Showing posts with label SYNOVATE. Show all posts
Showing posts with label SYNOVATE. Show all posts

4 Aug 2011


Tanzania yetu sijui inaelekea wapi!Yaani ufisadi unasambaa kila kona.Wengi mnakumbuka usanii waliofanya kampuni ya utafiti ya Synovate wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.Kwa kifupi,waliamua kuweka kando professionalism na hadhi ya kampuni yao ili wawaridhishe watu wa CCM.Nilikerwa sana na uhuni wao hadi nikafikia hatua ya kumwandikia bosi wao.Kama ilivyo kawaida ya wababaishaji,aliruka kimanga na kudai hawapendelei chama chochote.

Sasa leo nimekumbana na habari iliyonikera kupita maelezo.Eti kampuni hiyo imefanya utafiti wa kura ya maoni kuhusu nafasi ya urais.Hadi hapo hakuna tatizo kwani tunashuhudia takriban kila wiki taasisi za kura za maoni kama Gallup zikiendesha kura za maoni kupima utendaji kazi wa Rais Obama,Congress,nk.Tatizo la kura ya maoni ya Synovate lipo kwenye ukweli kwamba wamekwepa kumweka Rais Jakaya Kikwete kwenye opinion poll hiyo,na badala yake wameweka wanasiasa wengine,ambapo Dkt Willibroad Slaa ameibuka kidedea.

Synovate wamefanya makusudi kukwepa kupima utendaji kazi wa Kikwete.Wangeweza kabisa kuangalia approval rating yake pasipo kumpambanisha na Dkt Slaa.Lakini wamekwepa kwa vile wanajua bayana kuwa  wengi wa Watanzania wenye akili timamu wamechoshwa na ubabaishaji wa rais wao.

Lakini hata kama Synovate wameamua kuendelea kujipendekeza kwa Kikwete na CCM,hiyo haitoondoa ukweli kuwa wengi wa Watanzania wamemchoka Kikwete,na kwa hakika wanasubiri kwa hamu afungashe virago vyake hapo 2015 (huku kukiwa na hofu kuwa by then nchi itakuwa imeharibika beyond repair).

Sidhani kama Synovate wangeamua kuchapisha approval rating ya Kikwete wangelazimishwa kuondoka Tanzania.Lakini naamini kabisa kuwa kampuni hii inafahamu fika kuwa kuficha kukubalika/kuchukiwa kwa Kikwete hakumsaidii kiongozi huyo dhaifu.Ni sawa na mgonjwa wa ukimwi kufichwa matokeo ya vipimo vya damu yake.Kamwe virusi vya ugonjwa huo havitoondoka mwilini kwa vile tu mwathirika hajajulishwa.

Anyway,habari husia ni hii hapa chini
Dk Slaa ang’ara urais 
Wednesday, 03 August 2011 23:11
0
digg

NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.

Leon Bahati
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.

Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.

Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.

Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: “Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?”
Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

CCM wamtaka Dk Slaa
Utafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.

Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.

Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).

Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.

Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.

Mgombea urais CCM 2015
Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.

Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).

Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.
Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Uvuaji gamba CCM
Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.

Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.

Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.

Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.

Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.

Kero kubwa nchini
Asilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).

Katiba Mpya
Miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).

Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.
Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.

CHANZO: Mwananchi

17 Oct 2010

Moja ya mambo yaliyokuwa yakiwaumiza vichwa wafuasi wa Barack Obama wakati wa kinyang'anyiro kati yake na Hillary Clinton kupata mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats mwaka 2008 ni theory inayofahamika kama Bradley Effect.Kwa kifupi kabisa,Bradley Effect (au Wilder Effect) ni hali inayoweza kutokea kwenye kura za maoni katika chaguzi nchini Marekani panapokuwa na mgombea Mweupe (White) na asiye mweupe (non-White).Pengine ili wasionekane wabaguzi wa rangi,wahojiwa Weupe katika kura za maoni hueleza kuwa chaguo lao ni mgombea asiye Mweupe au husema kuwa hawajafanya uamuzi kuhusu chaguo lao (Undecided).

Kwahiyo,matokeo ya kura ya maoni yanaweza kuonyesha mgombea asiye Mweupe anapendwa zaidi kuliko mgombea Mweupe lakini inapofika kwenye hatua ya kupiga kura (ambapo mpiga kura anakuwa peke yake),wapiga kura Weupe wanampigia Mweupe mwenzao.

Asili ya Bradley Effect ni katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa uchaguzi wa gavana wa jimbo la California mwaka 1982 ambapo licha ya mgombea Mweusi,Meya wa Jiji la Los Angeles Tom Bradley kuongoza kura za maoni,aliishia kushindwa uchaguzi huo kwa mgombea Mweupe George Deukmejian.

Baadhi ya wachambuzi wa chaguzi nchini Marekani wanaamini pia kuwa Bradley Effect ilijitokeza tena kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa chama cha Democrats kwenye jimbo la New Hampshire ambapo licha ya Obama kuongoza katika kura za maoni,Hillary Clinton aliibuka mshindi kwenye jimbo hilo (japokuwa baadaye Obama alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla,na kupitishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Democrats,na hatimaye kushinda nafasi ya urais).

Katika post hii najaribu kubashiri (hypothesize) namna Bradley Effect inavyoweza kuwa sababu ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,kuongoza katika tafiti za  taasisi za Redet na Synovate kuhusu nafasi za wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa Tanzania hapo Oktoba 31.Hapa ntawazungumzia wagombea wawili tu,Kikwete na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

Japo Bradley Effect 'halisi' inahusu mgombea Mweupe na asiye Mweupe,sababu inayopelekea matokeo ya kura kutorandana na mwelekeo wa kura za maoni inaweza kutumika kuelezea kwanini kura za maoni za Redet na Synovate zilimpa Kikwete ushindi na sio Dokta Slaa.Kama ilivyo kwenye chambuzi mbalimbali,kuna mambo flani inabidi 'kupuuzwa' ili kufikia matokeo yanayokusudiwa.Katika uchambuzi huu,naomba 'nipuuze' urafiki kati ya taasisi hizo na CCM na badala yake nikazanie kwenye uwezekano wa Bradley Effect pekee.

Inawezekana kabisa kuwa wahojiwa kwenye tafiti za Redet na Synovate ni wananchi waliotoa majibu 'kuwaridhisha watafiti',yaani walisema wanampenda zaidi Kikwete kuliko Dokta Slaa.Moja ya sababu za kutoa majibu ya aina hiyo ni mazingira halisi ya Tanzania ambapo licha ya 'siasa za mkono wa chuma' za zama za chama kimoja kuonekana kama historia,ukweli unabaki kuwa baadhi ya wananchi wanaamini kuwa kusema lolote lisilowapendeza watawala ni kujitafutia matatizo.

Naomba kufafanua kidogo katika hilo.Nilipokwenda Tanzania mwaka 2005 kufanya fieldwork ya utafiti wangu wa shahada ya uzamifu (PhD) nilikumbana na wakati mgumu kuwahoji baadhi ya maustaadh (mada yangu inahusu masuala ya Waislam na Uislam nchini Tanzania) kwa vile baadhi yao walidhani mie ni wakala wa serikali niliyetumwa kuwachunguza ili 'serikali iweze kuwadhibiti zaidi'.Bahati mbaya,fieldwork hiyo ilifanyika wakati jeshi la polisi lilikuwa linamsaka mwanaharakati wa Kiislam,Sheikh Issa Ponda.Ilichukua kitambo kujenga uaminifu kati yangu na maustaadh hao.

Kuna wanaoilaumu Redet na Synovate kuhusu aina ya watu waliohojiwa wakidai kuwa huenda wahojiwa walikuwa watu walio karibu na CCM (kwa mfano mabalozi wa nyumba kumi).Uwezekano wa Bradley Effect  'yetu' (yaani isiyohusiana na ishu za ubaguzi wa rangi) ni mkubwa kwa vile wahojiwa wanaweza kutoa majibu yasiyoonyesha 'wanambagua mgombea wao' na hivyo kusema huyo ndio chaguo lao japo mioyoni wana dhamira na/au chaguo tofauti.

Of course,inawezekana tafiti hizo za Redet na Synovate 'zilipikwa' ili kuendana na matakwa ya CCM.Inawezekana pia kuwa aina ya watu waliohojiwa ni ambayo isingetoa majibu tofauti na 'ushindi kwa Kikwete'.Lakini,kama makala hii inavyojaribu kubashiri,inawezekana kabisa kuwa wahojiwa 'waliwazuga' jamaa wa Redet na Synivate 'ili isiwe shida'.Nani yuko tayari kuona genge lake au kibanda cha biashara kinabomolewa kwa vile tu amechoshwa na namna CCM inavyozidi kuahidi maisha bora lakini wanaonufaika ni mafisadi pekee?Mtu wa aina hii haoni shida 'kudanganya leo' kisha 'akaungama siku ya kupiga kura' kwa 'kumwadhibu Kikwete na CCM kwenye sanduku la kura ambapo hakutokuwa na wa kumtoa mimacho kwanini hajampigia kura Kikwete au CCM'.

Huu ni ubashiri tu.Unaweza kuwa sio sahihi lakini kama zilivyo bashiri nyingine-hususan zinazoambatana na mifano hai-unaweza kuwa na ukweli ndani yake.Kadhalika,Bradley Effect 'yetu' inaweza kutoa matokeo ya kuwashangaza wote wenye imani kuwa CCM na Kikwete watarudia kupata ushindi wa kishindo kama wa mwaka 2005.

Pengine kuna watakaohoji kwanini Bradley Effect 'yetu' haiwezi kutumika kwenye utafiti mwingine (wa TCIB) unaoonyesha kuwa Dokta Slaa anaongoza.Jibu langu ni kwamba watoa maoni hawana cha kupata (nothing to gain) kuwadanganya watafiti kuwa wanampenda Dokta Slaa wakati ukweli wanayempenda ni Kikwete.Likewise,kwenye tafiti za Redet na Synovate,inawezekana baadhi ya wahojiwa walikuwa na cha kupoteza laiti wangesema hawampendi Kikwete (si unajua kuhusu umoja na mshikamano ndani ya chama?).Vilevile,yawezekana wahojiwa hawakuwa na cha kupoteza (nothing to lose) kwa kudanganya kuwa wanampenda Kikwete (kwa minajili ya kuwaridhishwa watafiti na 'kulinda ugali wao') kisha wakamnyima kura katika usiri wa chumba cha kupigia kura.

Mwisho,naomba kusisitiza tena kuwa hypothesis hii imejaribu kupuuza sababu za 'wazi' kama vile upendeleo wa watafiti,uoga wa wahojiwa,na kubwa zaidi,UCHAKACHUAJI.

20 Sept 2010

Last night,I wrote an email to Synovate Tanzania Country Manager,Aggrey Oriwo.I am really grateful to him for responding to my email in which I enquired why their recent survey intentionally avoided disclosing which presidential candidate was leading in the race.In his reply,Oriwo categorically refuted my allegation that his organisation was playing politics in favour of the ruling party CCM.He went further to point out that Synovate is a company owned by Aegis Group,a global giant which is listed on the London Stock Exchange.

However,although Oriwo explained that their recent  survey  primarily focused on how local media covered the election campaigns,he did not clarify as to why it lacked a question,or rather an answer to the public,on voting intentions.

Well,one doesn't have to be a genius to assume that had Kikwete or CCM been leading in the polls,Synovate-and most likely REDET,would have already publicised their "findings".

Now I see the logic in the saying "ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS".Synovate's silence has unintentionally revealed what the pollster is trying to conceal to the public: Kikwete is certainly trailing in the polls.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.