Showing posts with label POMBE. Show all posts
Showing posts with label POMBE. Show all posts

15 May 2009

Pombe bwana!Huyu si "shoga",ni mwanaume ila tu kinywaji kimemkolea kaamua atinge gauni.Na sijui hiyo pozi kajifunzia wapi!

Huyu "Beyonce Mweupe" anaonyesha ufundi wa kunengua.

Hao si watoto wa shule,na huo "upole" ni sehemu ya kinywaji pia!

"Kwanini Mungu aliwapendelea ng'ombe kuwa na miguu minne na sie wanadamu miguu miwili?"Yaelekea ndio "malalamiko ya muungwana huyo anayetambaa.Au anakumbukia alivyokuwa akitambaa wakati wa utoto?Katika pombe,lolote linawezekana!

Kilio tena!?

Pombe huwafanya wanyonge wajione majabali,only kinywaji kinapoyeyuka kichwani hujikuta wakiwa wanyonge vilevile PLUS majeraha.
"Yes!Nimeweza.Si mlisema siwezi kulibalansi hilo boksi la take-away eti nimelewa?Mbona nimeweza.Watu tumeanza pombe zamani,in fact kabla ya kunyonya maziwa ya mama...teh teh teh"
"Basi nikwambie shoga,mwaka 1978 nili....halafu kabla ya hapo mwaka 1749 nilikuwa....na mwaka huu 2004 nita....".Stori za kilevi hazihitaji kuwa makini na tarehe au muda.Na zinaweza kuendelea milele.Kimsingi huwa haziishi,na mada hubadilika kama bendera na upepo.

" Nahisi kama niko 'leba' mtoto najifungua.Hee nimezaa mtoto wa kiume".Si ajabu huyu akiamka asubuhi anamaizi kuwa kweli "alizaa" lakini mtoto ni "pooh" (ile kitu inayotupeleka msalani).
Duh.Hapa ni ujenzi wa mahekalu hewani
Huyu ashukuru ufanisi wa polisi wa doria wanaosaidiwa na CCTV.Ukaaji huo mitaa ya uswahilini ingeweza kumfanya huyo jamaa kwa siku kadhaa asitoke nyumbani kutokana na aibu.Ni mkao hatari sana!
Hoi!

Ah,nani kasema kitanda lazima kiwe chumbani.Hapa napata 'nepu' ya bure buleshi.
" Hee hawa vipi tena?",dada wa kushoto haamini anachokiona."Ahaaa,ndio mana wanaume wa kiskotishi wanapenda hizo kilt zao wanapokwenda out..." Anazidi kutafakari mdada wa watu.

"Kuanzia leo mto wangu utakuwa tairi..."Chapombe afanya uvumbuzi usiku wa manane.
Huy kibonge sijui anatoa nasaha gani kwa wenzake.Pombe huleta "busara" za ajabu kabisa.
Oh dear dear....
Picha hizi zimepigwa na mwanafunzi wa KiPolish jijini Cardiff,Wales.Habari zaidi kuhusu picha hizo na utamaduni wa chapombe (binge culture) BONYEZA HAPA.





22 Sept 2008

Kwa Dar es Salaam,na pengine kwingineko pia,sijui utaenda baa gani ambayo hawajafungulia muziki kwa sauti ya juu.Kumbe kuna maelezo ya kisayansi kwanini wenye baa wanapendelea muziki full blast.BONYEZA HAPA kupata undani zaidi.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.