Nianze
makala hii kwa kuwashukuru ndugu nyote mlionitumia salamu za upendo,kunipa pole/kunipa
moyo baada ya jina langu kutajwa miongoni mwa watu 9 wanaodaiwa kuwa hatari kwa
usalama wa Tanzania.
Orodha
hiyo ilitajwa na mtu mmoja anayejiita Cyprian Musiba japo taarifa nilizonazo ni
kwamba jina hilo lina walakini kama lilivyo jina la rafiki yake – na miongoni
mwa watu waliofanikisha press conference yake – Daudi Albert Bashite. Waingereza
wanasema "birds of a feather flock
together."
Kichekesho
ni kwamba mara ya kwanza kumfahamu mtu huyo ni wakati flani aliponitumia ujumbe
kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akinifahamisha kuwa wana gazeti lao
linaitwa 'Tanzanite' na kuniomba niwe nawatumia makala. Nilipuuza ombi hilo kwa
sababu kutoka level ya kuandikia gazeti kubwa kama Raia Mwema kwenda kuandikia
kijigazeti kipya kama hicho cha Tanzanite ingekuwa kujishushia heshima yangu.
Kwa
upande mmoja,tuhuma za huyo mtu hazijanishangaza kwa sababu kadhaa. Kwanza,
tunafahamu fika ugumu wa maisha huko nyumbani, na sio suala la ajabu kuona
baadhi ya watu wakiuza utu wao ili mradi tu "njia ya kwenda msalani isiote
nyasi."
Lakini
pili, kuna jitihada kubwa za kuigeuza Tanzania kuwa kama wilaya ya Kanda ya
Ziwa. Huyo mtoa tuhuma ana asili ya maeneo hayo, na kuna hali inayozidi kuota mizizi
kwa baadhi ya wahuni wanaotoka eneo moja na Magufuli kujiona wana hatimiliki ya
Tanzania yetu.
Jingine
ambalo lilinifanya nipuuze hizo tuhuma za huyo bwege ni ukweli kwamba safari
yangu kimaisha hadi hapa nilipo imepshapitia vilima na mabonde. Nimeshaeleza
mara kadhaa kuhusu janga lililonisibu Februari 2, 2013 ambapo chombo kimoja cha
usalama hapa kilinifahamisha kuwa kuna tishio dhidi ya uhai wangu, tishio from
Tanzania. Na kwa zaidi ya mwaka mzima tangu wakati huo, nikawa ninaishi maisha
ya kutambua kuwa muda wowote ule naweza kudhurika. Licha ya ugumu mkubwa, hali
hiyo ilinipa uzoefu wa kuishi na vitisho.
Lakini
pia, hiyo hatua tu ya huyo mzembe kunituhumu naona kama tusi flani kwangu. Mie
sio wa kutuhumiwa na mtu asiyejulikana kama yeye. Ilipaswa labda awe kigogo
flani wa Usalama wa Taifa, ndo ningeweza kuchukulia suala hilo seriously.
Wanasema "usiongee na mbwa bali ongea na mwenye mbwa."
Hata
hivyo, japo sikushangazwa na tukio hilo la kihuni, nilikerwa na vitu vikuu
vitatu. Kwanza, wakati nina uhakika wa asilimia 100 kuwa huyo bwege ametumwa tu,
nilikerwa mno na uongo wa mchana kweupe uliokuwemo kwenye tuhuma zake. Uongo
huo ni pamoja na kudai kuwa FBI ni shirika la ujasusi la Marekani. Hivi hao
wapuuzi waliomtuma hawakufanya research japo kidogo ya kuwaelewesha kuwa
shirika la ujasusi la Marekani ni CIA na sio FBI?
Halafu
huyo bwege akachapia tena kwa kudai kuwa chama cha Kansela Angela Markel ni CDP
ilhali chama chake ni CDU. Halafu sijui ni mie tu na "macho yangu ya
kishushushu" niliyeona huyo jamaa akiongea kwa kuhema kana kwamba
anakimbizwa, huku amejawa na uoga mkubwa. Hizi njaa zitakuwa watu mwaka huu.
Seriously!
Kingine
kilichonikera ni jinsi huyo bwege alivyopewa umuhimu mkubwa asiostahili. Hivi
kwa mfano hiyo video ya press conference yake ingepuuzwa, nani angejua kuwa
kuwa mwendawazimu flani kuitisha press conference kutuhumu watu kadhaa wenye
heshima zao katika jamii? Kuna nyakati ukimya una nguvu zaidi ya kupigiana
kelele na mtu. So far, huyo mhuni amefanikiwa kufikisha ujumbe wake kwa watu
wengi mno kutokana na sie wenyewe – including tuliotuhumiwa -kumsaidia
kusambaza ujumbe wake muflis. Anyway, by muda huu hizo 15 minutes of fame
zimeshaisha muda wake.
Lakini
pia nilikerwa na ukweli kwamba uhuni wa aina hii ukiachwa tu bila kuchuliwa
hatua unaweza kusababisha madhara makubwa huko mbele. Maana tumeshaona jinsi Bashite
alivyoweza kuvamia studio za Clouds kisha Rais Magufuli bila aibu akamtetea
hadharani na kumsifia kuwa ni mchapakazi. Kwa kifupi, huko ni kusherehesha
uhuni.
Sasa
huyu bwege si mara ya kwanza kuibuka na press conference za kiendawazimu.Last
time aliitisha press conference na kutishia kumfungulia mashtaka shujaa Tundu
Lissu. Katika tukio hilo nilikerwa zaidi na ukweli kwamba kuna viumbe wenye
roho mbaya kama wachawi, ambao hawajatosheka na mateso aliyepitia Lissu baada
ya karibio la kutaka kumuuwa. Mie nimesoma"War Studies" na miongoni
mwa kanuni za vita ni kwamba pindi adui yako akiwa chini basi unatarajiwa kutomdhuru.
Kwahiyo hata kama Lissu ni adui yao, basi angalau wangesubiri apone kwanza
kabla ya kuanza kumwandama namna hiyo
Kwa
taarifa nilizonazo, press conference ya huyo bwege inamhusisha Bashite ambaye
bila shaka ana baraka za baba yake, lakini pia watu wa Kitengo nao wamehusika.
Ni vigumu kujua "kitengo kipi" maana kwa sasa ni kama tuna "Idara
mbili" – hiyo tunayoifahamu na hiyo "kampuni binafsi ya ulinzi wa
JPM/Bashite."
So who is this man Cyprian Musiba? Surely someone was behind his press conference: Is it @MagufuliJP? Bashite or TISS?
I'll have answers soon
| Je mtu huyu Cyprian Musiba ni nani? Kwa hakika ametumwa: Je ametumwa na Magufuli? DAB au Kitengo?
Lakini
kubwa zaidi, na hasa ndio lengo la makala hii ni kuwafahamisha Watanzania
wenzangu kwamba tafsiri halisi ya tuhuma zilizotolewa kwenye hiyo press
conference ni kuwafanya ninyi Watanzania hamna akili ya kuweza kubaini nani
hasa ni tishio kwa usalama wa taifa lenu.
Twende
hatua kwa hatua japo kwa umbali mfupi tu.Hivi katika ya hao watu tisa ni yupi
alishiriki kupanga na kutekeleza shambulio la kinyama dhidi ya Lissu? Kibaya
zaidi, Lissu nae yumo katika orodha hiyo.
Je
ni yui kati ya hao tisa alitoa ruhusa kwa askari kumpiga risasi na kumuuwa
binti asiye na hatia Akwilina? Je ni nani kati yetu aliyehusika na mauaji wa
Katibu wa Chadema Kata ya Hananasifu marehemu Daniel na Diwani wa Kata ya Namwawala
Marehemu Luena? Maana kwa matukio haya matatu tu, na pengine la nne ni la
Lissu, inatosha kuonyesha kuwa kuna pattern ya mauaji dhidi ya raia wasio na
hatia. Na kwa vile hakuna jitihada zozote za vyombo vya dola kuwasaka wahusika
na kuwatia nguvuni, yayumkinika kuhisi ushiriki wa serikali ya Magufuli katika
matukio yote hayo.
Sasa
yule bwege kuwaona ninyi Watanzania hamnazo, kwamba "anamudu kuwalisha matango
pori" kwa kudai kuwa huyo na huyu ndiyo tishio kwa usalama wa nchi yetu,
ilhali kila mwenye akili timamu anafahamu bayana kuwa tishio kubwa zaidi kwa
sasa linatoka kwa WATU WASIOJULIKANA.
Je
sie tisa tuliotajwa ndo tumegeuka kuwa "watu wasiojulikana" ambao
sote wenye akili timamu twatambua ndio tishio kwa usalama wa Tanzania?
Ni
rahisi kulitazama suala hilo kama ni uhuni wa huyo mbwa dhidi yetu lakini
kiukweli mbwa huyo kawanyea Watanzania wote wenye akili timamu. Kawafanya hamna
uwezo wa kutofautisha pumba na mchele. Huyu mtu ni adui yenu zaidi ya adui wa
sie aliotutuhumu.
Sasa
je hasira yako dhidi ya mtu huyu na waliomtuma unaionyeshaje? Mie ushauri wangu
ni mwepesi tu: kama una uwezo wa kuwasomea dua mbaya, itakuwa vema. Kama una
utaalamu wa masuala ya asili, basi ni vema pia. Hata ukitukana kimoyomoyo ni
vema pia. Lakini ukipata wasaa wa "kumpa a uso" popote pale – iwe mtandaoni
au mtaani – tafadhali fanya hivyo.
Naamini
kabisa kati ya sie tisa tuliotajwa na huyo bwege, tuna watu walio tayari
kutafuta haki kwa ajili yetu.Na haki si lazima ipatikane mahakamani. Na
mahakama zenyewe hizi zinazoendeshwa kwa rimoti na Magufuli hadi kumfunga Sugu
wala hazina maana. Ombi langu kwenu ni kila aina ya laana dhidi ya mtu huyo, si
kwa sababu labda ana umuhimu flani bali ukweli huo niliyotanabaisha hapo juu
kuwa amewaona ninyi Watanzania kama hamnazo hadi kufikia hatua ya kutuzushia
sie tusio na hatia tuhuma hizo za kuhatarisha usalama ilhali sote tunafahamu
vema akina nani wanaohatarisha usalama wa Tanzania yetu.
Kama
ukinitumia picha wakati unamfanyia kisomo huyo mbwa basi itakuwa vema sana haha
Nianze
makala hii kwa kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki
wa marehemu Daniel John, ambaye hadi alipouawa kinyama alikuwa Katibu wa
Chadema kata ya Hananasifu, na pia kwa familia, ndugu,jamaa na marafiki wa
marehemu Acqulina Akwilin (samahani kama nimekosea jina).
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe,
mwili wa marehemu Daniel uliokotwa kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam
ukiwa na majeraha. Alieleza kuwa awali marehemu alichukuliwa na Land Rover
nyeupe na watu waliohifanya askari polisi, lakini tangu wakati huo Polisi
hawakuwa na taarifa zozote za kiuchunguzi, na hata jitihada za kupatikana mwili
huo zilifanywa na Chadema wenyewe.
DAR: Katibu wa Kata ya Hananasifu(CHADEMA) afariki dunia katika mazingira yenye utata. Mwili wake umekutwa ukiwa na jeraha la Panga kichwani
Kwa upande wa
marehemu Acquilina, kifo chake kilisababishwa na kasumba hatari inayozidi
kuzoeleka kwa watumishi wa vyombo vya dola kufanya mzaha katika matumizi ya
silaha za moto, ambapo katika tukio husika, polisi waliokuwa wakizuwia
maandamano ya wafuasi wa Chadema, walitumia risasi za moto,na moja kati ya
risasi hizo ilipelekea kifo cha binto huyo, ambaye hadi mauti yanamfika alikuwa
mwanafunzi katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) akisomea shahada ya
ununuzi na ugavi.
Ni muhimu
kutambua kuwa vifo vyote hivi viwili vingeweza kuepukika laiti utu na ubinadamu
wetu ungewekwa mbele ya chuki za kisiasa. Huhitaji kuwa mjuzi wa uchunguzi wa
mauaji kufahamu kuwa vifo hivyo ni matokeo ya chuki, hujuma, uonevu na kila
aina ya baya dhidi ya chama kikuu cha upinzani, Chadema, kuhusiana na kampeni
za uchaguzi mdogo katika jimbo la Kinondoni, ambalo kama ilivyo kwa jimbo la
Siha, ni "piga ua" kwa CCM ishinde. Yaani chama hicho tawala kilitarajiwa
kutumia kila mbinu kuhakikisha inashinda katika majimbo hayo mawili.
Lakini kabda
sijaingia kwa undani katika mada hii - ambayo lazima nikiri kwamba inanipa
wakati mgumu sana kuiandika kwa sababu nimebanwa na mchanganyiko wa majonzi na
hasira, sambamba na hofu ya kuona taifa langu likisukumwa kuelekea kwenye
upotevu wa amani na mshikamano wetu – naomba kuweka wazi masuala matatu ya
msingi kunihusu mie mwandishi wa mwakala hii.
Kwanza, mimi
licha ya kuwa na makazi nje ya Tanzania kwa takriban miaka 15 sasa bado no Mtanzania.
Utanzania wangu ni haki nilioirithi kutoka kwa wazazi wangu, na itabaki hivyo
milele. Naeleza hili kwa sababu kuwa wabaguzi wanaopenda kutuhukumu Watanzania
tunaoishi huku ughaibuni, na kutaka tuonekane kama Utanzania wetu sio kamili.
Kwa mantiki hiyo, kama Mtanzania, nina kila haki ya kutoa maoni yangu kuhusu
mustakabali wa taifa letu, hususan katika nyakati hizi ambapo kuna dalili za
wanaotaka kulipeleka kubaya taifa letu.
Pili, mwaka 2015
nilishiriki kikamilifu katika kampeni zilizomwingiza madarakani Rais John
Magufuli. Kwa upande mmoja nililazimika kumkampenia Magufuli kwa vile nilikuwa
nina "sababu binafsi" dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu, mgombea
urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa. Wanasema "adui ya adui yako ni
rafiki yako."Kwa upande mwingine, nililipwa kutoa huduma ya ushauri wa
kitaalamu (usadi, yaani consultancy kwa kimombo) hususan kwenye mitandao ya
kijamii. Natanabaisha hili ili asije akakurupuka mtu na kusema "ah
ulishiriki kutupigia kampeni kwa vile tulikupa pesa."
Tatu, huko nyuma
nilikuwa mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Na kabla ya kuanza utumishi
katika taaluma hiyo muhimu na nyeti, nilikula kiapo kwa nchi yangu, kiapo
ambacho nitaishi nacho hadi ninaingia kaburini. Kiapo hicho sio cha kukitumikia
chama flani au viongozi wake bali Tanzania yetu. Nchi ni muhimukuliko vyama vya siasa au wanasiasa.
Mtu aliyepikwa
na kuiva kwenye taaluma ya uafisa usalama wa taifa, katika nchi yoyote ile, anapaswa
kubaki kuwa mtiifu kwa nchi yake bila kujali yupo ndani au nje ya ajira ya
taasisi inayohusika na usalama wa taifa wa nchi husika.
Wanasema hata
nje ya ajira rasmi, kila mtu aliyewahi kuwa afisa usalama wa taifa anaendeshwa
na "sense of public duty born in
their previous lives" yaani wajibu kwa umma uliozaliwa katika maisha
yao huko nyuma. Jasusi mmoja mstaafu anaeleza “...I have obligations, professional obligations. If there’s a national
security emergency or possible national security issue, I should report it."
“ ‘You know, I have obligations, professional obligations. If there’s a national security emergency or possible national security issue, I should report it.’ ” ~ Steele
Kwahiyo, hata
kama "maafisa wenzangu wa zamani" wataamua kukaa kimya kwa sababu
moja au nyingine – wengi wanahofia usalama wa maisha yao – sie wengine hatuwezi
kukaa kimya, hasa kwa vile baadhi yetu tumeshalipa gharama kubwa kwa kelele
zetu. Kukaa kimya ni sawa na kuafiki uhuni unaoendelea ambao ni tishio kwa
usalama wa taifa.
Lakini licha ya
wajibu huo unaotokana na utumishi wetu kwa nchi huko nyuma, Rais Magufuli
amefanikiwa kuvifunga mdomo vyombo vya habari kiasi kwamba haviwezi kusema
lolote kuhusu "mabaya" yake, na amefanikiwa kuvijengea nidhamu ya
uoga vyombo hivyo vya habari kiasi kwamba habari pekee zenye umuhimu kwao ni za
kumtukuza na kumpamba "mungu-mtu" huyo. Kwahiyo na sie tuliopikwa na kuiva kuhusu ujasiri, kujitoa mhanga na kutokuwa waoga tukiufyata na kukaa kimya - ilhali media zetu ndio zishapigwa kufuli - hali itazidi kuwa mbaya.
Rais wa Tanzania John Magufuli ayaonya baadhi ya magazeti nchini humo https://t.co/grUpqa52uq
Baada ya kuweka
wazi nafasi yangu, sasa tuangalie kwa kina kinachoendelea huko nyumbani hasa
kuhusiana na uchaguzi mdogo kwenye jimbo la Kinondoni na Siha na kuuawa kwa Daudi
na Acquiline.
Ni muhimu
kutambua kwamba ukandamizaji dhidi ya vyama vya upinzani sio kitu kilichoanza
chini ya utawala wa Magufuli bali hali hiyo imedumu mfululzo tangu kuanzishwa
kwa mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1992. Labda kilicho tofauti kwa zama
hizi ni "ujasiri" wa Magufuli kutoficha chuki yake dhidi ya vyama vya
upinzani. Yaani angalau akina Mwinyi,Mkapa na Kikwete walikuwa "wanauma na
kupuliza." Kwamba angalau walikuwa na "mshipa wa aibu" na
walijitahidi japo kutowaonea Wapinzani waziwazi.
Kwa wanaojua
"yanayojiri nyuma ya pazia" watakwambia kuwa hujuma dhidi ya vyama
vya upinzani ni miongoni mwa vipaumbele vikubwa kwa CCM na serikali zake, na
hiyo imepelekea kujengeka "symbiotic relationship" kati ya chama
hicho tawala na taasisi za dola, ambapo kila mmoja anategemea uhai wa mwenzie.
Lakini kama kuna
kitu kinachokera zaidi kuhusu hujuma dhidi ya demokrasia ni pale CCM na taasisi
zake hasa za dola wanapoweka mbele maslahi yao mbele ya utu na uhai wa
Watanzania. Na hili halijaanza jana au katika kampeni za chaguzi ndogo katika
majimbo ya Kinondoni na Siha.
Uchaguzi mkuu wa
kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 ulihusisha matukio mengi tu ambayo kwa
makusudi hayapo kwenye kumbukumbu za wazi (japo yamehifadhiwa mahala flani).
Lakini kama
wanavyosema "amekula asali sasa anachonga mzinga," baada ya hujuma za
kimyakimya za mwaka 1995 kuzaa matunda, CCM na taasisi zake ikanogewa, na
matokeo yake ni kwamba uchaguzi mkuu uliofuata, mwaka 2000 uliweka doa kubwa
kwa historia ya Tanzania yetu ambapo kwa mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha
wakimbizi kufuatia unyama uliofanyika huko Zanzibar na kupelekea vifo kadhaa (idadi halisi ya vifo haijawahi kuwekwa hadharani japo "wenyewe"
walisema zaidi ya watu 19 ndio waliokufa kwenye machafuko hayo. Wasichosema pia
ni idadi ya watu waliobakwa, kuteswa na kuwekwa kizuizini.
Kwamba hujuma
hizo za CCM dhidi ya demokrasia zilipelekea vifo na majeruhi ni kitu kibaya
kabisa. Lakini kitu kingine kibaya ni ukweli kwamba hakuna mtu hata mmoja
aliyechukuliwa hata kutokana na unyAma waliofanyiwa Wazanzibari hao.
Kwa namna ya
kipekee, CCM ikawa kama imepewa ruhusa ya kutumia vyombo vyake vya dola kufanya
lolote itakalo ili ifanikishe hujuma zake dhidi ya Wapinzani na demokrasia kwa
ujumla, kisha iibuke na ushindi.
Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2005 ulikuwa na "uchafu kupindukia." Kundi lililofahamika kama "mtandao"
lilijipenyeza katika kila sekta, kuanzia kwenye vyombo vya habari, taasisi za
dola hadi kwenye taasisi za dini. Yayumkinika kabisa kuhitimisha kwamba
yaliyojiri wakati "mtandao unafanya jitihada za kumwingiza mtu wao
Ikulu" ni mabaya zaidi ya haya tunayoshuhudia sasa tangu Magufuli aingie
madarakani.
Kwanini basi
hayo yaliyojiri kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 hayajulikani? Jibu ni
kwamba, wakati mbinu iliyotumika mwaka 1995 na 2000 ilitegemea zaidi vyombo vya
dola, uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010 ulitegemea zaidi nguvu ya fedha, nyingi
zikiwa fedha haramu. Na sehemu ya fedha hiyo ilitumika "kununua ukimya" wa wanahabari wengi tu. Lakini si fedha tu bali pia kuna hujuma mbalimbali –
nyingine chafu na za kuchefua – zilizotawala safari za ushindi wa chama tawala
kwenye chaguzi hizo.
Labda tofauti
nyingine kuhusu mwaka 2005 na 2010 ni ukweli kwamba wakati chaguzi hizo
zilihusisha "kikundi binafsi" yaani hicho cha wanamtandao ambacho
hakikuwa taasisi ya serikali au chama.
Lakini muda wote
huo, CCM ilikuwa kama imepwa ruhusa na Watanzania kuendeleza hujuma zake dhidi
ya Wapinzani na demokrasia kwa ujumla. Hakujawahi na utashi miongoni mwa
Watanzania kutaka kukabiliana kwa dhati za uhuni/uhalifu wa kisiasa. Na kwa
bahati mbaya, kwa vile vipaumbele vya Watanzania wengi ni kwenye
"ubuyu" na "kubeti/mkeka" basi habari mbaya ni uwezekano wa
CCM kuendelea kufanya itakavyo kwa muda mrefu sana.
Sio kama kwa
kubashiri kuwa unyanyasaji wa CCM utaendelea muda mrefu sana ninamaanisha kuwa
nimekata tamaa. Hapana. Ninakuwa mkweli tu. Tatizo ni zaidi ya CCM na uhuni
wake. Watanzania wenyewe ni sehemu ya mfumo unaowezesha CCM kufanya uhuni/uhalifu
huo.
Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 ulihusisha pia matuki kadhaa yaliyojiri "nyuma ya pazia."
Na ukitaka kufahamu kuwa Tanzania yetu haijawahi kuhangaishwa na mauaji ya
kisiasa – kuanzia yale ya mwaka 2001 huko Zanzibar hadi haya ya Daudi wa Hananasifu
na dada Acquilina – ni kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila.
Kwahiyo, na
ninaandika haya kwa uchungu mkubwa uliochanganyika na hasira, kuuawa kwa Daudi
na Acquilina kutaishia kuwa moja tu ya matuko yaliyowahi kutokea katika
Tanzania yetu. Tutawasikia wanasiasa wetu wa vyama vya upinzani wakiongea kwa
hisia kubwa. Tutashuhudia pia wanafiki wengi tu miongoni mwa wasanii wetu nao
wakijifanya kuguswa na vifo hivyo, lakini wakiwa makini kuepuka kumuudhi
"Bashite na baba yake" au kuitibua CCM. Tutashuhudia pia kundi la
wanafiki hatari ndani ya CCM wakijifanya kuumizwa na mauaji hayo, na kutaka
uchunguzi ufanyike, ilhali nao ni kondoo waliojivika ngozi ya mbwa mwitu.
Cheap politics + unafiki. Mbwa mwitu wanaojivika ngozi ya kondoo. Inapofika wakati wa kujitoa mhanga kwa minajili ya kuondoa mfumo kandamizi, hawa wanafiki huonyesha rangi yao halisi na kujivika ukada. https://t.co/39aZHTpFQt
Bora tu JPM au Polepole ambao wapo honest kuhusu chuki zao kwa Upinzani/Wapinzani kuliko wanafiki "wanaouma na kupuliza." Bora maadui milioni kuliko "rafiki" mmoja mnafiki https://t.co/39aZHTpFQt
Kama ambavyo
"mauaji mengine ya kisiasa" yalivyoruhusiwa kupita kimyakimya, ndivyo
unyama huu uliofanywa dhidi ya Daudi na Acquilina utakavyoruhusiwa uishe
kimyakimya.
Kwa upande mmoja
tusitarajie Rais Magufuli awajibike – sio kwa yeye binafsi kujiuzulu kwa sababu
hilo litakuwa kutarajia zaidi ya muujiza – kwa kumtimua Waziri husika na watendaji
katika jeshi la polisi. Kwa upande mwingine, hakuna wa kumshinikiza Rais
Magufuli achukue hatua stahili dhidi ya wahusika.
Na nisingependa
kuuma maneno hapa. Yeye Magufuli mwenyewe ni chanzo muhimu cha siasa hizi za
uhasama zinazoendelea kuitafuna Tanzania yetu. Huyu ni mtu ambaye wala hapati
shida kuonyesha chuki zake za waziwazi dhidi ya Wapinzani, Upinzani na
demokrasia kwa ujumla.
Tufike mahala tuambiane ukweli: @MagufuliJP anaipeleka Tanzania kusikostahili. And that is too bad. But what's even worse ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanasubiri miujiza, kwamba siku moja huyu bwana atabadilika. He won't. Worse is yet to come (God forbid)#MarkThisTweetpic.twitter.com/Uy3VnkOKOH
Kama ilivyo kwa
madikteta wengine duniani, Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutumia
ajenda yake ya ufisadi kama kisingizio cha kusigina haki za binadamu nchini
Tanzania, na kubinya kila fursa ya haki za kidemokrasia na uhuru wa habari. Kama
nilivyoeleza awali, amefanikiwa kuviziba midomo vyombo vya habari na ndio maana
hata habari za kusikitisha kuhusu mauaji ya Daudi na Acquiline hazijaripotiwa
vya kutosha.
Kwa kuviziba
midomo vyombo vya habari Magufuli amefanikiwa kuzuwia "habari asizozipenda"
na ndio maana hadi muda huu ni Watanzania wachache tu wanaofahamu kilichojiri
huko MKIRU katika kilichoitwa "operesheni dhidi ya ugaidi." Kuna siku
yaliyojiri huko – na ambayo yamechangia "kupotea" kwa mwandishi wa
gazeti la Mwananchi Azory Gwanda – yatajulikana hadharani. Haijalishi itachukua
miaka mingapi.
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema mwandishi wa Mwananchi aliyetekwa, Azory Gwanda alikuwa anafuatilia taarifa za mauaji ya chini kwa chini yaliyokuwa yanaendelea Kibiti
Lakini
"yaliyojiri MKIRU" ni uthibitisho mwingine wa hicho nilichoeleza hapo
juu kuwa Watanzania wenyewe ndio wanaopaswa kubeba lawama nyingi katika kasumba
ya CCM kutojali uhai katika harakati zake za kukandamiza demokrasia. Kwamba
kama yaliyojiri MKIRU yameachwa yaishe kienyeji, kwanini tutegemee hali tofauti
kwa vifo vya Daudi na Acquiline?
Kama ndugu zetu
wa Chadema (na kila mpenda haki) "wamekubali yaishe" kuhusu kifo cha
Kamanda Mashaka, "kupotea" kwa kada Ben Saanane (hata zile kampeni za
#BringBackBenAlive zimejifia kifo cha asili), na hawasumbuliwi na serikali ya
Magufuli kupuuzia jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu, kwanini tutarajie
jipya katika mauaji yaliyofanywa dhidi ya Daudi na Acquiline?
Yaani Mnadhimu
Mkuu wa upinzani anamwagiwa risasi hadharani wakati mkutano wa bunge unaendelea
huko Dodoma, na tunaambiwa kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo lenye ulinzi
mkubwa na lenye CCTV, kwanini basi wanaosumbuliwa na tukio hilo wasitafute njia
stahili za japo kuifanya serikali ione aibu na kufanya japo "uchunguzi wa
kizushi"?
Kuhusu hujuma
"za kawaida" za uchaguzi, kama kila aina ya uhuni uliofanywa na CCM
kwenye chaguzi ndogo za madiwani katika kata 43 uliofanyika Novemba mwaka jana uliruhusiwa
upite "kimya kimya" – kwa maana kwamba hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
dhidi ya uhuni huo – kwanini basi chaguzi hizi ndogo katika jimbo la Siha na
Kinondoni zilitarajiwa kuwa tofauti?
Na katika hili,
inapaswa wana-Chadema wajiulize kuhusu busara za viongozi wao kuamua kushiriki
katika chaguzi hizo ndogo Siha na Kinondoni ilhali mazingira yaliyokuwepo yalikuwa
yaleyale yaliyopelekea chama hicho kususia chaguzi nyingine ndogo tatu katika
majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini uliofanyika mwezi
uliopita.
Hadi wakati
ninaandika makala hii, tayari Tume ya Uachaguzi ilikuwa imeshamtangaza mgombea
wa CCM jimbo la Siha, Godwin Mollel kuwa mshindi kwa tofauti kubwa tu ya kura dhidi
ya mgombea wa Chadema. Hata kama CCM wameiba kura, ukubwa wa tofauti kati ya
kura za mgombea wao na huyo wa Chadema zinaashiria kuwa chama hicho kikuu cha
upinzani kilipitisha mgombea fyongo.
Mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel ametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 dhidi ya mpinzani wake, Elvis Mosi wa CHADEMA aliyepata kura 5,905 - Mwananchi pic.twitter.com/hG6oT9GUpZ
Na kama
ilivyotarajiwa mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia, naye ametangazwa mshindi.
Breaking news: Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa ticket ya CCM, Maulid Mtulia ametangazwa kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Jimbo la Kinondoni.
Mtulia amepata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353#MillardAyoUPDATESpic.twitter.com/rYsb0Jgbie
Mie mtumishi wako nilishabashiri mapema
tu kuwa chama hicho tawala kingeshinda majimbo hayo, "iwe isiwe."
Ushindi kwa
wagombea hao wa CCM ulipaswa kupatikana kwa gharama yoyote kwa sababu laiti wangeshindwa,
kinachoelezwa kama "mkakati wa Magufuli kuua upinzani kwa kununua wabunge na
madiwani wa Upinzani" kingemfanya
achekwe hata huko kwenye chama chake.
Na kwa vile hadi
sasa wabunge na madiwani waliohama upinzani na kujiunga na CCM wamefanikiwa
kurudi madarakani baada ya chama hicho tawala kuwapa fursa ya kuwa wagombea
wake kwenye chaguzi ndogo, na kuwasaidia kwa hali na mali washinde, tutarajie
wabunge na madiwani wengin zaidi kuhama vyama vya upinzani na kujiunga na CCM.
Kisa? "Dili hilo linalipa," kwa CCM na kwa wanasiasa hao wanaohama.
Na unadhani
mbunge au diwani "mwenye moyo mwepesi" akiona jinsi chama chake "kilivyochukulia
poa" yaliyowasibu akina marehemu Mashaka na Daudi, na yaliyowasibu Ben
Saanane na Lissu, kwanini iwe ngumu kwake kushawishika kuhama?
Ningetamani sana
kuhitimisha makala hii kwa kushauri nini kifanyike lakini itakuwa kupoteza muda
wangu na muda wako msomaji. Ni vigumu mno kuwashauri watu waliokubali kwamba
mgao wa umeme ni stahili yao kwa zaidi ya miaka kumi sasa, na ambao kila mara
umeme unaporudi wanashangilia kana kwamba wamepewa upendeleo flani.
Kama Watanzania
wameshindwa kuilazimisha Tanesko iache mgao wa umeme, wataweza kweli
kuilazimisha CCM iache hujuma dhidi ya vyama vya upinzani na demokrasia kwa
ujumla? Ndio maana bila utu wala aibu, chama hicho tawala kinapata ujasiri wa kukifanyia mzaha kifo cha Acquiline ambapo kwa kudai polisi (haohao waliomuua binti huyo) wachukue hatua dhidi ya Mbowe. Utterly disgusting!
@ccm_tanzania This is too low. Kwanini msitumie akili badala ya makalio kutambua mnachofanyia mzaha huu ni uhai wa Mtanzania uliokatishwa kinyama na polisi haohao mnaowapa kinga kwa kumsingizia @freemanmbowetz? Hamna utu wala mshipa wa aibu? Mungu awalaani kwa hili
cc @MagufuliJPpic.twitter.com/7lgzKh0ofe
Na kama mauaji mbalimbali ya kisiasa huko nyuma yameachwa yapite na
kusahaulika, kwanini tutarajie miujiza kwenye mauaji haya ya sasa dhidi ya
wapendwa wetu Daudi na Acquline?
Na ukweli
mchungu ni kwamba Magufuli ataendelea kuwapelekesha Watanzania atakavyo ka
sababu si watangulizi wake -Mwinyi, Mkapa na Kikwete – wenye jeuri ya kumwambia
"Ee bwana ee, huku unakoipeleka nchi siko." Hawawezi kwa sababu nao
ni kama "mateka." Madhambi waliyofanya kwenye tawala zao yanawafanya
wahofie hatma yao pindi wakimkosoa "mungu-mtu" aliyepo madarakani.
Na wakati
wastaafu au watumishi wa zamani wa Idara za Usalama wa Taifa kwenye nchi kama
Marekani wamekuwa mstari wa mbele kukemea kila tendo linalotishia usalama wa
nchi hiyo – kwa mfano 'ndoa' kati ya Rais Donald Trump na Russia – wastaafu wetu
sie hawana jeuri ya kufungua mdomo sio tu kwa vile wanahofia kuathiri posho na
marupurupu yao bali kwa vile nao ni mateka wa "madudu" waliyofanya
walipokuwa madarakani. Ukiwa mchafu unajinyima uhuru wa kukemea uchafu.
James Comey mkuu wa zamani wa FBI na John Brennan mkuu wa zamani wa CIA ni miongoni mwa sauti muhimu kuhusu mustakabali wa taifa la Marekani. Wako wapi "akina Comey na Brennan" wetu kuhusu mustakabali wa Tanzania yetu? pic.twitter.com/DSA0mWYZ8A
Basi niishie
hapa kwa kurejea tena salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na
marafiki wa marehemu Daudi na Acquiline. Ni vigumu kuwaambia maneno yanayotosha
kuwaliwaza lakini la muhimu ni kuendelea kuzikumbuka roho za marehemu hao, hasa
katika kipindi hiki cha Kwaresma ambapo sisi Wakristu tunaadhimisha mateso ya
Bwana Yesu Kristo. Pumziko la Milele awape Bwana, na Mwanga wa Milele
awaangazie, wapumzike kwa amani. Amen
Jana
Januari 9, 2018, wiki moja na siku mbili baada ya kuanza kwa mwaka huu mpya, duru
za siasa za Tanzania zilitikiswa na habari kuhusu kiongozi maarufu wa Chadema,
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kukutana na Rais John Magufuli kwa “mazungumzo”,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baada
ya “mazungumzo” hayo Lowassa alimmwagia pongezi Magufuli kwa kile alichokiita “kazi
nzuri anayoifanya” na kutaja mafanikio katika sera ya elimu bila malipo, ujenzi
wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s
Gorge), na ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli ya “standard gauge”.
“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana
na Mheshimiwa Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri
anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo,” alinukuliwa
Lowassa aliyejiunga na Chadema miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 baada ya ndoto zake kuwania urais kwa tiketi ya CCM “kuota mbawa.”
Mwanasiasa
huyo ambaye baada ya kujiunga na Chadema alipitishwa kuwa mgombea urais kwa
tiketi ya muungano wa vyama vinne vya upinzani – Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na
NLD – uliofahamika kama UKAWA, aliendelea kusema kuwa “Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza
ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na
kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler’s Gorge
ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha
kusema kwamba tunajenga ajira. Jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi
kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya
kutosha, kwa kweli nakushukuru Mheshimiwa Rais, you made my day.”
Rais
Magufuli kwa upande wake alimpongeza Lowassa kwa kile alichokiita “kutambua
kazi kubwa inayofanywa na Serikali” na kumtaja Lowassa kama mmoja wa viongozi
ambaye kwa wakati wake alitoa mchango wake katika nchi.
Magufuli
alimmwagia sifa Lowassa akidai kuwa “ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi
kumtukana.”
“Mheshimiwa Lowassa ameniomba mara nyingi
nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya
kwake na mimi nimemwambia ya kwangu. Kwa ujumla Mheshimiwa Lowassa ni
mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani
walifanya mambo mazuri, na mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama
alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi,” alisema Rais Magufuli
“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza,
ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7,
amezungumzia juu ya elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati
nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza
juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za
hospitali na mengine” aliongeza Rais Magufuli.
Kwanza,
ni muhimu kutambua kuwa kama Mtanzania yeyote yule, Lowassa alikuwa na kila
haki ya kukutana na Rais wake. Kadhalika, kama mmoja wa viongozi wakuu wa
upinzani, isingepaswa kuwa jambo la kushangaza kwa viongozi hao wawili
kukutana.
Hata
hivyo, Lowassa sio tu amekutana na Magufuli, bali pia ammemwamgia sifa. Je ni
dhambi kwa kiongozi wa chama cha upinzani kumwagia sifa Rais aliyepo
madarakani? Jibu lingepaswa kuwa “si dhambi,” laiti uhusiano kati ya Rais
Magufuli, serikali yake na taasisi zake (kama vile jeshi la polisi, Tume ya Taifa
ya Uchaguzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa), watendaji wa serikali (hasa
mawaziri na manaibu wao, na wakuu wa mikoa na wilaya), pamoja na chama cha Magufuli
yaani CCM, na chama anachotoka Lowassa, yaani Chadema, na Upinzani kwa ujumla,
ungekuwa mzuri.
Lakini
ukweli ni kwamba japo tangu kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992,
uhusiano kati ya CCM, serikali zake na taasisi zake, na vyama vya upinzani
umekuwa “wa kusuasua,” hali katika miaka miwili tu ya utawala wa Magufuli
imekuwa mbaya zaidi hususan kutokana na ukweli kwamba hakuna jitihada za
kuficha chuki iliyopo dhidi ya Upinzani.
Kama
kiongozi wa ngazi za juu kabisa wa Chadema, na pengine mwanasiasa anayeheshimiwa
zaidi ya kiongozi mwingine yoyote ndani ya chama hicho, ni wazi Lowassa
anafahamu vema msimamo na mtazamo wa chama chake kuhusu Magufuli na utendaji
kazi wake, na serikali yake, na chama chake.
Pengine
kwa kuweka picha sawia, inaelezwa kwamba hadi wakati huu, zaidi ya wana-Chadema
400 ikiwa ni pamoja na viongozi na wanachama, aidha wapo jela au wana kesi
zinazoendelea mahakamani ambazo takriban zote ni matokeo ya chuki za kisiasa
zinazofanywa na Magufuli, serikali yake na chama chake.
Kadhalika,
katika utawala wa Magufuli, vyama vya upinzani ikiwemo Chadema ambayo Lowassa
ni kiongozi wake wa kitaifa vimepigwa marufuku kufanya shughuli zao za kisiasa
ikiwa ni pamoja na mikutano na maandamano. Hayo yanatokea wakati CCM ikiwa huru
kufanya mikutano na maandamano itakavyo, mara nyingi ikitumia raslimali za
umma.
Sambamba
na jitihada za Magufuli kubana fursa ya siasa (political space), utawala wa
kiongozi huyo umekuwa mstari wa mbele kuvibana vyombo vya habari na kudhibiti
uhuru na haki ya wananchi kutoa mawazo yao kama Katiba inavyowaruhusu.
Lakini
jingine ambalo Chadema ni mhanga mkubwa, kada maarufu wa chama hicho Ben
Saanane “alipotea” Novemba mwaka jana na hadi leo hajapatikana.
Na
ni wakati ninaandika makala hii nimebaini kuwa Lowassa hajawahi kuongelea suala
la kada huyo (naomba nikosolewe kama nimekosea).
Kubwa
zaidi linaloweza kuhalalisha hasira za Chadema kwa utawala wa Magufuli ni tukio
la hivi karibuni ambapo Mbunge wake maarufu, ambaye pia alikuwa mpinzani
maarufu dhidi ya Magufuli, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kunusurika
kuuawa baada ya shambulio la risasi kadhaa huko Dodoma. Kwa sasa Lissu yupo
nchini Ubelgiji kwa matibabu, lakini japo Lowassa alimtembelea alipokuwa
hospitalini Nairobi, Magufuli hakuwahi kutia mguu kumjulia hali mwanasiasa huyo
ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni na Rais wa Tanganyika Law
Society (TLS).
Kwahiyo
japo pongezi za Lowassa kwa Magufuli zinaweza kuwa na uzito, mapungufu ya
utawala wa rais huyo wa awamu ya tano, hususan kuhusiana na chuki na uonevu
dhidi ya vyama vya upinzani, hususan Chadema, yalipaswa “kumzuwia” kada huyo wa
zamani wa CCM kumwaga pongezi hizo.
Kibaya
zaidi, imebainika kuwa Lowassa alishawahi kumwomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo amsaidie kukutana na Magufuli. Hata hivyo, Gambo alipotamka hilo
hadharani, Lowassa “aliruka kimanga.”
#OMG! So this was actually true. Uzuri wa hii drama ya leo kuhusu Lowassa inathibitisha kuwa sie tuliojivua ushabiki wa Chadema (baada ya ujio wake huko) tulikuwa sahihi. I hope waliotutukana watapata ujasiri wa kutuomba msamaha pic.twitter.com/pctNKaXnaU
Hata
hivyo, jana Magufuli alitamka bayana kuwa Lowassa aliomba mara kadhaa kukutana
naye. Kwahiyo, alichosema Gambo kilikuwa kweli, na Lowassa hakuwa mkweli
alipokana kuwa hajaomba kukutana na Magufuli.
Tukio
hilo la Lowassa kukutana na Magufuli na kumwagia pongezi limepokelewa kwa hisia
tofauti. Wakati kuna kundi dogo la wana-Chadema waliopongeza hatua hiyo, kwa
mfano “kada” mmoja wa chama hicho Yericko Nyerere, wengi ikiwa ni pamoja na
baadhi ya viongozi wamepingana waziwazi na Lowassa.
Wakati
Yericko aliandika haya
Mbunge
maarufu wa Chadema, Godbless Lema alikuwa wa kwanza kueleza bayana kutoafikiana
na pongezi za Lowassa kwa Magufuli.
Mh Lowassa,umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu,mema yapi umeyaona katika Serikali hii?Wkt Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi,maiti zinaokotwa,Uchumi unaanguka,Benki zinafungwa ,demokrasia imekufa Bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza
Baadaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,
Freeman Mbowe, naye alieleza kuwa kauli za Lowassa ni zake binafsi na sio
msimamo wa chama hicho.
"Alichokisema Lowassa leo alipotembelea Ikulu ya Tanzania ni msimamo wake binafsi na wala sio msimamo wa CHADEMA" ~ Freeman Mbowe leo, ameyasema hayo akihojiwa na DW- Idhaa ya Kiswahili jioni hii. pic.twitter.com/WUjOo9qocL
Kadhalika, Mbowe alionekana kumkumbusha Lowassa kuhusu matukio mbalimbali yasiyopendeza katika utawala wa Magufuli
"Kumekuwepo na matukio ya watu kuuawa na kupotea, demokrasia na haki za binadamu zinaminywa, uchumi unazidi kudidimia. Katika mazingira hayo, tunashindwa kuelewa unapata wapi ujasiri wa kuisifu serikali ya Rais Magufuli."- M/Kiti CHADEMA, Freeman Mbowe (Mb) pic.twitter.com/AVXmnNMqg0
Lakini
pengine aliyeeleza kwa kirefu kuhusu suala hilo ni Lissu, ambaye akiwa
hospitalini huko Ubelgiji, alitoa waraka huu hapa chini.
Waheshimiwa
habari za Tanzania na poleni kwa yote.
Naomba
na mimi niseme kwa uchache kuhusu suala hili. Samahani kama 'uchache' wangu
utakuwa mrefu kidogo.
Baada
ya Mwenyekiti kuzungumzia jambo hili, inaelekea kuwa wazi kwamba Mheshimiwa
Lowassa hakumshirikisha Mwenyekiti kabla ya kukubali au kuamua kwenda Ikulu
kukutana na Rais Magufuli.
Na
juzi tu wakubwa wetu hawa wawili walikuwa pamoja hospitalini kumsalimia Mzee
Ngombale Mwiru.
Je,
inawezekana Mheshimiwa Lowassa hakuwa anajua tayari kwamba ana appointment
Ikulu?
Kama
alikuwa anajua, kutokumshirikisha Mwenyekiti wake kuna tafsiri gani hasa?
Katika
mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, uamuzi wowote wa kufanya nae
mazungumzo, hata kwa nia njema yoyote ile, bila kushauriana au kuwashirikisha
viongozi wa juu wa chama, ni uamuzi usio sahihi na mgumu kukubalika.
Vile
vile, kauli za aina ambayo tumeisikia leo kutoka kwa Mheshimiwa
Lowassa, zina athari kubwa kisiasa.
Sio
tu zinachanganya wanachama na wafuasi wetu, lakini pia zinawapa mtaji wa
kisiasa maadui zetu.
Kuanzia
sasa tutegemee sana kuwasikia maCCM yakishangilia 'busara' za Mheshimiwa
Lowassa.
Masuala
ya ukiukwaji haki za binadamu, uvunjwaji wa Katiba na mengine mengi sasa
yatajibiwa kwa namna moja: Lowassa amemkubali Magufuli nyie wengine mnapiga
kelele za nini.
Huu
ni mtaji wa bure kwa Magufuli. Ukweli, ambao umesemwa sana humu, ni kwamba
amefeli karibu katika kila jambo.
Hata
hiyo reli anayosifiwa nayo na Lowassa bado ni ndoto tu: nani ajuaye itajengwa
kwa hela za nani???
Za
Wachina kama tulivyoambiwa mwanzoni; au za Waturuki kama tulivyoambiwa baadae;
au za Afrika Kusini kama alivyosema mwenyewe anaenda kumwomba Zuma???
Kama
chama hatujawahi kukataa mazungumzo na Rais au kiongozi mwingine yeyote wa
serikali.
Na
hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili
nchi yetu.
Lakini
ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla
ya mazungumzo hayo.
Na
baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa
hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja.
Katika
mazingira ya sasa, ambako viongozi na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani
kwa mapanga na hata kwa risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye na matendo
yake.
Katika
mazingira ya kesi nyingi za kutunga dhidi yetu, 'kazi nzuri' inayofanywa na
Magufuli ina maana gani hasa, kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.
Katika
mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa Rais
Magufuli, kutoa kauli kwamba 'anafanya kazi nzuri' ni 'kumtupia taulo' la
propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia Watanzania katika miaka
hii miwili.
Kwa
vyovyote vile, kitendo cha Mheshimiwa Lowassa sio cha kunyamaziwa au
kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.
TUNDU
LISSU(MB).
Top of Form
Kadhalika,
kada maarufu wa kike wa chama hicho, Hilda Newton nae alieleza masikitiko yake
kutokana na kauli za Lowassa.
Bila kumung'unya maneno leo Mh @edwardlowassatz kanikwaza mpaka nahisi kupasuka
Yani kabisa umefunga safar unaenda kuongea na adui tena mwenye roho ya Ukatili alaf unamsifia??
Nmeumia sana mpaka machozi yamenitoka, Lowassa katukosea sana yani nchi ipo kwenye mkwamo wa kisiasa yeye anaenda kumsifia adui!!..@tundulissutz kashambuliwa kwa risasi, Serikali ipo kimya hakuna cha uchunguzi wala nin yeye kapata wapi ujasir wa kumsifia adui ??
Kama
alivyotahadharisha Lissu, ni wazi kwamba CCM watakuwa wamepewa “silaha” mpya
katika “kumpamba” Magufuli na “kuwapenda” wapinzani, kwamba “hata Lowassa wenu
anamkubali Magufuli.” Na ni rahisi kwa CCM kuonekana wana mantiki katika hoja
hiyo, kwa kudai “kama mtu muhimu kabisa kwenye chama chenu (yaani Lowassa)
ambaye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Magufuli kwenye uchaguzi mkuu uliopita,
anamkubali mkuu huyo wa nchi, ninyi ni akina nani kumpinga?”
And guess what, Lowassa amewapatia CCM narrative muhimu sana: "hata @edwardlowassatz wenu anamkubali @MagufuliJP" and unless you missed your meds, you can't disagree with them.
Wakati
ni wazi kwamba uamuzi wa Lowassa kukutana na Magufuli, na kumwagia pongezi,
umezua “sintofahamu” huko Chadema, kuna masuala kadhaa ya muhimu yanayopaswa
kuangaliwa kwa makini kwa ajili ya mustakabali wa chama hicho.
Kwanza,
ni muhimu kwa viongozi na wanachama wa Chadema kutambua nafasi ya Lowassa katika
chama hicho. Wakati baadhi ya wachambuzi wa siasa – mie nikiwa mmoja wao –
wanaamini kuwa ujio wa Lowassa katika chama hicho ulikuwa na hasara zaidi
kuliko faida, jitihada zilizofanywa na chama hicho kumpigania mwanasiasa huyo
zimemjengea hadhi ambayo haipo kwa mwanasiasa mwingine yoyote ndani na nje ya
chama hicho.
Ikumbukwe
kuwa hadi wakati jina lake lilipokatwa na vikao vya CCM katika mchakato wa
kusaka mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho tawala, Lowassa alikuwa ndiye
mwanasiasa maarufu kuliko wote Tanzania. Yayumkinika kusema alikuwa mtu wa pili
kwa umaarufu baada ya marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Licha ya
kulazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu mwaka 2008 kutokana na kashfa ya Richmond,
Lowassa aliendelea kuwa mwanasiasa maarufu na mwenye nguvu kuliko yeyote yule
ndani ya CCM, hata zaidi ya Rais na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho wakati
huo, Jakaya Kikwete.
Na
japo kukatwa kwa jina la Lowassa huko CCM kulimpunguzia kidogo umaarufu wake
kwa siasa za Tanzania – ilikuwa kama miujiza kuona CCM ilikuwa na ujasiri wa
kukata jina la mwanasiasa huyo- alihamia Chadema akiwa na sapoti ya kutosha
kiasi japo si kubwa kama ilivyotarajiwa.
Japo
kuna “tuliopishana nae mlangoni” – kwa maana yeye alipoingia, sie tukatoka –
ujio wake ulipelekea kuwa mwanasiasa maarufu zaidi ya wote wa Upinzani. Na ndio
maana haikuwa vigumu kwake kupitishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.
Nimeeleza
kuwa baadhi yetu “tulipishana nae mlangoni” kwa sababu mie binafsi nilikuwa
naiunga mkono Chadema, si kama mwanachama bali ukweli kwamba kwa muda mrefu
nimekuwa nikijihusisha na harakati za mapambano dhidi ya ufisadi, na chama hicho
kilijitokeza kuwa championi wa mapambano hayo. Kwahiyo, “naturally” nilijikuita
nikikiunga mkono.
Hata
hivyo, ujio wa Lowassa katika chama hicho ulinikimbiza. Sababu kuu ni binafsi
zaidi, na nisingependa kuongelea hapa, lakini sababu nyingine ni kile
nilichotafsiri kama usaliti wa Chadema. Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2006, chama
hicho “kilimkalia kooni” Lowassa kumtuhumu kuwa ni fisadi, na ndicho
kilichofanya jitihada kubwa zilizopelekea mwanasiasa huyo kujiuzulu Uwaziri
Mkuu mwaka 2008.
Mmoja wa watu walionipa kiu ya uandishi asema "Lowassa anawaadhibu Mbowe,Lissu,nk kwa kumwita fisadi for 9 yrs." Mtu huyo ni Johnson Mbwambo
Sasa
bila hata kutumia jitihada kidogo tu za busara, chama kilichomwandama Lowassa
kuwa ni fisadi, kwa miaka 9 mfululizo, yaani 2006 hadi 2015, kilionekana kituko
kwa baadhi yetu tuliokuwa tukikiamini, kwa sababu, pamoja na mengine,
isingewezekana kutumia miezi mitatu (Julai 2015 Lowassa alipojiunga na chama
hicho hadi Oktoba wakati wa uchaguzi mkuu) kumsafisha vya kutosha.
Na
gharama ya ujio wa Lowassa ilikuwa kubwa. Moja kubwa zaidi ilikuwa lazima kwa
Chadema “kuitosa” turufu yake muhimu, ajenda ya vita dhidi ya ufisadi.
Ililazimika kufanya hivyo kwa sababu kuzungumzia ufisadi ilhali chama hicho
kimemkumbatia mwanasiasa kiliyemwita “baba wa ufisadi” kwa miaka 9 mfululizo
ingeonekana kioja.
Kadhalika,
kwa kumpokea Lowassa, Chadema ilikuwa haina jinsi ya kukwepa tuhuma kutoka CCM
kuwa chama hicho upinzani ni cha kifisadi kwa sababu ya kumkumbatia mwanasiasa
ambaye kilikuwa kikimuita fisadi. Jitihada za Chadema kujibu mashambulizi kuwa “kama
Lowassa ni fisadi mbona hajachukuliwa hatua,” zilikuwa hazina mashiko.
Lakini
jingine lililoipa jeuri CCM ni ukweli kwamba kwa chama hicho, Lowassa alikuwa
ni “makapi” sambamba na wanasiasa wengine waliomfuata huko Chadema. Hiyo
ilikipa chama hicho tawala “jeuri” ya namna flani. Na waliitumia vema kwenye kampeni,
kwamba “hawa jamaa si lolote si chochote. Yani wameshindwa hata kutafuta
mgombea wao wenyewe mpaka wakasubiri makapi kutoka kwetu ndo wakapata mgombea
urais.” Na pamoja na maneno hayo kuwa machungu, ndo ukweli ulivyokuwa.
Chadema
na UKAWA kwa ujumla walikuwa na takriban mwaka mzima wa kujipanga; kuafikiana
kuhusu mgombea urais kwa tiketi ya umoja huo, na kumnadi, huku wakitumia “advantage”
ya “vita vya wenyewe kwa wenyewe” kati ya zaidi ya makada 40 waliokuwa
wakichuana kuteuliwa na CCM.
Badala
yake, kumbe tayari kulikuwa na makubaliano ya siri kati ya uongozi wa baadhi ya
viongozi wa juu wa Chadema kwamba wasubiri kutangaza mgombea wao hadi baada ya
mchakato wa CCM kupata mgombea wake, ka maana ya “kumhifadhia nafasi Lowassa
endapo jina lake litakatwa huko CCM.”
Kabla
ya kwenda mbali na makala hii ningependa nishauri Chadema irejee suala hilo la
Lowassa kuandaliwa nafasi ya kuwania urais japo wakati huo alikuwa CCM. Hatua
stahili zinapaswa kuchuliwa dhidi ya wote waliohusika na mpango huo.
Na
ujio wa Lowassa ulipelekea Chadema kumpelekea mmoja wa magwiji wa siasa za
upinzani, Dokta Willbrord Slaa. Umahiri wa Dokta Slaa haukuwa tu katika
kuchukia ufisadi kwa dhati bali umahiri wake mkubwa katika kujenga hoja kisomi.
Kadhalika, alikuwa akiaminiwa na watu mbalimbali muhimu ndani ya serikali,
kiasi kwamba baadhi yao walihatarisha ajira zao kwa kumpatia mwanasiasa huyo
nyaraka muhimu zilizoiwezesha Chadema kuwa na ushahidi mbalimbali katika vita
yake dhidi ya ufisadi.
Na
kuonyesha kuwa alikuwa na msimamo imara, Dokta Slaa aliamua kujiweka kando katika
uongozi kupinga Lowassa kupewa ugombea urais wa UKAWA. Lakini jambo la
kusikitisha mno, kiongozi huyo aliyekifanyia mengi chama hicho alidhalilishwa
na kutukanwa kupita kiasi.
Na
“akina sie” tulishindwa kustahimili ujio wa Lowassa, na kwa vile kwa baadhi
yetu ilikuwa muhimu kumzuwia asiingie Ikulu, na hivyo kulazimika kumpigia
kampeni mpinzani wake yaani Magufuli, tulitukanwa kila aina ya matusi. Sijui
watu hawa waliojitoa ufahamu wataweka wapi sura zao pindi Lowassa “akirejea
nyumbani” CCM.
Wakati
anajiweka kando na uongozi wa Chadema, Dokta Slaa alikitahadharisha chama hicho
kuwa ili kuleta mabadiliko ya kweli (badala ya hayo “ya kisanii” aliyokuwa
akiyanadi Lowassa) chama hicho kinahitaji mkakati makini utakaoongozwa na watu
makini. Na kwa hakika, tangu wakati huo, Chadema imekuwa kama kundi la
wanaharakati wa kudandia hoja kuliko chama cha siasa chenye ajenda ya
kueleweka. Uamuzi wa kuitelekeza ajenda ya vita dhidi ya ufisadi ulipelekea chama
hicho kutokuwa na ajenda moja ya maana, huku CCM “wakipora” kiurahisi ajenda ya
vita dhidi ya ufisadi.
Je
mustakabali wa Chadema ukoje? Japo sio rahisi sana kubashiri kwa uhakika kuhusu
hatma ya chama hicho, binafsi – kwa kutumia uzoefu wangu na uelewa wa kutosha
wa siasa za Tanzania, sambamba na kuwa na fursa ya kufahamu “yanayojiri nyuma
ya pazia” la siasa za nchi yetu – ninadhani kuwa kuna uwezekano mkubwa tu kwa
Lowassa kurudi CCM kama sio kuachana kabisa na siasa.
Kwanini
Lowassa anaweza kurudi CCM? Kuna sababu kuu mbili. Moja ni dalili za wazi kuwa
ndoto zake za urais kupitia chama hicho ni kama zimeyeyuka. Umaarufu wake
umegubikwa na kuibuka na kuimarika kwa umaarufu wa Lissu. Ni dhahiri kwamba
ikipigwa kura ya maoni kuwa nani kati ya Lowassa na Lissu awe mgombea urais kwa
tiketi ya Chadema mwaka 2020, Lissu ataibuka mshindi. Na Lowassa anafahamu kuwa
hakuna njia ya mkato kwa yeye “kulazimisha” awe mgombea katika uchaguzi mkuu
huo ujao, licha ya ukweli kwamba alishatangaza kuwa atagombea.
Sababu
nyingine ni binafsi zaidi. Lowassa ni mmoja wa matajiri wakubwa nchini
Tanzania. Kama utajiri huo ulipatikana kihalali au kifisadi, si lengo la makala
hii kujiingiza katika mjadala huo. Lililo wazi ni ukweli kwamba licha ya kuwa
mwanasiasa, yeye pia ni mfanyabiashara. Na kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika,
serikali ya Magufuli imefanikiwa kutumia nyenzo yake muhimu dhidi ya wapinzani
ambao pia ni wafanyabiashara, KODI.
Inaelezwa
pia kwamba mali mbalimbali za mwanasiasa huyo zipo hatarini kutokana na uwepo
wake huko Upinzani. Inadaiwa kuwa hata jengo la Tanesco Ubungo ambalo serikali
imetangaza kulivunja, linamilikiwa na Lowassa, na tishio la kulivunja lilikuwa
kama kufikisha ujumbe kwake.
Katika
hili, Lowassa hatoonekana mtu wa ajabu akiamua kurudi CCM ili asibughudhiwe
kuhusu biashara na mali zake. Ni nani kati yetu anayeweza kujitoa mhanga kwa
ajili tu ya imani yake ya siasa? Si kama hawapo ila ni adimu mnooo! Na kibaya
zaidi, hata akiamua kung’ang’ania huko Chadema, hatma yake na ya chama hicho haieleweki
kwa sababu hadi muda huu – na hii ni licha ya zuwio la Magufuli dhidi ya vyama
vya upinzani kufanya shughuli zao za siasa – chama hicho kikuu cha upinzani “kipo
kipo” tu. Hakina ajenda moja ya kueleweka zaidi ya kudandia kila tukio
linalojiri.
Iwapo
Lowassa ataamua kubaki Chadema, hiyo itakuwa fursa mwafaka kwa chama hicho
kumpumzisha. Naamini kuwa wana-Chadema wakiweka kando ushabiki wa kisiasa,
wanafahamu fika kuwa mwanasiasa huyo hana nguvu, uwezo wala mvuto wa
kukabiliana na siasa hatari zinazoendelea muda huu huko nyumbani.
"Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, atangaza kurejea CCM. Asema anaridhishwa na uchapakazi wa Rais Magufuli"#FutureTweet#MarkThisTweet [Future Tweet ni tweet ya kufikirika japo yaweza kuwa kweli] pic.twitter.com/DiiKxtbwj3
Kwa upande mwingine, tukio la Lowassa kukutana na Magufuli Ikulu linaweza pia kuhusishwa na tamko la hivi karibuni la Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, ambaye kama Lowassa, alimmwagia sifa Magufuli.
Je kuna disconnect kati ya baadhi ya viongozi wakuu wa upinzani na wengi wa wafuasi wa vyama hivyo? pic.twitter.com/IkA9566Oop
Nimefanya uchambuzi kuhusu kauli za wanasiasa hao wawili hapa, lakini ninachoweza kugusia hapa ni haja ya kutambua kuwa wanasiasa hao bado wanatunzwa na serikali kutokana na nyadhifa walizowahi kushika huko nyuma. Haihitaji uelewa mkubwa kuhusu "siasa za kibabe" kuhisi kwamba huenda "malezi" wanayopewa na serikali yametumika kama "chambo" cha kuwavuta karibu na Magufuli. Kuhusu matatizo yanayoikabili Chadema muda huu,ukweli ni kwamba ni zaidi ya uwepo wa Lowassa ndani ya
chama hicho. Japo huu ni ukweli mchungu usioruhusiwa kabisa kusikika ndani ya
chama hicho, licha ya kazi nzuri ya kuifikisha Chadema ilipo leo, mwenyekiti wa
taifa Mbowe anapaswa kutoa fursa kwa wana-Chadema wengine kusukuma gurudumu la
chama hicho. Na hatua hiyo wala haihusiani na mchango wake mkubwa wa kumleta
Lowassa ndani ya chama hicho na “kumpa” ugombea urais wa UKAWA.
Kirefu
cha Chadema ni Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo
ambayo inaruhusu mwenyekiti mmoja kuwa madarakani milele? What if “uenyekiti wa
milele” ni miongoni mwa vikwazo kwa maendeleo ya chama hicho?
Lakini
hata kama “muda wa Mbowe kutoka madarakani haujafika,” busara tu inapaswa
kumfahamisha kiongozi huyo kuwa ni vema kuzingatia busara za akina Nyerere
waliojing’atua wakiwa bado wanahitajika. Sipendi kubashiri hili, lakini laiti
Mbowe asipohamasisha mageuzi kwenye medani ya uongozi wa chama hicho, haitokuwa
jambo la ajabu akiishia kung’olewa kwa nguvu.
Na
kwa bahati mbaya kwake, hili “songombingo” alilolianzisha Lowassa jana linaweza
kuwa kama mnyororo mrefu ambao mahala flani yupo Mbowe. Ndiye aliyemkaribisha
Lowassa.
Moja
ya mapungufu makubwa mno yanayoitafuna Chadema muda huu ni pamoja na kulipuuza
kundi muhimu linalokisaidia mno chama hicho, lundo la vijana wanaoshinda na
kukesha katika mitandao ya kijamii wakijaribu kukinadi chama hicho angalau kwa
kuikemea serikali ya Magufuli au CCM kwa ujumla.
Laiti
chama hicho kingekuwa na ajenda ya kueleweka, basi jeshi hili la vijana
lingekuwa nyenzo muhimu mno. Ni rahisi kuwalaumu vijana hawa kuwa “kazi yao
kubwa ni kudandia hoja tu,” lakini ukweli ni kwamba chama chao hakiwapatii
ajenda ya/za kueleweka. Kibaya zaidi, hata pale wanapojaribu kutengeneza ajenda
wao wenyewe – kwa mfano jitihada za kumsaka Ben Saanane – hawapati sapoti ya
kutosha kutoka uongozi wa juu wa chama hicho.
Ni
hivi, wengi wa hawa vijana wanahatarisha maisha yao kwa kuwa tu “upande usiotakiwa”
na serikali ya Magufuli. Hawategemei malipo yoyote zaidi ya kuamini kuwa siku
moja wanaweza kukiingiza chama chao madarakani. Hakuna jitihada za makusudi za
uongozi wa juu wa chama hicho kuwa karibu na kundi hili muhimu.
Ukiwa
UVCCM una uhakika wa angalau “kuhongwa na Bashite” au kualikwa kwenye “mnuso”
sehemu flani. Lakini ukiwa kijana wa upinzani, “zawadi” kubwa yaweza kuwa
kusumbuliwa na vyombo vya dola na kuishi maisha ya wasiwasi. Kwahiyo vijana wa
upinzani wana kila sababu ya kuichukia siasa, kwa sababu inahatarisha maisha
yao, lakini mapenzi yao katika imani ya chama inawalazimisha kung’ang’ania
hivyo hivyo.
Niionye
Chadema kuwa katika zama hizi za “ununuzi wa binadamu kama zama za utumwa,”
chama hicho kisishangae pindi wengi wa vijana hawa watakapoamua kubwaga
manyanga na kukubali “kununuliwa.” Kwanini waendelee kuhatarisha maisha yao
ilhali uongozi wa juu wa chama hicho hauna muda nao?
Akina
Hilda Newton, Ben Malisa, Bob Wangwe, Ndehani Mwenda, Noel Shao, Gift Nanyaro
ni miongoni mwa vijana wanaofanya kazi kubwa kwa ajili ya Chadema, bila ya
matarajio ya malipo au fadhila flani, zaidi ya kuhatarisha maisha yao. Kama
ilivyo kawaida ya mwanadamu yeyote yule, inaweza kufika mahala mtu akarudi
nyuma na kujiuliza, “is it worth it?” Na japo sitarajii kuona makada hao vijana
wakiamua kuipa kisogo Chadema, lakini sintoshangaa baadhi yao wakiamua kuipa
kisogo siasa, hasa kama tasnia hiyo itaendelea kuwa “yenye manufaa kwa genge
flani tu.”
Nihitimishe
makala hii kwa kukuhamasisha msomaji kujipatia nakala yako ya kitabu changu kipya
cha kielektroniki kinachochambua kwa kina miaka miwili ya utawala wa Magufuli.
Baadhi
ya niliyaoyazungumzia kwenye makala hii yamezungumwa kwa kirefu katika kitabu
hicho ambacho hakielemei upande wowote. Kitabu hicho kwa sasa kinasubiri
uzinduzi rasmi utakaokiwezesha kununulika kwa “mobile money” kama m-pesa,
tigopesa,nk. Nitawataarifu. Ila kwa wasiohitaji kusubiri, waweza kukinunua HAPA