tag:blogger.com,1999:blog-26327165.post6763686667003228842..comments2023-12-12T11:46:45.188+00:00Comments on Kulikoni Ughaibuni : MAZINGAOMBWE YA RICHMOND YANAKIFUEvarist Chahalihttp://www.blogger.com/profile/08220429042701710191noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-26327165.post-76566331886908404112009-10-22T19:24:27.827+01:002009-10-22T19:24:27.827+01:00Ndugu Evarist,
Mimi nimesoma katikati ya mstari. N...Ndugu Evarist,
Mimi nimesoma katikati ya mstari. Nakubaliana na wewe kwamba hii skandali kufikia mwisho wake, ni mpaka watu waamue kujilipua, kuamua liwalo na liwe almuradi mafisadi wasiachwe wakitamba watakavyo. Mambo haya yanaudhi na kukera isipokuwa kama tutakuwa tunaongozwa na ushabiki wa kijinga chama fulani kisiojulikana kinapindua nini mpaka leo.
Ukifuatilia kwa nidhamu suala hili, kuna maswali mengi ya kuudhi yanajitokeza. Kwanza kabisa mtu unajiuliza, ni kwa nini serikali inaonekana kunywea linapokuja suala la kuwashughulikia hawa mabwana ambao Bunge lilikubaliana kwa azimio rasmi kwamba wawajibishwe? Kwa nini inakuwa ngumu? Ni kwa nini serikali katika Bunge lililopita iliamua kutugeuzia kibao kwa kujaribu kuwasafisha wahalifu hawa? Hivi hii haimaanishi kwamba serikali nayo ina maslahi fuylani fulani katika uhalifu huu? Nasema hivyo kwa sababu haiingii kabisa akilini kwamba watu ambao IMETHIBITIKA kuwa wana hatia na kuitambua hatia hiyo kumefanyika kupitia vyombo vilivyopewa dhamana kama Bunge, bado wanaendelea kubembelezwa mpaka leo.
Inachekesha unaposikia eti leo wanapewa likizo ya kustaafu kwa raha zao kwa namna ambayo inaleta picha kwamba hilo limekuwa kwa mujibu wa mabadiliko ya kawaida ya ofisi.
Halafu kama hiyo haitoshi na kwa kwa kweli, kinacholeta wasiwasi zaidi, kila mpiga kelele anapojaribu kupaza sauti kuhusu ujambazi huu, maadamu anaonekana kuwa na nia ya kweli kweli kuwasulubishwa wahalifu hawa, wakubwa (kwa maana hasa ya ukubwa) wanafanya jitihada za kuwanyamazisha kwa mlango wa nyuma. Why? Kuna nini hapa tusichokijua?
Mimi nisingependa kuamini kwamba skandali hii iliasisiwa na wenye madaraka makubwa serikalini waliyoyapewa kama dhamana na wananchi ambao leo wanawadharau. Sipendi kuamini hivyo maana ikiwa hivyo, inatisha.
(Nashindwa kuelewa kwa nini watu wa ile ofisi ya magogoni mara zote wamejitokeza kukanusha habari ambazo hakuna aliayeziulizia. Nasisitiza sijui.)
Nashindwa kuelewa pia kwa nini wananchi hatuandamani tuambiwe nani hasa ni jambazi wa Richmond. Inaniwia vigumu kuelewa ni sababu ipi hasa inayotufumba macho kiasi cha kuwaacha watawala watuchezee kwa kiasi hiki.

Kama watu hawa waliotajwa na kamati teule ya Bunge hawana hatia (na ndivyo inavyotaka kuonekana kwa namna ambavyo tamthlia inavyoendelea) basi tuambiwe nani hasa yuko nyuma ya Richmond ambaye tunamwogopa sana kiasi kwamba akijulikana jua halitachomoza alfajiri ya pili yake? Maana kwa jinsi mwenendo wa mambo ulivyo, mtu anaweza kushawishika kwmaba siku mambo yakijulikana kwa ukamilifu wake, tunaweza kufa kwa kihoro.

Nashauri jambo moja hapa. Kwa kuwa chama chenye serikali kimeendelea kutuzunguka mchana kweupe, kwa kuwakumbatia wahalifu wa kila skandali la ufisadi tulilowahi kulisikia; na kwa kuwa chama hiki kimeonekana kinajitahidi kuwatisha wawakilishi wetu wanaotusemea kuhusu ujambazi huu wa kuchefua wasiokubaliana na mwenendo wa chama chao; na kwa kuwa chama hiki ndicho kilichounda serikali ambayo haitaki kabisa kushughulikia hata vivuli vya mafisadi ambao inawakumbatia kwa lazima; na kwa kuwa uwezo tuliobaki nao ni kuwakataa kupitia sanduku la kura; basi watanzania tuna kila sababu ya kukipindua chama hiki kilichochoka na kulewa madaraka kwa njia za kistaarabu za kupiga kura zetu kwa bidii ifikapo 2010 (kama haitatokea basi uchaguzi ukawahishwa kabla.)Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.com