUKIAMINI KUWA HABARI HIZO NI ZA KWELI,CCM ITOE FEDHA HIZO KISHA MAX APANDE JUKWAANI KUMNADI MGOMBEA BUKWIMBA,KISHA CHAMA HICHO KISHINDWE KWENYE UCHAGUZI (WHICH IS POSSIBLE KAMA KUTAKUWA NA UCHAGUZI HURU NA HAKI)........FILL IN THE BLANKS,MZALENDO MWENZANGU.

KAMA LEO CCM INADIRIKI KUTOA FEDHA KUMSHAWISHI MAX APANDE JUKWAANI,ITASHINDWAJE KUWAPA FADHILA MAFISADI KATIKA UCHAGUZI WA MWAKANI IWAPO CHAMA HICHO KITAELEKEA KUSHINDWA?HAYA YALITOKEA 2005,NA NDIO VYANZO VYA SKANDALI ZA EPA NA NYINGINEZO.SIJUI INGEKUWAJE LAITI MAREHEMU BABA WA TAIFA ANGERUDI DUNIANI NA KUKUTA CHAMA ALICHOKIASISI KINAFANYA UTUMBO KAMA HUU!

11 May 2009


Na Frederick Katulanda, Busanda

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzongwa na kundi la wananchi waliomuhoji juu ya ahadi zake za umeme alipowasili katika mji wa Katoro wilayani Geita.

Tukio hilo mithili ya mdahalo lilitokea kati ya majira ya ya saa 9:30 hadi saa 10:15 muda mfupi tu baada ya Ngeleja kuwasili Busanda akitokea Mwanza.

Maswali yalianza baada ya Waziri Ngeleja kusalimiana na wananchi hao na akajibiwa kwa kuonyeshwa alama za vidole viwili.

Hali hiyo ilimfanya waziri huyo kuwauliza wananchi hao sababu za kuichukia CCM wakati imekuwa ikijitahidi kuwaletea maendeleo na ndipo walipoanza kumuuliza maswali huku akiyajibu wakati fulani kugeuka mabishano.

"Hatuwezi kuwashangilia nyinyi... mmetuahidi umeme siku nyingi na hatuuoni, leo mnakuja kutuambia nini. Alikuja hapa sijui (Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam) Malima akasema umeme utakuja, lakini wapi hatujaona lolote mpaka leo," alisema mwananchi mmoja.

Ngeleja alipotaka kujibu, mwananchi mwingine alidakia kusema: "Hata kwenye machimbo mmekuwa mkitunyang'anya maeneo yetu na kuwapa wawekezaji. Sisi mnatuona hatufai kama vile ni wakimbizi ndani ya nchi yetu."

Ngeleja alilazimika kuwatuliza na kuwaomba wapunguze maswali ili ajibu swali moja baada ya jingine, lakini kila mtu akataka kumuuliza swali na kukawa na msuguano kati yake na wananchi.

Alianza kujibu kwa kusema kuwa serikali ipo mbioni na kwamba kinachofanyika sasa ni kufuata taratibu kwa sababu mchakato wa suala hilo hauwezi kumalizika siku moja, hivyo akawaomba wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea.

Ngeleja alidai kuwa suala lao kuhusu umeme liko katika hatua ya kuridhisha na kwamba wanapaswa kutambua utaratibu wa kushughulikia miradi ya serikali umekuwa ukifanyika kwa hatua.

Majibu hayo yalipingwa na wananchi ambao walimwambia wamekuwa wakidanganywa kama watoto kwa sababu ya kutaka kura na wakishapata, hutoweka.

"Sikiliza basi nikujibu, wewe naona umetanguliza ushabiki tuu. Naomba unisikilize. Ni kweli tulipowaahidi umeme tulidhani mchakato ungekamilika mapema, lakini kuna mambo yametukwamisha, tunaomba mtuvumulie," alisema huku wananchi hao wakiendeleza maswali.

Wakati wakiendelea na mjadala huo, lilipita gari la mgombea CCM wa kiti cha ubunge cha Busanda, Lolensia Bukwimba na mara moja wananchi hao wakageuka na kuanza kuzomea msafara.

Wakati wakiendelea kuzomea ndipo Ngeleja alipopata mwanya na dereva wake akawasha gari na kuondoka.

Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited.

CCM imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na Faustin Kabuzi Rwilomba ambaye alifariki akiwa nchini India alikoenda kutibiwa
.

CHANZO: Mwananchi

IWAPO KUNA LOLOTE LA KUJIFUNZA KATIKA KAMPENI HIZI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUSANDA BASI NI NAMNA CCM ILIVYO KICHWA NGUMU KUELEWA SOMO.THING IS,WAMESHAHADAA WAPIGA KURA KIASI CHA KUTOSHA KWA AHADI HEWA,HIVYO KUREJEA TENA AHADI HIZOHIZO AMBAZO HAWAJAZITEKELEZA NI MITHILI YA,ASHAKUM SI MATUSI,KUMTONGOZA MTALAKA WAKO.

PENGINE JINGINE NI NAMNA CHAMA HIVYO KISIVYO SERIOUS NA USTAWI WA WANANCHI.WHY?BADALA YA KUREJEA AHADI HIZO AMBAZO HAZIJATEKELEZWA,CHAMA HICHO KWANZA KILIPASWA KUWAOMBA RADHI WAPIGA KURA KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA AHADI HIZO HADI SASA,NA ANGALAU BAADA YA HAPO KINGEWEZA KUJARIBU KETE YA KUREJEA AHADI HIZO.NASEMA THAT IS INDICATIVE OF LACK OF SERIOUSNESS KWA VILE CCM INAAMINI KUWA KAMA ILIKUWA IKITOA LOTS OF EMPTY PROMISES FOR AGES NA WAGOMBEA WAKE WAMEENDELEA KUCHAGULIWA,BADO KUNA IMANI KUWA SUCH A RISKY STRATEGY COULD WORK AGAIN AND AGAIN.

CCM HAIDHANI KUWA IMAGE YAKE IKO SEVERELY TARNISHED NA USWAHIBA WAKE NA UFISADI/MAFISADI.INAENDELEA KUAMINI KUWA SHUTUMA DHIDI YAKE KWAMBA NI KICHAKA NA HIFADHI YA MAFISADI NA ZA WATOVU WA NIDHAMU WACHACHE KAMA SIE LAKINI SIO KWAMBA KELELE ZETU NI UWAKILISHI TU WA VILIO VYA MAMILIONI YA WATANZANIA WALIOCHOKA KUFANYWA WAJINGA.

HIVI KIONGOZI MWENYE BUSARA ANAWEZA KUDIRIKI KU-BRING UP ISHU ZA DOWANS KWENYE BY-ELECTION KAMA YA BUSANDA?CAN'T BLAME NGELEJA KWA KUWA KWA YEYE NA VIGOGO WENZIE WA CCM,EQUATION YA DOWANS=RICHMOND HAIJAMWINGIA KICHWANI.

8 May 2009


Na Frederick Katulanda, Busanda

KAMPENI za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda jana zilizidi kukumbana na upinzani mkali baada ya makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela, kujikuta wakizomewa wakati walipokuwa wakijinadi katika mkutano uliofanyika Nyarugusu wilayani Geita.

Mbali na vigogo hao wa CCM, mgombea wa chama hicho katika uchaguzi huo mdogo, Lolencia Maselle Bukwimba na mumewe, Maselle Buziku walizomewa wakati walipotambulishwa kwenye mkutano huo wa kampeni.

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya chama hicho kujikuta kikiwa na watu wachache wakati wa kuzindua kampeni zake kwenye kata ya Kaseme, tofauti na mikutano ya vyama pinzani vya Chadema na CUF.

Dalili za hali mbaya katika mkutano huo zilianza wakati viongozi hao wakiingia eneo la Nyarugusu ambalo ni maalumu kwa wachimbaji wa dhahabu. Viongozi hao walipokelewa na alama ya vidole viwili kila walikopita. Alama ya vidole viwili hutumiwa na Chadema.

Zomea zomea hizo ziliwakabili viongozi hao wa CCM wakati walipokuwa wakimnadi mgombea wao. Hali mbaya ilianza kwa katibu mwenezi na uhamasishaji, Simon Mangelepa wakati aliposimama jukwaani na kuanza kuwatambulisha wageni walioambatana nao na kufuatiwa na mbunge wa viti maalum mkoani Mwanza, Maria Hewa ambaye alizomewa baada ya kuwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kutulia.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Clement Mabina alisimama jukwaani kabla ya kumkaribisha Malecela ili amnadi mgombea wa chama hicho na kuwaeleza kuwa anazo taarifa kuwa kuna watu ambao wamepangwa hapo kwa ajili ya kuzomea, naye kuzomewa.

Baadaye ikawa zamu ya Malecela ambaye baada ya kusimama jukwaani aliwaeleza wananchi kuwa shutuma za ufisadi hazina nafasi katika kampeni kwa sasa na kuwataka wenye ushahidi wa ufisadi kuupeleka polisi, kauli ambayo iliwafanya wananchi ambao walikuwa wametulia, kuanza kuzomea wakimtaka aondoke huku wakionyesha vidole viwili.

Hata hivyo, Malecela aliwatuliza na kuwaeleza kuwa hiyo ndio njia sahihi ya kushughulikia mafisadi na kuendelea kuwaeleza wananchi kuwa iwapo wataichagua CCM katika uchaguzi huo watapatiwa umeme pamoja na kutengewa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo.


Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo," alisema lakini akakatwa kauli na kelele za wananchi ambao walisema miaka yote wameichagua CCM na kuahidiwa mambo hayo bila ya kufanikiwa.

Kutokana na hali hiyo Malecela aliamua kuwatuliza na kuomba Busanda isigeuke kama Tarime na kwamba wao CCM wanataka kampeni za amani na utulivu.

Ndipo ilipofika zamu ya Msekwa kumnadi mgombea na baada ya kupanda jukwaani alimkaribisha mgombea aliyemsimamisha mumuwe, Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao.


Hata hivyo zomea zomea hizo hazikuweza kuhatarisha amani katika mkutano huo na mgombea huyo alijieleza bila ya matatizo na kupiga magoti lakini alipoomba kura, naye akajikuta anazomewa.

Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amekiri kuwa kuna hali ngumu kwenye Jimbo la Busanda na kuwataka viongozi wa chama hicho kupigana kufa au kupona ili kuhakikisha jimbo haliangukii mikononi mwa upinzani kwa kuwa machungu ya kushindwa Tarime anayajua.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamba juzi mchana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika mkutano wa ndani kwenye ofisi za CCM wilayani Geita baada ya kuwasili kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni wa chama chake zilizofanyika juzi katika kata ya Kaseme.

Makamba alikiri kuwa hali ni ngumu na hivyo kuwaomba kila mmoja kuhakikisha mgombea wa CCM anashinda, akilalamika kuwa makali ya kushindwa alishayaonja Tarime.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa chama wilayani humo zimeeleza kuwa Makamba aliamua kufanya mkutano huo kwa lengo la kuwekana sawa kutokana na CCM kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wale walioenguliwa katika kura za maoni za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho.

Makamba amesema "jamani kushindwa ni kubaya, mwenzenu Tarime nilionja ubaya wake mpaka ilibidi nitoroshwe na Green Guard ili kuepuka kuzomewa, sasa tusiposhikamana mambo yatakuwa magumu tutoe tofauti zetu,'” alisema mmoja wa wajumbe waliokuwa kwenye kikao hicho akimnukuu Makamba.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo Makamba alishtuka na kuhoji iwapo walikuwemo waandishi wa habari ukumbini humo na kuonya utoaji wa taarifa hizo baada ya kujibiwa hawakuwemo.

Aidha baada ya kujibiwa kuwa hakuna waandishi Makamba alishtuka baada ya kubaini kuwa kulikuwa na mpiga picha wa chama na kumuagiza kuhakikisha mkanda huo anaukabidhi kwa katibu wa CCM wa mkoa.

Makamba alipoulizwa kuhusu suala hilo alijibu kuwa hajawahi kukiri kuwepo kwa hali ngumu kwa vile hana wasiwasi na uchaguzi huo na kusema alikuwa akieleza masuala ya kushikamana.

“Wewe unataka nikueleze mikakati yangu, kama nilikuwa nawahimiza watoto wangu kulima we unakutakia nini,” alihoji katibu huyo wa CCM alipoulizwa na Mwananchi kuhusu kikao hicho.

Sambamba na hatua hiyo Makamba alimtaka mjumbe wa halmshauri kuu ya chama hicho mkoani Mwanza, Anthony Diallo kutumia uwezo wake kuhakikisha kampeni hizo zinakuwa na hamasa ya kutosha ikiwa ni pamoja na kurusha taarifa zake katika vyombo vya habari.

Uchaguzi katika jimbo la uchaguzi la Busanda umepangwa kufanyika Mei 24 kwa lengo la kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Faustine Kabuzi Rwilombe.

Vyama vingine vinavyowania kiti hicho ni Chadema, CUF na UDP.

CHANZO: Mwananchi

WANACHOHITAJI CCM NI BUSARA ZA KI-UTU UZIMA,YAANI KUKIRI PALE WALIPOKOSEA,NA KUAHIDI KUJIREKEBISHA BADALA YA KUENDELEZA AHADI HUKU ZILE WALIZOTOA MWANZO ZIMEENDELEA KUBAKI AHADI TU PASIPO KUZITEKELEZA.WAINGEREZA WANASEMA " A PROMISE MEANS NOTHING UNTIL DELIVERED."
HALAFU HIZI KAULI ZA KIBAGUZI KUWA "ICHAGUENI CCM IWALETEE HIKI AU KILE" (AS IF AWALI ILIYOCHAGULIWA ILIKUWA CHADEMA AU CUF) NI KUWAFANYA WAPIGA KURA WAJINGA AU WASAHAULIFU.KAMA WALIKUWA NA NIA YA KULETA HUO UMEME,SI WANGEFANYA HIVYO WAKATI WAPIGA KURA WALISHAWAPA HESHIMA YA KUMCHAGUA MGOMBEA WA CCM KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA?SASA HIZI HABARI KUWA MKITUCHAGUA TENA NDIO TUTAFANYA HIKI AU KILE NI MITHILI YA KUWAHADAA WANANCHI.
I HOPE WAPIGAKURA WA BUSANDA HAWATAISHIA KUFIKISHA UJUMBE KWA CCM KWA KUZOMEA TU BALI PIA KUINYIMA KURA ILI IKIAMSHE CHAMA HICHO KUTOKA USINGIZINI KWAMBA THIS IS 2009,AND SO FAR THE ASSESSMENT OF HOW THE PARTY HAS IMPLEMENTED ITS ELECTION MANIFESTO LEAVES A LOT TO BE DESIRED.KAMA TARIME WALIWEZA,BUSANDA PIA WANAWEZA.NA KAMA WOTE WASIORIDHIKA NA MWENENDO WA CCM WATAAMUA KUWA ENOUGH IS ENOUGH,NO MORE FALSE PROMISES,THEN CHANGE IS NOT ONLY COMING BUT WILL EVENTUALLY BE ACHIEVED.
AS OBAMA SAID,YES WE CAN IF WE BELIEVE IN CHANGE.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.