3 Oct 2008

CLICK HERE to see how the votes were cast

Kuna nyakati huwa napatwa na hisia kwamba baadhi ya makampuni makubwa huko nyumbani (hasa ya kigeni) yanachuma faida kubwa kupita kiasi to an extent of kukurupuka na sherehe zisizo na vichwa wala miguu.Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima,kampuni ya Multichoice leo itafanya sherehe za kumpongeza mshiriki wa kwanza kutolewa kwenye Big Brother ya Afrika,Latoya Lyakurwa wa Tanzania.Hivi anapongezwa kwa upuuzi aliofanya ndani ya jumba hilo au kwa kuwa wa kwanza kutolewa katika mashindano hayo?Kama jibu ni ndio kwa swali la kwanza basi huu ni ufisadi wa kimaadili (moral corruption) na kama jibu ni ndio kwa swali la pili basi yayumkinika kuamini kwamba Multichoice wana fedha za kuchezea (pengine kutokana na faida kubwa wanayopata) kupongeza a loser badala ya winner kama ilivyozoeleka.Yaani hata kushindwa nako kunaambatana na sherehe ya pongezi!?


Mdahalo kati ya running mates wa vyama vya Democrat na Republican,Joe Biden na Sarah Palin,respectively,umemalizika hivi punde.Uchambuzi wa haraka haraka unaonyesha kuwa Palin amejitahidi kufanya vizuri kuliko ilivyotarajiwa.Matarajio kwamba Palin angefanya vibaya yalitokana na performances zake za hivi karibuni katika mahojiano (ya nadra) na wanahabari.Hofu zaidi ilikuwa ni kweli u-kilaza wake kwenye mambo mbalimbali.Kwa upande wa Biden,huku akitarajiwa kuutumia vizuri uzoefu wake wa muda mrefu kwenye ulingo wa siasa,hofu zaidi ilikuwa ni katika tabia yake ya "kusema ovyo" na kuwa gaffe-prone.Hata hivyo,uchambuzi wa awali unaonyesha kuwa Biden amefanya vizuri sana katika mdahalo huo,kiasi cha mchambuzi mmoja kudai kwamba it was his best ever performance.

Kwa upande mwingine,Palin ameonekana kama amethibitisha kwamba McCain hakufanya kosa kumchagua yeye kuwa running mate wake lakini ameshindwa kum-portray McCain kama mtu anayefaa zaidi  kuwa rais kuliko Barack Obama.Lakini Biden,pengine kwa kuhofia kuonekana kuwa ni sexist dhidi ya Palin,ametumia muda mwingi kuonyesha kwanini Obama anafaa zaidi kuwa rais kuliko McCain na wakati huohuo kuonyesha kuwa tiketi ya McCain-Palin ni mwendelezo mwingine wa miaka minane ya George W Bush.

Kiujumla,na kama ilivyotarajiwa na wengi,Biden ameonekana kuwa msindi katika mdahalo huo japo hilo haliwezi kukubalika among the Republicans.Pia matokeo ya awali ya kura kadhaa za maoni baada ya mjadala huo zinaonyesha ushindi mzuri kwa Biden hasa miongoni mwa undecided voters.


Kama kawaida yake,gazeti la Raia Mwema katika toleo la wiki hii limesheheni habari na makala mbalimbali zilizoandikwa kwa umakini na uchambuzi wa hali ya juu.BONYEZA HAPA kusoma gazeti hilo.

1 Oct 2008

Grandfather, 71, told he's pregnant

A 71-year-old grandfather treated in a US hospital was informed that he was suffering abdominal pains because he was pregnant.

John Grady Pippen was given a bulletin, saying: "Based on your visit today, we know you are pregnant."

The staff at Curry General Hospital in Gold Beach, Oregon, gave the retired mechanic and logger the happy news this month, along with some pain pills. Hospital administrator William McMillan said an errant keystroke caused the hospital's computer to spit out the wrong discharge instructions for the grandfather.

SOURCE: MSN NEWS




Muhidini Issa Michuzi (left) and Haki Hakingowi
Photo courtesy of MICHUZI

30 Sept 2008

Je wajua kuwa licha ya kuwa gaidi nambari moja duniani,Osama bin Laden pia ni mshairi?Well,mie nilikuwa sifahamu kuhusu hilo hadi niliposoma habari kwamba kuna mjadala unaoendelea kuhusu la jarida la Language and Communication kama lichapishe mashairi ya gaidi huyo au la.Watetezi wa hoja ya kuchapisha mashairi ya Osama wanadai kuwa kwa kuyachapisha inaweza kusaidia kumjua kwa undani zaidi gaidi huyo,huku wapinzani wakidai kwamba kuchapisha mashairi hayo kutampatia forum nyingine zaidi ya kujitangaza.


























Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.