Showing posts with label TAZARA. Show all posts
Showing posts with label TAZARA. Show all posts

14 Oct 2008

 Choo katika behewa la First Class TAZARA

Habari hii imenisikitisha sana kwa vile inanigusa binafsi.Ili nifike nyumbani Ifakara nina choices mbili ambazo zote si nyepesi.Kuna usafiri wa barabara ambao kwa hakika unahitaji moyo hasa kutokana na ubovu wa barabara kuanzia maeneo ya Ruaha/Kilombero.Kana kwamba hiyo haitoshi,wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kwenda mikoani ni kama wameisusa barabara ya kwenda kwetu kwani takriban mabasi yote yaendayo huko ni mikweche ya daraja la kwanza.Mabasi kama Moro Best,Islam na Chimpanzee yamechoka kupita kiasi,na yanaendelea kutumika kwa vile tu  imekuwa kawaida yetu Watanzania kuvumilia mateso.Kikwazo kikubwa cha usafiri wa barabara ni msimu wa masika.Kuna eneo sugu kati ya Mang'ula na Kiberege ambapo kupita kunahitaji zaidi ya sala na trekta linalovuta mabasi yanayokwama kwenye matope.

 Kiza katika Stesheni Kuu ya TAZARA Dar es Salaam.Imagine kama stesheni kuu ni hivyo,stesheni ndogo itakuwaje!

Mkombozi wa wengi alikuwa TAZARA japo mara ya mwisho nilipotumia huduma zao (tena daraja la kwanza) nilitamani kulia:madirisha hayafungiki,taa zinawaka kwa kubembelezwa na vyoo ni kama kwenye baa za uswahilini.Ili ushuke kutoka behewani hadi kwenye platform ya stesheni ni muhimu kuwa mwanamazoezi wa short- au long-jump.Sasa ndio hata huduma hiyo ya kichovu nayo imepunguzwa ambapo kutakuwa na safari mbili tu kwa wiki,moja ya express na nyingine ya ordinary.Sishangai TAZARA kuchukua uamuzi huo kwani shirika hilo muhimu liko mahututi intensive care,hali yake ni mbaya na linasubiri kufa kifo cha kizembe siku si nyingi.

 Adha ya usafiri wa barabara kwenda kwetu Ifakara

Najua siko peke yangu ninaesononeshwa na habari hii lakini japo wanasema kilio cha wengi ni harusi ukweli unabaki kwamba Maisha Bora kwa "wana wa pakaya" yanazidi kuwa a distant pipedream.

23 Apr 2008

Naamini wengi wenu mnakikumbuka kibao cha "Ingekuwa Vipi" cha wasanii Jay-Mo na Mwanafalsafa.Nakipenda,sio kwa beats zake pekee,bali pia kimebeba ujumbe mzito wenye maswali mazito.Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la Raia Mwema imeanza kwa kunukuu verse moja ya wimbo huo,lengo likiwa sio uchambuzi wa muziki bali kufanya tafakuri kuhusu mwelekeo wa mambo katika nchi yetu.Tangu nifike hapa nyumbani takriban wiki tatu zilizopita,nimekutana na watu kadhaa ambao wamekuwa wakidai BORA MKOLONI ARUDI KUTUTAWALA.Aliyenisukuma zaidi kujadili suala hili ni abiria mwenzangu niliyesafiri nae katika chumba cha "daraja la kwanza" cha TAZARA,ambaye nae alidai kwamba "Bora Mkoloni arudi" baada ya adha lukuki zilizotupata katika safari yetu.Mie nadhani bora Wachina warejeshewe TAZARA kwani sie Waswahili imetushinda.Hilo la Mkoloni kurudi sina hakika nalo sana,ila ni dhahiri kwamba kuna wanaharamu wanaotutesa mara 100 zaidi ya walivyofanya wakoloni.By the way,wakoloni hawakuwa Watanzania wenzetu,lakini hawa washenzi wanaotufisadi na kulimbikiza fedha (wenyewe wanaita vijisenti) huko nje ni watu tuliozaliwa nao nchi moja iitwayo Tanzania.Makala yangu hiyo imehitimishwa kwa onyo kwa CCM kwamba ikiendeleza porojo zake za Maisha Bora kwa kila Mtanzania (or did they mean "kwa kila fisadi"?) basi wasishangae wakikutana na yaliyowakuta KANU huko Kenya.Ukisikia wananchi wanatamani Mkoloni arudi basi hizo ni dalili kuwa wamechoshwa na porojo za watawala.Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti la Raia Mwema,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA

Pia kuna picha kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Bongo.



















Nadhani kuna wanaoikumbuka joint moja ya maeneo ya Namanga kuelekea Msasani iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Studi Becker.Sasa hivi inaitwa New Angel.Pengine kwa vile ni ya "Malaika Mpya" ndio maana toilets zao ziko kizani kama inavyoonekana (au isivyoonekana?) katika picha.


















Picha hizi nzuri (hapo juu na zinazofuata chini) zimepigwa na dada mmoja mrembo wa Hoteli ya Kempinski (ameomba jina na sura yake vihifadhiwe) kutoka ghorofa ya sita ya hoteli hiyo.Dada huyo mdau wa blogu hii anadai amepatwa na wazo la kupiga na kunitumia picha hizo baada ya kuona kile "kimbembe cha zule" cha picha za matope ya barabara ya Ifakara.Picha zote zinaonyesha mandhari ya bandari ya Dar es Salaam,minus ufisadi wa Mamlaka ya Bandari na TICTS.







21 Apr 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inaelezea kwa kirefu nightmare niliyokumbana nayo baada ya kuingia mkenge wa kusafiri "first class" ya Tazara.Hiyo ilikuwa wakati naelekea nyumbani Ifakara mkoani Morogoro.Baada ya mateso ya hiari huko Tazara,nikaamua usafiri wa kurudi Dar uwe kwa njia ya Barabara.Nadhani picha zifuatazo zinatosha kukueleza namna Maisha Bora kwa kila Mtanzania yanavyowezekana.Kuna jamaa aliyeziona picha hizi kabla sijaziposti amenitania kwamba heri wale ambao "nyumbani" ni Dar es Salaam na si Ifakara,et al kwani hawahitaji Tazara wala matrekta ya kuvuta mabasi.Nikamuuliza iwapo Dar es Salaam anayozungumzia ni ya Oysterbay na Upanga au ile ya Mwananyamala kwa Ali Maua au Mbagala Kibondemaji...kwani alijibu!?
















15 Apr 2008

MASHABIKI WA SOKA WA IFAKARA WAKIFUATILIA MECHI KATI YA TAIFA STARS NA HARAMBEE STARS YA KENYA
HUYU NYAU ANAJARIBU KU-GOOGLE NENO "UFISADI"
HIKI NI CHOO NDANI YA BEHEWA LA DARAJA LA KWANZA LA TAZARA.EVER HEARD OF A TRAIN FROM/TO HELL?
UFISADI KUTOKA CHINA: HII NI PIRACY YA DARAJA LA KWANZA (ZAIDI YA LILE LA TAZARA).MOVIES TAKRIBAN 40 ZIMELUNDIKWA KWENYE DISC MOJA.BEI MAELEWANO.HI SAMPLE NILINUNUA KWA SHS 5000.NAOMBA KUSISITIZA KUWA NILINUNUA ITEM HII KWA AJILI YA KUKUONYESHA WEWE MSOMAJI WA BLOG HII,NA SIO KUWANUFAISHA MAFISADI.TRUST ME!
UFISADI,CHINESE STYLE
HIVI UNAWEZA KU-GUESS HAPO NI WAPI?I DONT THINK SO.NI RAHISI ZAIDI KU-EXTRACT DAMU KUTOKA KWENYE JIWE KULIKO KUPATA JIBU SAHIHI KWENYE KIJISWALI HIKI.ANYWAY,HAPO NI KWENYE PLATFORM YA KUONDOKEA,STESHENI KUU YA TAZARA DAR ES SALAAM,NA HILO DUDE KULIA NDIO TRENI LA KWENDA ZAMBIA.MWANGA HAPO NI HAFIFU ZAIDI YA ZILE DISCO LIGHTS ZA KIZAMANI.NDANI YA HILO DUDE LIITWALO TRENI NI ADHABU FROM THE MOMENT UNAINGIA TILL UPOTEREMKA UENDAKO ("KUTEREMKA" IS A POLITE WORD,"KURUKA" WOULD BE MORE PRECISE)
ANGALIA KWA MAKINI "TAIFA LA KESHO" (WATOTO) WAKIFUATILIA MECHI YA TIMU YETU YA TAIFA HUKUWAKIWA WAMEKAA CHINI.HAPA NI IFAKARA.RUNINGA ZIPO MADUKANI LAKINI NI AFFORDABLE KWA WATU WACHACHE.UNYANYASAJI WA WATOTO HAPA NYUMBANI UNAPASWA KUTANGAZA JANGA LA KITAIFA.NOBODY SEEMS TO CARE JAPO KUNA WIZARA INAYOHUSIKA NA MASUALA HAYA.NA HAKUNA SEHEMU NZURI YA KUPIMA POROJO ZAMAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KAMA HUKU UPCOUNTRY.

MORE PICS LATER,STAY TUNED!

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.