Showing posts with label LIFE BEHIND BARS. Show all posts
Showing posts with label LIFE BEHIND BARS. Show all posts

14 Oct 2008


Wanasema maisha ya jela,popote pale duniani,ni balaa.Lakini maisha ya jela katika nchi masikini kama Tanzania ni zaidi ya balaa.Hebu fikiri,iwapo baadhi ya watu wasio na hatia,na ambao wanalipa kodi kupata huduma stahili,wanateseka kupata HAKI hizo (mifano hai ni kwenye huduma muhimu kama afya,maji,barabara,nk) unatarajia nini kitokee kwa WAHALIFU!Yaani kwa mfano mfupi,kama ndugu wa wanandoa wanawekewa vikwazo kuingia kwenye harusi,what would you expect kwa wazamiaji?

Kuna mantiki zilizojengeka katika jamii kuhusiana na hali flani.Ugonjwa wa ukimwi,mathalan,unahusishwa moja kwa moja na ngono,japo kuna njia nyingine za maambukizi.Kuwa mfungwa nako kunahusishwa moja kwa moja na uhalifu,japo inafahamika wazi kwamba katika baadhi ya sehemu ambapo kuna sheria kwa wenye uwezo na nyingine kwa wasio na uwezo,mtu anaweza kujikuta jela akiwa hana kosa lolote:kasingiziwa kesi,kashindwa kumpata mwanasheria mzuri,nk.Kwahiyo wakati tunahitimisha kwamba wafungwa wote ni wahalifu ni muhimu pia kukumbuka kwamba baadhi yao wapo huko kutokana na haki zao kufinyangwa.Lakini hata kama wote ni wahalifu,hiyo haiondoi umuhimu wa kuwapatia baadhi ya haki za msingi as long as haziwafanyi watamani kuishi jela milele.

Kampuni ya Global Publishers leo imeandaa tamasha la kihistoria huko nyumbani ambapo mwanamuziki mahiri (ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha) Nguza Viking,maarufu kama Babu Seya,na wanae watatumbuiza wafungwa wenzao katika shughuli hiyo itakayofanyika kwenye gereza la Ukonga.Hili ni tukio la kihistoria na Global Publishers wanastahili pongezi nyingi kwa kuja na wazo kama hili.Wakati umefika sasa kuonyesha kwa vitendo kwamba wafungwa ni sehemu ya jamii,hasa ikizingatiwa kwamba status yao ya ufungwa,kwa namna moja au nyingine,ni matokeo ya interaction zao na wanajamii wenzao.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.