EVARIST CHAHALI
Mimi ni mtoto wa tano katika familia ya Mzee Philemon Chahali na mkewe marehemu Adelina Mapango.Ninaishi mjini Aberdeen,Scotland,nchini Uingereza ambako ninasomea Udaktrari wa Falsafa katika Siasa za Kimataifa,hususan kuhusu Afrika.Pia nafanya utafiti kuhusu Uislam na Harakati za vikundi vya Kiislam nchini Tanzania.Nilipata Shahada ya Kwanza katika Elimu ya Jamii pale Mlimani (UDSM),kabla ya Kupata Shahada ya Uzamili katika Siasa na Uhusiano wa Kimataifa hapa Aberdeen,na baadaye Shahada ya Uzamili wa Utafiti (Master of Research-MRes) katika Utafiti wa Siasa (Political Research) hapahapa Aberdeen.