Showing posts with label KOSOVO. Show all posts
Showing posts with label KOSOVO. Show all posts

8 Mar 2008

Mzimu wa uhuru wa Kosovo unaendelea kuisumbua Serbia na sasa serikali yake imesambaratika kutokana na tofauti za kimsimamo kati ya Waziri Mkuu,Vojislav Kostunica mwenye mtizamo wa kitaifa (nationalist) na Rais Boris Tadic mwenye mtizamo wa kimagharibi zaidi.Habari zaidi,soma HAPA.

PIA KUNA HABARI MOJA IMENIGUSA SANA KUHUSU BIASHARA YA "UNGA" KATIKA NCHI YA GUINEA BISSAU.UNAWEZA KUISOMA HAPA



20 Feb 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inazungumzia UHURU.Inaanza kwa kuhabarisha kuhusu tangazo la Uhuru wa Kosovo,kisha inachambua "urafiki mpya" wa Marekani na China kwa Bara la Afrika na kuhitimisha kwamba urafiki huo ni mithili ya Mkutano wa Berlin 1884-5 ulioligawa bara la Afrika miongoni mwa wakoloni.Makala hii inakumbushia pia kwamba kuna uwezekano ziara ya Bush barani Afrika ikabaki kumbukumbu muhimu kwake kutokana na namna alivyonyenyekewa katika kipindi ambacho ni mmoja ya marais wanaochukiwa sana katika sehemu mbalimbali duniani,na very unpopular nyumbani kwake US of A.Kadhalika makala inawashikia bango Mwanyika na Hosea kwamba wajiuzulu haraka sana,sambamba na wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya Tume ya Mwakyembe.Pamoja na makala nyingine zilizokwenda shule ya hali ya juu,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.

17 Feb 2008

Muda mchache uliopita,Kosovo imejitangazia uhuru wake ikiahidi kuwa nchi ya kidemokrasia,katika hatua inayoungwa mkono na Marekani na nchi nyingine za Magharibi lakini ikipingwa vikali na Russia na Serbia.

Spika wa Bunge Jakup Krasniqi,Waziri Mkuu Hashim Thaci na Rais Fatmir Sejdiu,ndio waliosaini tangazo hilo la uhuru ambalo limepokelewa kwa nderemo na vifijo katika nchi hiyo,hususan katika mji mkuu Pristina ambapo maandalizi ya shughuli hiyo yalianza kwa siku kadhaa.

Wakati hayo yakitokea,Rais wa Serbia Boris Tadic amelaani hatua hiyo ya Kosovo kujitangazia uhuru na kubainisha kuwa nchi yake haitambui uhuru huo wa Kosovo.Akijibu mashambulizi,Waziri Mkuu Thaci alisema kwamba kamwe Kosovo haiwezi kuwa tena chini ya himaya ya Serbia.Thaci,mpiganaji wa zamani wa Jeshi la Ukombozi la Kosovo ambalo kati ya mwaka 1998 hadi 1999 lilipambana na majeshi ya Serbia katika vita ya kudai uhuru iliyogharimu zaidi ya maisha 10,000.

Kwa undani zaidi kuhusu kuvunjika kwa nchi iliyokuwa ikijulikana kama Yugoslavia (unamkumbuka Tito!?) hadi kufikia Kosovo,bonyeza KIUNGANISHI hiki

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.