tag:blogger.com,1999:blog-26327165.post5821077547270991829..comments2023-12-12T11:46:45.188+00:00Comments on Kulikoni Ughaibuni : TALIBAN NDANI YA KENYA!!!?Evarist Chahalihttp://www.blogger.com/profile/08220429042701710191noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-26327165.post-8506586572070161512008-01-08T19:48:00.000+00:002008-01-08T19:48:00.000+00:00Awari ya yote napenda kuchukua nafasi hii kukupong...Awari ya yote napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe binafsi kama Chahali kwa hatua nzuri uliyofikia kimasomo.Pili kuipongeza blog hii ambayo wewe binafsi unajalibu kutoa mawazo yako binafsi katika nyanja za siasa. Mimi kama mwana Kilombero mwezako niliyopo hapo Urusi mara kwa mara hupenda kutembelea katika blog hii, ingwa mimi siko kwenye fani ya mambo ya siasa lakini huwa napenda kufaham mambo yanayo zunguka jamii katika nyanja tofauti ikiwemo siasa.Katika blog hii huwa nasoma chambuzi zako nyingi ikiwa ni pamoja na habari za OBAMA na uchaguzi wa majirani zetu wa kenya.Kwa leo ningependa kuchangia kuhusu uchaguzi wa majirani zetu wa kenya, ni kweli kabisa kwamba wakenya wengi wamepoteza maisha katika vurugu zilizodumu takribani wiki moja na nusu hivi, na sababu kubwa ni kutokukubariana na matekeo ya uchaguzi hususa wa kiti cha Uraisi katika pande mbili zinazo pingana. Na tukumbuke kwamba Walao na Wakikuyu ni makabila makubwa yanayopingana nchini kenya, pamoja na hayo yote makabira hayo huwa hayaonyeshi upendo miongoni mwao, tofauti na Tanzania ambakowatu wa makabira tofauti hujichanganya katika shughuri mbalimbali za kijamii,Kisiasa,Utamaduni na michezo na hata kiuchum,kwa hiyo mauwaji hayo ni chuki zilizomo katika makabira hayo na uchaguzi huo umetumika kama kigezo tu cha kutimiza matakwa hayo.Na mimi siko mbali na wewe katika kurani mauwaji hayo.Hashimhttps://www.blogger.com/profile/05509899294741892689noreply@blogger.com