7 Aug 2009



Kwa mfumo wa tarehe za "kwetu" tunaanza na tarehe kisha mwezi,tofauti na wenzetu wa kwa Obama ambao wanaanza na mwenzi kisha tarehe.Yaani,kwa hapa,na kama ilivyo huko nyumbani TZ,ni tarehe 07/08/09 japo kwa wenzetu wa US itaandikwa 08/07/09.Basi,leo mchana kulikuwa na tukio adimu katika uhai wa wengi.Kama inavyoonekana pichani juu,kuna muda saa na kaelnda ilisomeka 1-2-3-4-5-6-7-8-9,yaani saa 12 na dk 34 na sekunde 56 tarehe 7 mwezi wa nane mwaka 2009 (12:34:56 7/8/9).Ulikumbuka kuhusu tukio hili?

MHAMASISHA VITA DHIDI YA MAFUA YA NGURUWE NAYE AAMBUKIZWA....


Na the funny side ya "maadhimisho" hayo ni habari hapa Uingereza kwamba jamaa aliyetumika katika tangazo la "Wizara" ya Afya katika runinga kuhamasisha jamii dhidi ya mafua ya nguruwe (swine flu) nae ameambukizwa ugonjwa huo.Msanii Davidi McCusker (pichani juu).Hata hivyo,lililo dhahiri ni kwamba maambukizo hayo hayana mahusiano na ushiriki wa msaanii huyo David McCusker katika tangazo hilo.

2 comments:

  1. Wamarekani wanapenda kufanya mambo kivyaovyao. Pamoja na hilo la tarehe, mengine ni pamoja na kukataa kutumia metric system katika vipimo vyao (hapa tunatumia paundi, yadi, maili n.k.), tofauti ya vipimo vya umeme, mfumo wa televisheni tofauti, "football" yao inachezwa kwa kutumia mikono, kuendeshea magari upande wa kushoto mwa barabara na hata jinsi tu ya kuwasha umeme unapoingia chumbani hapa ni kinyume. Inaonekana ni kama vile walikuwa wanatafuta njia za kuwa tofauti na watu wengine.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.