Showing posts with label MBEYA. Show all posts
Showing posts with label MBEYA. Show all posts

16 Nov 2011

Miraj Kikwete (kushoto)


MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Miraj Jakaya Kikwete, amekitetea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akipinga chama hicho kuhusishwa na vurugu mbalimbali zinazotokea nchini, zikiwemo zile za Wamachinga, zilizotokea jijini Mbeya hivi karibuni.

Mtoto huyo wa Rais alionyesha kukerwa na watu wenye mtazamo wa kukisingizia chama hicho kikuu cha upinzani kwa kukihusisha na vurugu, wakati hali halisi inaonyesha wazi kuwa wananchi wenyewe hawaridhishwi na hali ya mambo ilivyo na hivyo kuamua kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao.

Miraj aliweka wazi msimamo wake huo kupitia mtandao wake wa facebook akichangia mjadala mzito uliohoji kwa nini CHADEMA inasingiziwa vurugu Mbeya?

Mtoto huyo wa Rais, aliweka wazi ujumbe wake huo baada ya mchangiaji mmoja, kuchangia kwa jazba akitabiri machafuko kutokea kabla ya 2015.

Mchangiaji huyo alisema yeye si mtabiri, lakini kwa hali ilivyo nchini, tunaelekea kwenye vita na haina hata mpito wa chaguzi mbili mbele kwa maana ya 2015 na 2020.

Mchangiaji mwingine, Gallus Mpepo, ambaye ndiye aliyekuwa akijadiliana na Miraj, alianza kwa kumrushia lawama Mkuu wa Mkoa mpya wa Mbeya, Abbas Kandoro, kwamba kila mkoa anaokwenda, amekuwa ukikumbwa na vurugu za Wamachinga.

Mpepo alisema anashangaa kuona baadhi ya wachangiaji wa mjadala huo, wanahusisha vurugu za Mbeya na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), licha ya kwamba chanzo chake kiko wazi kwamba wafanyabiashara hao walikuwa wakipinga kuondolewa kwenye maeneo yao ya biashara bila kupewa maeneo mbadala.

Alisema hii inatokana na hali ya kutaka kuficha makosa yaliyofanywa na uongozi wa mkoa huo chini ya Kandoro, kutoongoza kwa busara katika kutatua kero za wananchi.

Katika ujumbe huo, Mpepo alieleza kufurahishwa na ujumbe wa mtoto wa Rais Kikwete na kwamba ameupenda ufafanuzi wake kuhusu mjadala huo.

Akichangia mjadala huo, Miraj ambaye ni nadra kujihusisha na masuala ya siasa, alihoji nani anayedai haki Mbeya kati ya CHADEMA na wananchi hadi kusababisha vurugu hizo.

Mtoto huyo wa Rais Kikwete alisema ni makosa kuihusisha CHADEMA na vurugu hizo kwani CHADEMA si nchi.

“CHADEMA si nchi ni chama na si kwamba wanachama wa CHADEMA ndio pekee wenye shida na matatizo, ni Watanzania wote,” alisema mtoto huyo wa Rais.

Miraj alienda mbali kwa kusema ni fikra potofu kufanya kama vile kuna Tanzania na CHADEMA.

“Maana serikali ndiyo Tanzania na CHADEMA ni chama ndani ya Tanzania, ni chama cha Watanzania kwa ajili ya Watanzania, kama kilivyo Chama cha Mapinduzi (CCM), NCCR-Mageuzi na kadhalika.

“Tofauti ni harakati na sera... tupendane Watanzania, tutafika mbali kwa umoja na mshikamano wetu na wala si kwa kejeli na matusi…, wenye haki tuwasimamie wote na penye haki tusimame sote,” alisema Miraj


12 Nov 2011

Vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wangonjwa katika Zahanati ya Ipinda, iliyopo Mwanjelwa jijini Mbeya vikiwa wazi baada ya wagonjwa kukimbia mara baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi

02. Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.

03.  Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akionesha Bomu la machozi lililopigwa na Jeshi la polisi na kuingia ndani ya Wadi.

04.  Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa.

05. Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya.

06. Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akiwa ameshika kigae kilichodondoka mara baada ya bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.
 CHANZO:  www.mbeyayetu.blogspot.com
:

6 Aug 2011



Juu ni taswira mbali mbali zinazo onesha jinsi ujenzi wa soko kuu la Mwanjelwa ulivyo simama, ulianza kwa kasi lakini kwa sasa hakuna kinacho endelea na miezi kadhaa iliyo pita jengo hilo lilibomoka wakati wanaendelea na ujenzi. Tutaendelea kuwafahamisha zaidi juu ya swala hili 

HUU NDIO UBUNIFU WA DARAJA LA JUU KWA WATEMBEA KWA MIGUU WA JIJI LA MBEYA ENEO LA MWANJELWA MIAKA MIWILI IJAYO KAMA ULIVYOBUNIWA NA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

Taswira ya karibu inayo onesha Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya 

SWALI NI JE ITAWEZEKANA? IKIWA SOKO TUU LINASUA SUA NA LIPO BARABARANI ENEO WANALO TAKA KUWEKA KIVUKO HICHO.

Imetumwa na Mbeya Yetu Blog

6 May 2011

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.