Showing posts with label SITUATION ROOM. Show all posts
Showing posts with label SITUATION ROOM. Show all posts

3 May 2011

Rais Obama,Makamu wake wa Rais Joe Bden (wa kwanza kushoto),Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinotn (aliyeweka mkono mdomoni),Waziri wa Ulinzi Robert Gates (wa kwanza kulia),pamoja na timu ya usalama wa taifa wakifuatilia shambulizi la askari wa kikosi maalum (SEALs) nchini Pakistan lililopelekea kuuawa kwa Osama Bin Laden.Hapo ni katika ukumbi wa kutathimini mwenendo wa mambo (Situation Room),Ikulu ya Marekani

Rais Obama akisisitiza pointi huku Mshauri wake wa usalama wa taifa Tom Donilon (kulia) akisikiliza.





Rais Obama na timu yake ya usalama wa taifa huku Makamu  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Marekani,Jenerali James Cartwright akonekana kwenye screen




Rais Obama akisikiliza kwa makini mwenendo wa operesheni ya kumuua Osama Bin Laden

Rais Obama akiongea kwenye simu katika moja ya simu mbalimbali muhimu alizopiga kufahamisha mafanikio ya operesheni ya kumuua Osama,ikiwa ni pamoja na simu kwa Maraisi wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton na George W. Bush




Rais Obama akipitia hotuba yake kabla hajalihutubia taifa kufahamisha kuwa Osama ameuawa




Viongozi waandamizi katika utawala wa Rais Obama wakifuatilia hotuba yake kwa taifa kuhusu kuuwawa kwa Osama.Kutoka Kulia kwenda Kushoto ni Makamu wa Rais Joe Baden,Waziri wa Nje Hillary Clinton,Mkuu wa Majeshi ya Marekani Jenerali Mike Mullen,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) Leon Panetta,Mshauri wa Rais katika usalama wa taifa Tom Donilon,na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa James Clapper.




Rais Obama akiwahutubia Wamarekani na dunia kutangaza kuuawa kwa Osama Bin Laden




Rais Obama akipena mkono na Mkuu wa Majeshi ya Marekani Jenerali Mullen baada ya hotuba yake.Wengine pichani ni Hillary Clinton na Mkurugenzi Mkuu wa CIA Panetta.
CHANZO: Picha za Ikulu ya Marekani katika tovuti ya picha ya Flickr

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.