Showing posts with label Intelijensia. Show all posts
Showing posts with label Intelijensia. Show all posts

23 Jul 2016

Munich-locator-600px
Ujerumani imekumbwa na janga jingine baada ya lile la siku nne ambapo kijana mmoja, mhamiaji kutoka Afghanistan, aliwashambulia abiria kwenye treni kwa kutumia shoka na kujeruhi watu wanne. 

Kijana huyo, Riaz Khan Ahmadzai (au Muhammad Riyad, kwa jina jingine), aliyekuwa na umri wa miaka 17, na aliyewasili Ujerumani mwaka jana kama mtoto anayesaka ukimbizi, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Katika tukio lililotokea jana, watu 10 wameuawa hadi wakati ninaandika makala hii na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya shambulio la risasi katika mgawaha wa McDonald kwenye kitongoji cha biashara katika jiji la Munich.
Awali, ilikuwa haifahamiki idadi kamili ya waliofanya shambulio hilo japo taarifa za awali zilitaja wahusika kuwa watatu. Licha ya shambulio hilo kwenye mgahawa huo ulio kwenye duka kubwa (mall), ilidaiwa kuwa milio ya risasi ilisikika pia maeneo mengine ya Munich.
Kulikuwa kuna theories tatu - mbili zenye uzito na moja yenye uzito mdogo kiasi - kuhusu nani hasa alihusika na tukio hilo. Theories hizo ni kama ifuatavyo.

Theory ya kwanza: shambulio hilo ni kazi ya magaidi, sanasana ISIS

Imekuwa ni kawaida sasa kwa nchi za Magharibi kwamba kunapotokea tukio lolote la kigaidi, hisia za kwanza ni usual suspects, yaani kama sio ISIS basi ni Al-Qaeda. Haya ndio makundi mawili ya kigaidi yanayoziandama mno nchi za Magharibi. Na kwa sasa, ISIS ndio inaongoza kwa mfululizo wa mashambulizi ilhali Al-Qaeda 'imekuwa kimya' kitambo sasa.

Hisia kwamba wahusika katika shambulio hilo walikuwa ISIS (au Al-Qaeda) ni, kwanza, tukio la majuzi la huyo kijana aliyefanya shambuli kwa kutumia shoka ambalo nimelieleza mwanzoni mwa makala hii. 

Pili, ni ukweli kwamba ISIS imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuishambulia Ujerumani na nchi nyingine za Magharibi. Kama ilivyo kwa Uingereza, wataalamu wa usalama wa kimataifa wanaeleza kuwa shambulio la ISIS kwa Ujerumani sio suala la "iwapo litatokea" bali "lini litatokea." 

Tatu, ISIS walishangilia tukio hilo la Munich, katika akaunti yao ya Telegram, kama inavyoonyesha pichani chini
ISIS rejoice in Munich attack

Hata hivyo, theory hii kuwa wahusika ni ISIS ilikabiliwa na 'pungufu' hili: ilielezwa kuwa moja ya maiti hizo 9 ni ya mmoja wa wahusika wa tukio hilo. Hiyo ilikuwa na maana gani? Ni kwamba, magaidi wa ISIS na wenzao wenye mrengo kama wao, hupania kuuawa na sio kujiuwa. Wanaamini kuwa kwa kuuawa - badala ya kujiuwa - wanakuwa wamejitoa mhanga kwa ajili ya imani yao. Kama sio kuuawa kwa kupigwa risasi basi kifo kitokane na kujilipua kwa bomu la kujitoa mhanga.

Lakini kifo cha mtu huyo anayedhaniwa kuwa mmoja wa wahusika wa shambulio hilo hakikutokana na kupigwa risasi na polisi au yeye kujilipua. Sababu pekee ya kifo inaweza kuwa alijipiga risasi mwenyewe, mbinu ambayo sio chaguo la magaidi wa ISIS na wenzao.

Theory ya pili: Wahusika walikuwa kikundi cha wabaguzi wa rangi wenye msimamo mkali dhidi ya Waislam, wakimbizi na raia wa kigeni

Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka mitano ya shambulio kubwa la kigaidi lililofanyika huko Utoya, nchini Norway, Julai 22 mwaka 2011 ambapo mbaguzi wa rangi mwenye msimamo mkali, Anders Behring Breivik, aliwapiga risasi na kuwauwa watu 77.
Wachunguzi wa masuala ya usalama walieleza kuwa kulikuwa na uwezekano kwamba shambulio hilo la Munich lilifanywa na kikundi cha kibaguzi chenye mrengo mkali kama maadhimisho ya tukio hilo la Norway, na pengine kama kumwenzi Breivik ambaye ni 'shujaa' kwa vikundi vya wabaguzi wa rangi.
Kingine kilichoipa uzito theory hii ni ukweli kwamba mmoja wa wahusika wa shambulio hilo alisikika akisema kuwa yeye ni Mjerumani asilia, na akawatukana wahamiaji nchini humo. Wataalamu wa lafidhi walieleza kuwa sio rahisi kwa mtu asiye mzaliwa wa Ujerumani kuwa na lafidhi iliyotumiwa na mtu huyo.

Theory ya tatu, wahusika sio watatu bali mtu mmoja tu aliyekuwa anayesumbuliwa na matatizo ya akili

Katika kile kinachotafsiriwa kama unafiki, 'mzungu' akiuwa watu kadhaa, maelezo yatakuwa "mtu mwenye matatizo ya akili." Uthibitisho wa hivi karibuni ni maelezo kuhusu mtu aliyemuuwa mbunge Jo Cox wa hapa Uingereza hivi karibuni. Ilielezwa kuwa muuaji huyo "alikuwa na historia ya matatizo ya akili."
Laiti angekuwa Muislam au Mwarabu basi maelezo hapo yangeelemea zaidi kuhusu Uislam wake, na wabaguzi wasingekawia kudakia hoja kuwa dini hiyo ni tishio kwa ustawi wa mataifa ya Magharibi.

Ilielezwa kuwa mtu huyo niliyemwelezea katika theory ya pili, licha ya kudai yeye ni Mjerumani na kuwatukana wahamiaji, pia alieleza kuwa ni mgonjwa wa akili na yupo kwenye matibabu.

Taarifa rasmi ya polisi kuhusu mhusika

Baadaye, polisi wa Munich waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa uchunguzi wao umethibitisha kwamba aliyefanya shambulio hilo ni kijana mwenye umri wa miaka 18, Mjerumani mwenye asili ya Aljeria, na alihamia nchini humo miaka miwili iliyopita.

Kama taarifa hiyo ya polisi haina mapungufu, ukweli kwamba siku 4 zilizopita mhamiaji kutoka Afghanistan alifanya shambulio la kigaidi kwa kutumia shoka na kujeruhi watu wanne kabla ya kuuawa, na jana mhamiaji mwingine kutoka Iran, mwenye umri wa mwaka mmoja tu zaidi ya huyo wa majuzi, naye amefanyanya shambulizi na kuuwa watu 10 (hadi wakati naandika makala hii), chuki dhidi ya wageni inaweza kuongezeka maradufu.

Ikumbukwe kuwa Ujerumani imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wakambizi miongoni mwa nchi za Magharibi. Licha ya upinzani mkali, hususan kutoka kwa makundi ya kibaguzi yenye mrengo mkali, Kansela Angela Markel amekuwa mstari wa mbele sio tu kuhamasisha nchi za Magharibi zipokee wakimbizi, bali pia ameruhusu idadi kubwa kabisa ya wakimbizi kuingia na kuishi katika nchi hiyo.

Kama kuna 'nafuu' kidogo, basi ni hiyo asili yake ya Iran, nchi ambayo ni nadra kuzalisha magaidi. Pia ukweli kuwa alijiuawa mwenyewe inaweza kuendana na hiyo theory ya pili hapo juu kuwa magaidi wa ISIS na wenzao huwa hawajiuwi kwa kujipiga risasi, huuawa kwa kupigwa risasi au kujilipua wenyewe, na kwa kufanya hivyo huwa wamejitoa mhanga kwa ajili ya imani yao.

Hata hivyo, huo u-Iran wake unaweza kuwapa nguvu wabaguzi wa rangi kuendeleza upinzani wao dhidi ya serikali ya Kansela Markel kuruhusu ujio wa wakimbizi nchini humo, ambao wanatizamwa kama 'magaidi watarajiwa.'

Endelea kutembelea blogu hii kwa uchambuzi wa kina wa mada mbalimbali kama hii inayohusu masuala ya intelijensia, na nyinginezo.21 Jul 2016


Julai 15 mwaka huu, serikali ya Uturuki ilinusurika kupinduliwa katika jaribio la mapinduzi liliyodumu kwa chini ya masaa 12. Tayari watu zaidi ya 60,000 aidha wamekamatwa, wamesimamishwa au wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusiana na jaribio hilo lililofeli.

Jaribio la mapinduzi lilitokeje?

Awali daraja kuu katika mkondo wa Bosphorous liliwekewa vizuizi na kundi la wanajeshi wakitumia vifaru, na wakati huohuo ndege za kivita zilikuwa zikiruka katika anga la mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara, huku milio ya bunduki ikisikika sehemu mbalimbali.

Baadaye, Waziri Mkuu Binali Yildrim, alitangaza kwamba kulikuwa na jaribio linaloendelea la kuipindua serikali.

Muda mfupi baadaye, kikundi cha wanajeshi kilitangaza kupitia radio ya taifa kuwa jeshi limechukua madaraka kutoka kwa Rais Recep Tayyip Erdogan ili kulinda demokrasia.

Kisha likafuatia tangazo la hali ya hatari (curfew), sheria za kijeshi (marshall law) na maandalizi ya katiba mpya.

Rais Erdogan ambaye alikuwa likizoni alifanikiwa kuwasihi wananchi waingie mtaani kupinga mapinduzi hayo. Alitoa wito huo kwa kutumia app ya Facetime ya iPhone na kuonyeshwa live kama inavyoonekana pichani chini.
Katika usiku huo, vituo vya televisheni vilivamiwa na wanajeshi, milipuko kadhaa ilisikika sehemu mbalimbali za Ankara na Istanbul, abaadhi ya waandamaji walishambuliwa na wanajeshi na kuuawa au kujeruhiwa, jengo la bunge na ikulu zilishambuliwa, helikopta ya jeshi ilitunguliwa, na mnadhimu wa jeshi kuchukuliwa mateka.


Jaribio la mapinduzi liliishaje?

Ili jaribio hilo la mapinduzi lifanikiwe, wahusika walihitaji sapoti ya sehemu kubwa zaidi ya jeshi badala ya kikundi kidogo tu, na sapoti ya wananchi mtaani. Yote mawili hayakutokea. Kana kwamba hiyo haikutosha, vyama vya upinzani navyo vilijitokeza kulaani jaribio hilo.

Kufikia Jumamosi asubuhi -  chini ya masaa 12 baada ya tangazo la mapinduzi - baadhi ya wanajeshi walioshiriki katika jaribio hilo walianza kujisalimisha.

Soldiers involved in the coup surrender on the bridge over the Bosphorus in Istanbul (16 July)Kadhalika, polisi walifanikiwa kurejesha sehemu mbalimbali muhimu mikononi mwa dola kutoka kwa waasi. Kufikia Jumamosi mchana, mitaa ilikuwa imesheheni wananchi wakilaani jaribio hilo la mapinduzi na kuunga mkono serikali ya Erdogan.


Kwanini jaribio hili la mapinduzi lilifeli?

Kwanza, jaribio hilo halikuwa na sapoti ya kutosha ndani ya jeshi la nchi hiyo. Kilichoonekana ni kikundi kidogo tu cha wanajeshi kilichojumisha wanajeshi wapya, pasipo uwepo wa viongozi waandamizi wa jeshi la nchi hiyo.

Pili, jaribio hilo halikuwa na spaoti ya wananchi. Mara baada ya Rais Erdogan kuwataka wananchi waingie mtaani kupambana na jaribio hilo, ikageuka kuwa mapambano kati ya wanajeshi na wananchi, kitu ambacho kwa vyovyote kingeathiri 'uhalali' wa mapinduzi hayo.

Tatu, wahusika wa jaribio hilo la mapinduzi kushindwa kudhibiti njia zote za mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa serikali na wananchi, kwa mfano vituo vya televisheni na redio. Mwelekeo wa jaribio hilo la mapinduzi ulibadilika kwa kiasi kikubwa baada ya Rais Erdogan kuonekana kwenye kituo kimoja cha televisheni akiwataka wananchi waingie mtaani.

Nne, Uturuki ni taifa lenye asilimia kubwa ya watu wenye kipato cha kati na cha juu. Ni vigumu sana kwa taifa lenye wananchi wa aina hii kuunga mkono mapinduzi. Ni rahisi kwa mapinduzi kuungwa mkono katika nchi masikini ambapo mara nyingi 'chuki' dhidi ya serikali huwa kubwa.

Jaribio hilo la mapinduzi lilionekana kufeli bayana baada ya Rais Erdogan kurejea Instanbul na kuhutubia katika uwanja wa ndege wa Ataturk.

Arriving at Ataturk airport in Istanbul, President Erdogan was greeted by hundreds of supporters


Hali ikoje sasa?

Idadi halisi ya waliokamatwa, kusimamishwa kazi au kutimuliwa kazi na hatua nyingine zilizochukuliwa ni kama ifuatavyo

 • Watumishi 300 wa Wizara ya madini wametimuliwa.
 • Watumishi 184 wa Wizara ya Forodha wametimuliwa.
 • Waandamizi wanane wa Bunge wameondolewa.
 • Waturuki wote wanapaswa kuwa na nyaraka za ziada wanapofanya safari nje ya nchi.
 • Watumishi 86 wa taasisi ya udhibiti na usimamizi wa mabenki wametimuliwa.
 • Watumishi 51 wa Soko la Hisa wametimuliwa.
 • Majaji 140 wa Mahakama Kuu wametumiwa hati za kukamatwa.
 • Watumishi 15,200 wa Wizara ya Elimu wametimuliwa.
 • Vyombo vya habari 24 vimefutiwa hati za usajili.
 • Watu 429 wa taasisi ya umma ya masuala ya dini (Diyanet) wameondolewa.
 • Walimu binafsi 21,000 wamefutiwa leseni zao.
 • Watumishi 393 w Wizara ya Familia na Sera za Jamii wametimuliwa.
 • Watumishi 257 katika ofisi ya Waziri Mkuu wametimuliwa.
 • Wakuu (deans) 1577 wa vyuo vikuu wametakiwa kujiuzulu.
 • Magavana 33 wametimuliwa.
 •  Watumishi 9,000 wa Wizara ya Mambo ya Ndani wametimuliwa.
 • Maafisa Usalama wa Taifa 180 wamesimamishwa kazi
 • Majaji 2,745wametimuliwa.
 • Watumishi wa umma milioni tatu wamezuwia kwenda likizo.
 • Mjadala kuhusu kurejeshwa kwa hukumu ya kifo umeanza, na Rais Erdogan ametanabaisha kuwa pindi bunge likiridhia kurejeshwa kwa hukumu hiyo basi wote waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi watahukumiwa kifo.
 • Maafisa 1,500 wa Wizara ya Fedha wametimuliwa.
 • Majenerali na maadmirali 85 ni miongoni mwa maelfu ya wanajeshi waliokwishakamatwa. Pia zaidi ya polisi 8,000 wamekamatwa, wametimuliwa au wamesismamishwa kazi.
Mashushushu wa Uturuki walikuwa wapi wakati mapinduzi hayo ynaandaliwa na hadi yakakaribia kufanikiwa?

Makala hii inahusu hasa swali hilo hapo juu, kwa moja ya kazi kuu za Idara ya Usalama ya taifa lolote lile ni kutambua, kuzuwia na kudhibiti matishio ya usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na mapinduzi. Sasa wakati serikali ya Uturuki ikionekana kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi mbalimbali wa umma ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwasimamisha kazi na kuwatimua, ni idadi ndogo tu ya maafisa usalama wa taifa waliochukuliwa hatua (angalia juu nilipoandika kwa maandishi mekundu).

Lakini swali kubwa zaidi ni kwamba je Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hiyo, MIT, haikufahamu kuhusu mipango ya kufanyika kwa mapinduzi hayo, na kwanini?

Turudi nyuma kidogo. Oktoba mwaka jana, mhadhiri wa chuo kikuu cha Haifa , Israel, Norman Bailey, alieleza kwa uhakika kuwa jeshi la Uturuki linaweza kuchukua madaraka ya nchi hiyo iwapo litaona nchi inaelekea kusikofaa.

Kadhalika, Machi mwaka huu, wachunguzi wa masuala ya usalama wa Russia walionya kuwa jeshi la Uturuki lilikuwa likijiimarisha kisiasa, na hivyo kujenga msingi wa mapinduzi.

Baadaye mwezi huohuo, Michael Rubin wa taasisi ya American Enterprise, aliuliza "je Uturuki itakumbwa na mapinduzi?" na akajibu kwamba "isiwe jambo la kushangaza iwapo jeshi la Uturuki litajaribu kumng'oa (Rais) Erdogan na kuwatupa jela watu wake wa karibu."

Machi 30, jarida linaloheshimika la Foreign Affairs lilichapisha makala ya Gonul Tol, Mkurugenzi mwanzilishi wa Taasisi ya Mashariki ya Kati, kituo cha stadi za Uturuki, alieleza kuwa nchi hiyo ilikuwa ikikabiliwa na mapinduzi.

Kadhalika, mwanzoni mwa mwezi huu, Joseph Fitsanakis wa tovuti ya IntelNews alizungumzia kuhusu hali tete iliyokuwa ikiikabili Uturuki na kutanabaisha kuwa hakuna nchi katika eneo hilo ambayo ilikuwa 'haijatulia' kama Uturuki.

Pia, wachambuzi wa taarifa za kiusalama wa Marekani walikuwa wakihofia kitambo kuhusu hali ya usalama nchini Uturuki. Swali lilibaki kuwa lini kungetoa jaribio la mapinduzi na lingeongozwa na nani.

Sasa, kama wataalamu hao mbalimbali wa masuala ya usalama waliokuwa wakitegemea 'vyanzo vya wazi vya taarifa za kishushushu' (open sources) waliweza kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa jaribio hilo la mapinduzi, inatarajiwa kuwa mashushushu wa Uturuki pia walikuwa na tahadhari hiyo.

Kwa kuangalia 'sintofahamu' iliyoikumba serikali ya Rais Erdogan wakati wa jaribio hilo la mapinduzi, yayumkinika kuhisi kuwa idara ya ushushushu ya nchi hiyo nayo ilikuwa katika 'sintofahamu' pia. 

Na kuthibitisha kuwa taasisi hiyo haikuwa imejipanga vizuri, asuhuhi ya Julai 16 makao makuu yake yalishambuliwa na helikopta za jeshi pasipo upinzani wowote. 

Wakati serikali ikikabiliwa na jaribio la mapinduzi, mkuu wa idara ya ushushushu ya nchi hiyo, Hakan Fidan, alikuwa mafichoni.
Kuna sababu kuu tatu zinazoweza kueleza kwanini idara ya ushushushu ya nchi hiy, MIT, ilionekana kutokuwa na taarifa kuhusu jaribio hilo la mapinduzi na kushindwa kwake kulizuwia.

Kwanza, uwezo wa utendaji kazi wa taasisi hiyo ni duni, na kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikuzwa na vyombo habari kuliko hali halisi. Taasisi hiyo inaelezwa kuwa yenyeurasimu mkubwa, yenye kutumia mbinu za kale, in uhaba mkubwa katika mtandao wake wa upatikanaji taarifa za kiusalama, sambamba na mapungufu katika uwezo wake kwenye uchambuzi wa taarifa za kiusalama.


Pili, kuchanganya siasa na taaluma ya ushushushu. Awali, taasisi hiyo ilikuwa ikijitegemea na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia taaluma na utaalam wa ushushushu. Hata hivyo, tangu Erdogan aingie madarakani mwaka 2003, taasisi hiyo imekuwa kama chobo cha kisiasa cha AKP, chama tawala chenye mrengo wa kulia kidogo kidini kinachoongozwa na Erdogan.

Tatu, kwa takriban muongo mzima sasa, MIT imekuwa 'bize' zaidi na changamoto za matishio ya usalama kwa Uturuki kutoka nje, yaani tishio la kikundi cha kigaidi cha ISIS, harakati za uhuru za Wakurdi na wapiganaji wao wa PKK, kuibuka kwa taifa lisilo rasmi la Rajava huko Syria, na  hali tete ya usalama huko Iraki na Syria kwa ujumla. Changamoto hizo zimepeleka taasisi hiyo kuwekeza nguvu nyingi katika kukabiliana na matishio kutoka nje badala ya matishio ya kiusalama ya ndani ya nchi.


Kwa upande mwingine, kumekuwa na hisia kwamba huenda Erdogan alishirikiana na MIT kuruhusu wapinzani wa chama tawala na serikali ndani ya jeshi la nchi hiyo kufanya jaribio hilo la mapinduzi , lengo likiwa ni kuwa mapinduzi hayo yakishindikana (na lengo ni yashindikane) basi Erdogan awe na kila sababu na haki ya kuendesha taifa hilo kwa mkono wa chuma. Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu Erdogan amekuwa akifanya jitihada za kutaka taasisi ya urais wa nchi hiyo iwe ya kiutendaji kuliko sasa ambapo kinadharia mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu.

Nimalizie makala hii kwa kuahidi kufanya uchambuzi mwingine kadri taarifa mbalimbali zitakavyopatikana. Kwa habari zaidi kuhusu masuala ya ushushushu, bonyeza hapo juu palioandikwa 'INTELIJENSIA,' sambamba na kusoma habari nyingine katika blogu hii.


15 Jul 2016


Uchambuzi wangu wa kiintelijesnia kuhusu shambulio la kigaidi lililotokea jana usiku katika jiji la Nice, nchini Ufaransa ambapo hadi sasa watu 84 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gaidi mmoja kuliingiza lori kwenye kundi la watu waliokuwa wakisherehekea siku ya kitaifa nchini humo. Bonyeza hapo chini kusikiliza uchambuzi huo

Check this out on Chirbit

6 Apr 2015

Twaishi katika dunia ya mfumo dume, na mfumo huo umeota mizizi zaidi katika bara letu la Afrika. Japo jitihada za kitaifa na kimataifa zimeanza kuzaa matunda na sasa twashuhudia taaluma na yandhifa mbalimbali zilizozoeleka kuwa 'za kiume' zikikaliwa na akinamama.

Mfano mmoja wa 'wanawake wanaweza' ni huyu mwanamama, Gladys Sonto Kudjoe, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ushushushu la Afrika Kusini. Hii ni moja ya nyadhifa nyeti kabisa katika taifa lolote lile duniani, kwa sababu ushushushu ndio uti wa mgongo wa taifa (kuna wataokwambia uti wa mgongo wa taifa ni siasa au uchumi...think again!)
Anyway, hapa chini ni wasifu wake (kwa kimombo)

AMB GS KUDJOE

DIRECTOR-GENERAL: STATE SECURITY AGENCY
CURRENT POSITION/S
Ambassador Sonto Kudjoe currently serves as the Director-General of the State Security Agency.  She was appointed into her position in August 2013.
ACADEMIC QUALIFICATIONS 
1981 - 1987: BA and MA Degree in Law.  Specialised in Criminal Law at the Kishinev State University, in the former Soviet Union.

1992 - 1994: Post-graduate Placement Training Programme on the Administration of Criminal Justice and Criminology at the University of Hull, England.
1997: Diploma in Project Management, Damelin, Pretoria.
CAREER / POSITIONS / MEMBERSHIPS / OTHER ACTIVITIES
Prior to her appointment to her current position, Ambassador Kudjoe was with the Department of International Relations and Cooperation (DIRCO), formerly know as the Department of Foreign Affairs.  She has occupied several positions whilst at DIRCO. 
Ambassador Kudjoe held the position of Deputy Director-General: Africa Multilateral.  Her areas of focus whilst in this position dealt primarily with the development and implementation of policies relating to the African Union (AU), the Southern African Development Community (SADC), the New Partnership for Africa's Development (NEPAD), as well as peace and security issues on the African continent. 
Prior to the above position, Ambassador Kudjoe was Deputy Director-General responsible for the Africa Bilateral branch, concentrating on strengthening relations between South Africa and countries on the continent. 
From 2000 to 2002, Ambassador Kudjoe was appointed as the first Chief Director, Africa Multilateral.  Her main responsibilities, amongst others, were the establishment of a new Chief Directorate: Africa Multilateral, the development and implementation of its business plan. 
Between 2002 and 2006, she served as South Africa's Ambassador to Sweden.  She has also served as the country's Ambassador to Egypt for the period 2006 to 2010. 
Ambassador Kudjoe's professional experience also includes working at the former South African Secret Service (SASS) as a Manager responsible for Research, Analysis and Policy Advice on various issues related to Africa.  She has also held the position of Deputy Executive Director at the National Institute for Public Interest Law and Research.4 Apr 2015


Kabla ya kuingia kwa undani kuhusu mada hii, ni muhimu kutanabaisha kuwa uchambuzi huu wa kitaalam (kiintelijensia) unatokana na mchanganyiko wa hisia na facts.Lakini pengine ni muhimu pia kueleza kuhusu nilivyofikia hitimisho lililopelekea kichwa cha habari hapo juu.

Tabia nzuri: Miaka kadhaa wakati nikiwa mtumishi katika taasisi flani huko Tanzania, mkuu wangu wa kazi ambaye pia alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa taasisi hiyo alivutiwa sana na mtizamo wangu wa kutilia mashaka kila jambo. Sio tu kwa vile mtizamo huo uliendana na mafunzo yanayohusu kazi hiyo bali pia ulikuwa na mafanikio. Moja ya kanuni kuu za kazi hiyo ni 'usiamini kitu chochote' sambamba na 'kumini vitu kwaweza kukuletea matatizo au hata kuuawa.' Kwahiyo, kila jambo liliangaliwa kwa pande mbili, huku swali kubwa likiwa 'what if.' Kwa kifupi, mtizamo huo ulisaidia sana kutambua 'ubaya uliojificha katika uzuri.'

Tabia mbaya: Wanasema ukishakuwa mwalimu unabaki mwalimu milele. Nami kwa kiasi kikubwa nimejikuta katika hali hiyo. Uzoefu na ujuzi nilioupata katika kazi hiyo umenifanya niwe mtu wa kutoamini vitu kirahisi, na hata nikiamini bado ninakuwa na wasiwasi flani. Kwa 'maisha ya mtaani,' tabia hiyo ina madhara yake. Kwa mfano, inaathiri relationships kwa kiasi flani maana ili uhusiano uwe imara sharti kuwa na kuaminiana. Kadhalika, jamii inaweza kuniona kama prophet of doom, yaani mtu anayehubiri majanga. Ni rahisi pia kulaumiwa kuwa ni 'mtu wa kuongelea mabaya tu' pale ambapo wengi wanadhani panastahili sifa.

Bottom line: Kinachohitajika ni uwiano kati ya kuamini vitu/watu kwa kuzingatia facts na hisia, kwa uande mmoja, na kutilia shaka vitu/watu kwa kuzingatia facts na hisia. Hili ni rahisi kuliongea lakini pengine ni guu kulitenda hasa kama hisia zinatawala zaidi ya facts, hususan kama hisia zenyewe ni zile zinazofahamika kitaalam kama 'hisia ya sita' (6th sense, yaani zisizotumia kuona, kusikia,kugusa,kulamba,kunusa na kuona)

Baada ya utangulizi huo, tuingie kwenye mada husika. Kuna sababu kadhaa za kimazingira zinazonipa wasiwasi kwamba Tanzania yetu inaweza kukumbwa na shambulio la kigaidi, wakati huu wa sikukuu ya Pasaka au huko mbeleni. Hapa chini, ninabainisha sababu hizo.

Tukio la ugaidi Garisa, nchini Kenya:

Juzi, magaidi wa Al-Shabaab walifanya shambulio kubwa la ugaidi katika mji wa Garisa, uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia.Shambulio hilo limepelekea vifo vya watu takriban 150 huku taarifa mbalimbali zikionyesha uwezekano wa kuwepo idadi kubwa zaidi ya waliouawa. 

Awali, nilikuwa upande wa watetezi wa serikali ya Kenya na vyombo vya usalama vya nchi hiyo katika lawama kwamba walizembea kuchukua tahadhari. Hoja yangu kuu ilikuwa kwamba kupewa taarifa kuhusu ugaidi ni kitu kimoja, kuweza kuzifanyia kazi taarifa hizo na kuweza kuzuwia ugaidi ni kitu kingine kabisa. Hata hivyo, utetezi huo umepungua baada ya kupatikana taarifa mbalimbali zinazoashiria mapungufu makubwa ya serikali ya Kenya na taasisi za Usalama nchini humo kukabiliana na tetesi walizopewa kuhusu uwezekano wa shambulio hilo la kigaidi.

Tukiweka kando kilichojiri nchini Kenya lakini tukitilia maanani ukweli kuwa nchi hiyo ilitahadharishwa kabla ya tukio hilo, kwa Tanzania hali ni tofauti. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa Kenya ina ushairikiano mkubwa zaidi na taasisi za kiusalama za mataifa makubwa zaidi ya Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa Marekani, kwa mfano, ina 'base' yake ya kijeshi nchini humo (Manda Bay


Kwa maana hiyo, tahadharani ya Wamarekani kwa Kenya sio tu kwa maslahi ya Kenya bali ya Wamarekani pia. 

Hitimisho: Kwa kufanikiwa kufanya shambulio kubwa kabisa nchi Kenya, ikiwa ni takriban mwaka na nusu baada ya kufanya shambuli jingine la ugaidi kwenye supamaketi ya Westgate jijini Nairobi, magaidi wa Al-Qaeda wanaweza kushawishika kupanua kampeni yao ya uharamia hadi Uganda (ambako tayari kuna tishio kama ninavyoeleza hapo chini) na hata Tanzania (kwa sababu nitazobainisha mbeleni katika makala hii)

Uwezekano wa shambulio la kigaidi Uganda:

Machi 25 mwaka huu, Marekani ilitoa tahadhari kwa Uganda kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo. Kama ilivyo kwa Kenya, Marekani ina maslahi yake nchini Uganda ambako  inarusha ndege zake za upelelezi (PC 12) kutoka Entebbe, Kwahiyo usalama kwa Uganda una maslahi kwa Marekani pia.

Hitimisho: Iwapo Al-Shabaab watafanikiwa kutimiza uovu wao kuishambulia Uganda (Mungu aepushe hili), wanaweza kupata motisho wa kutanua zaidi kampeni yao hadi Tanzania hasa kwa kuzingatia kuwa kundi hilo la kigaidi linaziona nchi hizi tatu kama kikwazo kikubwa kwa uhai wake. 

Shaka ya ugaidi nchini Tanzania:

Moja ya matatizo makubwa ya kufahamu ukubwa au udogo wa tishio la ugaidi nchini Tanznaia ni siasa. Kwa muda mrefu, chama tawala CCM kimekuwa kikiutumia ugaidi kama kisingizio cha kudhibiti vyama vya upinzani na baadhi ya viongozi wake. Kwa minajili hiyo, hata serikali ikitoa taarifa sahihi kuhusu uwezekano wa tishio la ugaidi, kuna uwezekano wa wananchi wengi kudhani hiyo ni siasa tu.

Kana kwamba hiyo haitoshi, mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge hapo Oktoba. Japo haijazoeleka sana, historia inaonyesha kuwa angalau katika uchaguzi mkuu mmoja uliopita zilisikika taarifa za 'tishio la usalama' kutoka kwa nchi jirani. Mbinu hii hutumiwa na vyama tawala kujenga hofu ya kiusalama kwa wapigakura, na kuwaunganisha chini ya mwavuli wa chama kilichopo madarakani. Kwa mantiki hiyo, iwapo kutakuwa na taarifa za tishio la ugaidi, yayumkinika kuhisi baadhi ya wananchi wakatafrisi kuwa ni mbinu tu ya CCM kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Lakini tatizo kubwa zaidi kwa sasa ni imani ndogo ya wananchi kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete na nyingi ya taasisi za serikali yake. Uhaba huo wa imani unatokana na mchanganyiko wa hisia za ushahidi wa matukio yaliyopita. Kutokana na kuandamwa mno na kashfa za ufisadi, kumeanza kujengeka imani miongoni mwa Watanzania kuwa serikali yao ni ya kifisadi pia.

Matumizi mabaya ya 'taarifa za kiintelijensia' yamewafanya Watanzania wengi kuwa na hisia kuwa 'taarifa za intelijensia' ni mbinu ya serikali kuwadhibiti. Mara kadhaa,Jeshi la Polisi nchini humo limekuwa likipiga marufuku maandamano ya kisiasa au kijamii kwa kisingizio cha 'taarifa za kiintelijensia.' Hivi karibuni, zilipatikana taarifa za mapigano makali kati ya jeshi la polisi wakishirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya 'magaidi' kwenye mapango ya Amboni mjini Tanga. Mchanganyiko wa taarifa za kukanganya na imani haba ya wananchi kwa jeshi hilo vilipelekea tukio hilo kuonekana kama 'mchezo wa kuigiza.'


Lakini licha ya kasoro hizo zinazoihusu serikali na taasisi zake, kuna tatizo jingine linalohusu vyombo vya habari vya nchi hiyo. Utiriri wa magazeti ya udaku na uhaba wa uandishi wa kiuchunguzi katika 'magazeti makini' umekuwa ukichangia mkanganyiko katika kubaini ukweli na porojo. Mfano mzuri ni tukio hilo la Amboni ambalo kwa kiasi flani liligeuka kama mfululizo 'series' ya mchezo wa kuigiza, huku magazeti ya udaku yakiwa na 'habari' nyingi zaidi ya 'magazeti makini.'

Hali hiyo yaweza kuwa inachangiwa na mahusiano hafifu kati ya taasisi za dola na vyombo vya habari, sambamba na mazowea ya taasisi hizo kutoa tu taarifa pasipo kurhusu maswali kutoka kwa wanahabari. Ukosefu wa taarifa sahihi, sambamba na ugumu wa kupata taarifa hizo huchangia 'udaku' kuziba ombwe husika.

Tukiweka kando kasoro hizo hapo juu, hadi sasa kuna mabo yafuatayo ambayo yanaweza kuwashawishi magaidi kuvamia Tanzania.

1. Mgogoro wa muda mrefu kuhusu uanzishwaji wa mahakama ya kadhi: Japo hadi muda huu suala hili limeendelea kuwagawa Watanzania kwa njia za mijadala na kwa amani, yayumkinika kuhisi kuwa magaidi wanaweza kulitumia kama kisingizio cha kuishambulia Tanzania. Cha kutia hofu ni ukweli kwamba sio tu suala hili limedumua kwa muda mrefu, hasa baada ya chama tawala CCM kuahidi katika Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kuwa itaanzisha mahakama hiyo lakini imeshindwa kufanya hivyo hadi leo, bali pia uamuzi usio wa busara wa kuupeleka Bungeni  Muswada wa Uanzishwaji Mahakama ya Kadhi kisha kuuondoa. Kana kwamba hiyo haitoshi, majuzi Rais Kikwete alikaririwa akidai kuwa serikali haina mpango wa kuanzisha mahakama hiyo, na badala yake jukumu hilo linabaki kwa Waislamu wenyewe. Haihitaji uelewa wa sheria kujiuliza kwamba kama suala hilo lilikuwa la Waislamu wenyewe, lilipelekwa Bungeni kwa minajili gani?

Licha ya mjadala huo wa uanzishwaji wa mahakama ya kadhi kuendelea kwa amani, mjadala kuhusu suala hilo umewagawa viongozi wa dini (Wakristo na Waislamu) na kwa kiasi flani umerejesha mgogoro kati ya baadhi ya viongozi wa Kiislam na serikali, sambamba na kuleta sintofahamu miongoni mwa baadhi ya wanasiasa.

2. Vitisho bayana kutoka kwa watu wanaodai ni magaidi.

Hivi karibuni ilipatikana video nchini Tanzania ambapo mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kaisi Bin Abdallah alidai kuwa kundi lao limekuwa na mafanikio katika ugaidi wa kudhuru polisi na vituo vya polisi. Video hii chini inajieleza yenyewe.Licha ya 'mapungufu kadhaa' katika video hiyo, ambayo yanaweza kutupa imani kuwa ni porojo tu, kwa kuzingatia nilichokitanabaisha mwanzoni mwa makala hii, yawezekana tishio lililo kwenye video hiyo ni la kweli. Na hili ni moja ya matatizo ya kukabiliana na tishio la ugaidi: kuchukulia taarifa kuwa ni serious au kuzipuuza.

Hofu kuhusu uwezekano wa matukio ya ugaidi nchini Tanzania ilithibitishwa na kauli ya hivi karibuni ya Rais Kikwete kuwa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali nchini humo yana uhusiano wa ugaidi, japo hakubainisha iwapo kuna uhusika wa makundi ya kigaidi ya kimataifa au la.

3. Taarifa za kimataifa:

Hadi muda huu hakuna taarifa za moja kwa moja zinazoashiria uwezekano wa tukio la ugaidi nchini Tanzania. Hata hivyo, bado kuna hali ya tahadhari wa wastani kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi. Wakati serikali ya Canada inaeleza kuwa haina 'ushauri unaohusu taifa (Tanzania) zima, inawashauri raia wake kuchukua tahadhari kubwa kuhusiana na ugaidi. Kwa upande wake, Serikali ya Uingereza inatoa angalizo la jumla tu japo inatahadharisha kuhusu tishio la ugaidi wa Al-Shabaab kwa eneo  la Afrika Mashariki (ikiwa ni pamoja na Tanzania). Serikali ya Marekani inatoa ushauri wa jumla tu kwa kurejea matukio ya uvunjiafu wa amani huko nyuma.

Hata hivyo, ripoti iliyotolewa LEO na taasisi ya HTH Worldwide kuhusu risks zinazoikabili Tanzania, ugaidi unatajwa kuwa ni tishio la kuamika, japo uwezekano wa kutokea shambulizi la ugaidi ni wa wastani.

Pengine taarifa ya kuogofya zaidi ni ile iliyobainisha uwepo wa jitihada za kundi la kigaidi la ISIS kutaka kujiimarisha katika eneo la Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ISIS inajaribu kujenga ushirikiano na Al-Shabaab kwa minajili ya kuwa na infulence katika eneo la Afrika Mashariki.

Kadhalika, majuzi zimepatikana taarifa kutoka Kenya kuhusu mwanamke mmoja wa Kitanzania aliyekamatwa na wenzie wawili Wakenya wakijaribu kwenda Somalia kuwa wenza wa magaidi wa Al-Shabaab.


 Tukio hilo linaakisi kinachotokea katika nchi mbalimbali za huku Magharibi ambapo mabinti kadhaa wamekuwa wakitorokea Syria kwenda kuwa 'wenza' wa magaidi wa ISIS.

Hitimisho:

Ni vigumu kwa kuwa na hakika ya asilimia 100 iwapo magaidi watafanya shambulio au la. Kwa upande mmoja, magaidi wana muda wote wanaohitaji kabla ya kutimiza azma yao, yaani wanaweza kusubiri kwa muda mrefu, ilhali vyombo vya dola havina faida hiyo kwani vinatakiwa kuwa makini muda wote.

Kuna msemo maarufu kuhusu ugaidi, kwamba wakati magaidi wanahitaji DAKIKA MOJA TU kutimiza uovu wao, vyombo vya usalama vinahitaji KILA SEKUNDE YA DAKIKA kuwazuwia magaidi husika.

Na japo uwepo wa taarifa za uhakika kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi unaweza kusaidia jitihada za kukabiliana na magaidi husika, ukweli mchungu ni kwamba, kuwa na taarifa ni kitu kimoja, uwezo wa kuzitumia taarifa hizo ni kitu kingine.

Wakati huu tunaungana na wenzetu wa Kenya kulaani unyama wa Al-Shabaab, ni muhimu kuchukua tahadhari mahususi ili kuweza kukabiliana na uwezekano wa magaidi hao kushambulia Tanzania. La muhimu zaidi ni umoja na mshikamano, ambao kwa hakika unapotea kwa kasi, na haja ya haraka kwa Serikali kurejejesha imani ya wananchi kwake. Kingine ni umuhimu wa kuweka kando siasa katika masuala nyeti kama haya..

Kubwa zaidi ya yote ni la kitaalamu zaidi. Wakati serikali ya Tanzania imekuwa ikitegemea zaidi msaada wa kimataifa katika kuiimarisha kiuwezo Idara ya Usalama wa Taifa, ni muhimu jitihada za ndani pia zielekezwe katika kuijengea uwezo wa kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na ugaidi. Kwa uelewa wangu, uwezo wa vitengo vya kuzuwia ugaidi na kitengo cha kupambana na ujasusi unaathiriwa na mapungufu ya kimfumo na kisera, sambamba na nafasi ya maafisa wa Idara hiyo kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi 'kubweteka' na teuzi zinazodaiwa kufanywa kwa misingi ya undugu,urafiki au kujuana.

Mwisho, tishio la ugaidi sio la kufikirika. Lipo, na kwa bahati mbaya, mazingira ya kulirutubisha tishio hilo yapo pia. 

26 Mar 2015

The United States said on Wednesday it had information of “possible terrorist threats” to locations frequented by Westerners in Uganda’s capital, Kampala, and warned that an attack could take place soon.
The U.S. Embassy in Kampala issued the warning in a statement posted on its website.
"The U.S Embassy has received information of possible terrorist threats to locations where Westerners, including U.S. citizens, congregate in Kampala, and that an attack may take place soon," it said.
"Out of an abundance of caution, the U.S. mission has canceled some non-essential events scheduled at local hotels in the coming days," it added.
Uganda is a close security ally of the United States in East Africa. The embassy issued similar alerts last year about possible attacks in Uganda.
The embassy cautioned that foreigners staying in or visiting hotels should expect increased security sweeps.
Uganda is one of the countries that contributes forces to an African Union peacekeeping mission battling the Islamist militant group al Shabaab in Somalia.
Al Shabaab, which is aligned with al Qaeda, attacked a shopping mall in Nairobi, capital of neighboring Kenya, in 2013. In 2010, it bombed sports bars in Uganda where people were watching soccer’s World Cup on television. Dozens were killed in both attacks.
SOURCE: Matthew Aid

25 Mar 2015


Wiki mbili zilizopita niliandika makala iliyoonya tabia iliyoanza kuzoeleka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kufanya mzaha kuhusu ugaidi. Kwa muda mrefu sasa, viongozi wa chama hicho hususan Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba wamekuwa wakiihusisha Chadema na ugaidi. Lakini tabia hiyo haikuanzia kwa Chadema pekee kwani huko nyumaCUF nayo ilikumbwa na tuhuma kama hizo kutoka kwa CCM.

Katika makala hiyo ambapo nileleza kwa kirefu kiasi kuhusu hatari inayoikabili dunia hivi sasa kutoka kwa vikundi vinavyoongoza kwa ugaidi kwa muda huu, yaani ISIS, Al-Qaeda, Boko Haram na Al-Shabaab, nilitahadharisha kwamba tabia ya CCM kuufanyia mzaha ugaidi, kwa maana ya kuzusha tu 'Chadema ni magaidi au CUF ni magaidi', inaweza kutugharimu huko mbeleni. Nilibainisha kuwa mzaha huo unaweza kuwarahisishia magaidi halisi dhima ya kushambulia nchi yetu, kwani 'tayari tuna magaidi wa ndani- kwa maana ya tuhuma za CCM dhidi ya Chadema na CUF.

Vilevile nilitanabaisha kwamba kuufanyia mzaha ugaidi kunaufanya uzoeleke, uonekane ni kama jambo la kawaida tu ambalo halikauki midomoni mwa akina Nape na Mwigulu.Lakini pengine baya zaidi ni vyombo vyetu vya dola kuwekeza nguvu kubwa kudhibiti 'magaidi hewa' hali inayoweza kuwapa upenyo magaidi halisi.

Kwa bahati mbaya, tahadhari niliyoitoa kwenye makala hiyo inelekea kubeba uzito, baada ya kupatikana taarifa kwamba kikundi hatari kabisa cha magaidi cha ISIS kina mpango wa kujienga na hatimaye kufanya mashambulizi katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa za kituo cha televisheni cha Aljaazera, mawasiliano ya hivi karibuni ya kikundi hicho cha kigaidi yanaonyesha kuwa kinajaribu kujijenga Afrika Mashariki, eneo ambalo limekuwa likisumbuliwa na magaidi wa Al-Shabaab na Al-Qaeda kwa vipindi tofauti.

Hivi karibuni, kikundi cha kigaidi cha Boko Haram cha Nigeria kimetoa ahadi ya utiifu kwa ISIS, hatua iiliyotafsiriwa na wachunguzi wa masuala ya ugaidi kuwa inaweza kuongeza nguvu za ISIS katika maeneo mbalimbali ya bara la Afrika.

Hata hivyo, kitu ambacho hakikufahamika kwa wengi ni kwamba tukio hilo la Boko Haram kuonyesha utii wa ISIS lilitanguliwa wiki chache kabla ya ujumbe uliotumwa kwa kiongozi wa Al-Shabaab , Abu Ubaidah, kumwomba afanye kama walivyofanya Boko Haram (kutangaza utii kwa ISIS)

Ujumbe huo uliwasilishwa na  Hamil al-Bushra, jina linaloaminika kutumiwa na vyanzo viwili vya habari vinavyohusishwa na ISIS.

Katika ujumbe huo, Bushra aliwapongeza Al-Shabaab na kuwahamasisha wafanya mashambulizi Kenya, Ethiopia na TANZANIA.

Soma habari kamili HAPA

29 Jan 2015

AlexanderLitvinenko.jpg
Ushushushu unaendelea kuwa ni moja ya taaluma hatari kabisa kwa maana ya kutembea na roho mkononi pindi mambo yakienda mrama. Tatizo kubwa la ushushushu sio kutoka kwa maadui wa nje (kwa maana ya taifa la nje au maadui wasio wa kitaifa- non-state actors) bali pia hata maadui wa ndani. Kiasili, migogoro au kukosana ni sehemu ya 'kawaida' katika maisha yetu wanadamu.

Mie katika familia yetu tumejaaliwa kuwa na mapacha. Vitinda mimba katika familia yetu ni Kulwa na Doto. Hawa walipishana kuzaliwa kwa dakika chache tu, na wamefanana mno kiasi kwamba ninapokutana nao baada ya kupotean kidogo tu inabidi niwaulize yupi ni Kulwa na yupi ni Doto. Pamoja na hali hiyo, kuna nyakati hutofautiana na hata kugombana. 

Kwa mantiki hiyo, si suala la ajabu kwa mwajiriwa kukosana na mwajiriwa wake. Wakati kukosana na mwajiri wako katika taaluma nyingine kwaweza kupelekea kushushwa cheo, kuhamishwa au kupoteza ajira, kwa ushushushu hali ni tofauti kabisa. Kutibuana na mwajiri kwaweza kupelekea kifo, kama stori hii hapa chini inavyotanabaisha.

Ukisoma au kusikia balaa lililomwandama Alexander Litvinenko (pichani juu) hadi kifo chake, waweza kudhani ni simulizi kutoka kwenye filamu au riwaya flani. Litvinenko aliwa shushushu wa shirika la ushushushu la Russia, FSB, katika kitendo cha kubaliana na uhalifu mkubwa (organised crime). Kabla ya kuwa shushushu, Litvinenko alikuwa mwanajeshi ambapo alipanda cheo hadi kufikia ngazi ya ukamanda wa platuni.

Mwaka 1986, Litvinenko alianza kuingia kwenye taaluma ya ushushushu baada ya kuwa 'recruited' kuwa mtoa habari (informant) Shirika la zamani la ushushushu la Russia KGB, katika kitengo cha kupambana na ujasusi (counterintelligence). Miaka miwili baadaye, Litvinenko alihamishiwa rasmi KGB kwenye Kurugenzi Kuu ya Tatu iliyokuwa inahusika na military counterintelligence. Mwaka huohuo, baada ya kuhudhuria mafunzo ya ushushushu, Litvinenko akawa shushushu kamili katika eneo la kupambana na ujasusi hadi mwaka 1991, ambapo alipandishwa cheo na kuingia katika Federal Counterintelligence Service, shirika la ushushushu baada ya KGB, ambalo lilidumu kutoka mwaka 1991 hadi 1995lilipoundwa upya kuwa shirika la sasa la ushushushu la Russia yaani FSB. Shushushu huyo alipangiwa kitengo kilichohusika na kukabiliana na ugaidi sambamba na kujipenyeza (infiltration) kwenye makundi ya uhalifu mkubwa. Kadhalika, alikuwa na jukumu la kufuatilia 'maeneo ya moto' (hot spots), yaani maeneo nyeti ndani ya Russia na katika nchi znyingine zilizokuwa ndani ya USSR. Wakati wa vita ya Chechnya, Litvinenko alifanikiwa kupandikiza mashushushu kadhaa ndani ya Chechnya.

Mwaka 1994, Litvitenko alikutana na mmoja wa waliokuwa matajiri wakubwa nchini Russia, Boris Berezovsky (pichani chini) alipokuwa anafuatilia jaribio la mauaji dhidi ya tajiri huyo.


 Hatimaye akaanza kufanya kazi za pembeni kwa ajili ya Boris, na baadaye akawa msimamizi mkuu wa ulinzi wa kibopa huyo. Ofkoz 'ajira' hiyo ya Litvitenko kwa tajiri huyo ilikuwa sio halali lakini dola iliwavumilia hasa ikizingatiwa kuwa mishahara ya mashushushu kama yeye ilikuwa kiduchu.

Mwaka 1997 shushushu huyo alipandishwa cheo na kuingia Kurugenzi ya Uchambuzi na Ukandamizaji wa makundi ya uhalifu mkubwa, akiwa na wadhifa wa mtendaji mwandamizi na naibu mkuu wa Idara ya Saba.

Mwishoni mwa mwaka huo, shushushu huyo alitoa tuhuma nzito kuwa alipewa amri ya kumuua Boris.Mwaka uliofuata, Boris alimtambulisha Litvinenko kwa Vladmir Putin, rais wa sasa wa Russia lakini wakati huo akiwa shushushu mwandamizi wa FSB.
Putin akiwa amezungukwa na walinzi wake

Tatizo ni kwamba Litvinenko alikuwa akipeleleza ufisadi ambao Putin anadaiwa kuwa mhusika. Mwaka huohuo, shushushu huyo na baadhi ya wenzake wallijitokeza hadharani kueleza kuhusu njama za kutaka kumuuwa tajiri Boris.Baada ya tukio hilo, shushushu huyo alitimuliwa FSB na Putin alitanabaisha kuwa ndiye aliyetoa uamuzi huo.

Oktoba 2000, Litvinenko alitoroka Russia na familia yake na kwend Uturuki ambako aliomba hifadhi ya ukimbizi katika Ubalozi wa Marekani jijini Ankara lakini maombi yake yalikataliwa. Inaaminika kuwa kukataliwa huko kulitokana na hofu kuwa kuyakubali maombi hayo kungezua matatizo kati ya Marekani na Russia. Mwaka huohuo,shushushu huyo alinunua tiketi ya kusafiri kwa ndege kutoka Ankara kwenda Moscow kupitia London, Uingereza. Alipofika uwanja wa ndege wa Heatrhow kusbiri ndege ya kwenda Moscow, shushushu huyo aliomba hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa, ambapo maombi yake yalikubaliwa mwaka mmoja baadaye, si kwa sababu ya uelewa wake wa mambo ya ushushushu bali kwa sababu za kibinaadamu (humanitarian grounds).

Wakati akiwa London, Litivnenko alijihusisha na uandishi wa habari, sambamba na kumsapoti tajiri Boris (aliyekimbilia Uingereza) katika mapambano ya kiharakati dhidi ya utawala wa Putin. Oktoba 2006, shushushu huyo alipatiwa uraia wa Uingereza.

Wakati huohuo, gazeti la Independent la hapa, liliripoti kuwa Litvinenko alikuwa akitumia na shirika la ujasusi la Uingereza, MI6 kutokana na ushahidi wa malipo yaliyokuwa yakifanywa na shirika hilo kwa shushushu huyo.

Makao makuu ya shirika la ujasusi la Uingereza MI6 kwenye kingo za Mto Thames, eneo la Vauxhall, jijini London


Mwaka 2007, gazeti moja la Poland lilidai kuwa picha ya Litvinenko ilikuwa ikitumika kwenye mazoezi ya kulenga shabaha (kama huelewi, hiyo ni ishara ya kuwindwa kuuawa). Kabla ya hapo, mwaka 2002, shushushu mmoja wa FSB, Mikhail Trepashkin, alimwonya Litvinenko kuwa kulikuwa na mpango wa kumuuwa uliokuwa ukiandaliwa na FSB. Mwaka huohuo, shushushu huyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za rushwa, japo alikuwa nje ya Russia.
50pxx50pxpx
Nembo ya Shirika la Ushushushu la Russia FSB

Hata hivyo, wakati flani, wasifu wa shushushu huyo ulichafuka baada ya kupatikana taarifa kuwa alikuwa akiwatishia kuwaumbua matajiri kadhaa wa Russia kuhusu uhusika wao kwenye uhalifu mkubwa, na kudai pauni 10,000 kila mara ili asiwaumbue.

Wakati wa uhai wake, shushushu huyo alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya Putin, Russia na mwajiri wake wa zamani FSB. Miongoni mwa tuhuma hjizo ni Russia kuhusika na mashambulizi katika bunge la Armenia yaliyopelekea kifo cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Vazgen Sargsyan, FSB kufanya mauaji nchi Russia na kuwalaumu magaidi wa nje ili kupata uhalali wa kufanya ubabe nje ya nchi hiyo, mdai ya uhusiano kati ya Russia na Al-Qaeda, nk.

Novemba 2006, Litvinenko aliugua ghafla na kulazwa. Baadaye, vipimo vilibaini kuwa alidhuriwa kwa kemikali ya sumu ya Radionuclide Polonium-210. 

Litvinenko akiwa hospitalini jijini London baada ya kudhuriwa na sumu

Katika mahojiano, shushushu huyo alieleza kuwa alikutana na mashushushu wawili wa FSB Dmitry Kovtun na Andrei Lugovoi.Japo wote wawili walikanusha kumdhuru shushushu mwenzao, nyaraka zilizovuja za Ubalozi wa Marekani zinaeleza kuwa chembechembe za kemikali iliyomdhuru Litvinenko zilikutwa kwenye gari alilotumia Kovtun huko Ujerumani.

Dmitry Kovtun, right, with Andrei Lugovoi in 2007. Both deny murdering Alexander Litvinenko
Andrei Lugovoy (kushoto) na Dmitr Kovtun 

Baadaye mwezi huo, Litvinenko alifariki baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi kutokana na sumu iliyomdhuru. Kabla ya kifo chake, shushushu huyo aliandika taarifa iliyoeleza ameuawa.

Juzi, taarifa ya uchunguzi wa kifo chake ilieleza kuwa njia iliyotumika kumuuwa ilikuwa ni ya hatari zaidi kutokea katika Nchi za Magharibi.

Dokta Nathaniel Cary alieleza kuwa kifo cha shushushu huyo mwili wake ulidhurika vibaya mno kabla ya kifo chake kiasi kwamba ililazimu awekwe katika wodi maalum amapo wagonjwa hutengwa kwa ajili ya uchunguzi wa hali ya juu. Alisema kuwa shushushu huyo aliuawa kwa mionzi ya sumu. Kifo chake kilitokea takriban wiki tatu baada ya kunywa chai ambayo baadaye ilifahamika kuwa ilinyunyiziwa sumu ya Polonium.

Dokta Cary alieleza kuwa yye na timu yake walilazimika kuvaa suti mbili za kujikinga (kama zile za matabibu wa Ebola) ambazo ziliwekwa hewa ndanikupitia mirija maalum ili kukwepa athari za sumu husika. Alisema, "uchunguzi huo wa maiti ulikuwa ni usio wa kawaida kabisa katika historia ya nchi za Magharibi"

Natumaini habari hii imekusaidia msomaji kutambua hatari zinazowakabili mashushushu katika utendaji kazi wao, na hasa pale 'wanapotibuana' na aidha waajiri wao au watawala.

12 Oct 2014

Kama mtu mwenye uelewa kiasi kuhusu utendaji kazi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, nimekuwa 'nikipiga kelele' mara kwa mara kuhusu haja ya mageuzi ndani ya taasisi hiyo nyeti. Kwa bahati mbaya sio tu kelele hizo ni vigumu kueleweka kwa Watanzania wengi, uwezekano wa kusikilizwa ni mdogo hasa ikizingatiwa kuwa asili ya taasisi hiyo ni kutekeleza majukumu yake kwa siri, na kama hiyo haitoshi, mara nyingi wahusika wa taaluma hiyo inayopaswa kuhusisha matumizi ya hali ya juu ya akili, hawapendi kusikia ushauri wa 'walio nje' kama akina sie.

Mageuzi ninayoyapigia kelele ni ya kimfumo. Kubwa zaidi ni haja ya uwepo wa mazingira ya uwajibikaji pale watu wanapoboronga. Moja ya dhana zinazotawala fani ya ushushushu ni ile isemayo 'kushamiri kwa matishio ya usalama katika nchi husika ni dalili kuwa taasisi ya ushushushu katika nchi husika ina mapungufu.' Sasa huhitaji uelewa wa fani hiyo kutambua kushamiri kwa matishio kadhaa ya usalama katika Tanzania yetu, kubwa zaidi likiwa ufisadi. 

Labda waweza kujiuliza, iweje ufisadi uwe tishio la usalama? Jibu jepesi ni kwamba ufisadi unatoa fursa kwa maadui wa ndani na nje wa taifa kutimiza azma zao kwa urahisi. Kwa mfano, laiti kukiwa na ufisadi kwenye mipaka ambapo wahusika wanaruhusu kirahisi tu wageni kuingia nchini pasi kuzingatia taratibu zilizopo, ni rahisi kwa magaidi kutumia mwanya huo. 

Ufisadi unaweza kutuletea tapeli la kimataifa kuwekeza kwenye maeneo yanayofahamika kiusalama kama 'vituo muhimu' (vital installations) kama vile viwanja vya ndege na bandarini.

Sasa tukichukulia mfano wa ufisadi, sio tu umeshamiri vya kutosha lakini ndo wazidi kuongezeka. Kuna wanaojiuliza je TISS (Idara yetu ya Usalama wa Taifa) ipo likizo ndefu, wahusika wapo katika usingizi fofofo au kazi imewashinda? Mie sina jibu la moja kwa moja lakini nadhani tatizo la TISS ni la kimfumo zaidi kuliko kiutendaji, japo utendaji wao nao una walakini.

Lakini kabla ya kuingia kwa undani katika mada hii, nirejee kwenye kichwa cha habari. Majuzi, mkuu wa taasisi yenye jukumu la ulinzi wa viongozi wakuu wa Marekani, Secret Service, Bi Julia Pierson alilazimika kujiuzulu wadhifa huo baada ya mtu mmoja kuingia uzio wa Ikulu ya nchi hiyo na kutishia usalama wa Rais Barack Obama. Kwa wenzetu tukio hilo lilikuwa na uzito mkubwa sana, na lilitawala sana katika vyombo vya habari.


Hata hivyo, kwa vile wenzetu wanaendesha mambo kwa uwazi, mwanamama huyo aliitwa mbele ya kamati moja ya bunge la juu la nchi hiyo na kupewa fursa ya kuieleza, ambapo watunga sheria waliafikiana kwamba anapaswa kujiuzulu.
Tukirejea huko nyumbani, ukweli usiopingika ni kwamba licha ya vikwazo vya kimfumo vinavyoikabili TISS, ksingizio  cha 'taasisi hii yafanya kazi kwa siri na hakuna anayepaswa kuhoji' kinatoa fursa kwa wazembe kupata kinga katika utendaji wao mbovu. Ndio, kazi za TISS ni za siri lakini so far usiri huo haujafanikiwa kuwawezesha kukabiliana ipasavyo na matishio ya kiusalama, la wazi likiwa ni ufisadi.

Miongoni mwa mapendekezo yangu (yapo mengi) kuhusu haja ya mageuzi ni kama ifuatavyo.

Kwanza, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu unapaswa kufanywa kwa uwazi zaidi, ikiwezekana kuidhinishwa na Bunge. Hiyo itazuia uwezekano wa Rais kumpatia wadhifa huo mtu yeyote yule bila kuzingatia uadilifu na uwezo wake kikazi. Kwa kumpa Rais 'blank cheque' ni rahisi kwake kumchagua mtu wake, au mshkaji wake kwa minajili ya kumlinda au kuwa kibaraka wake badala ya kulitumikia taifa kiufanisi.
Pili, ni muhimu TISS kama taasisi iwajibike kwa umma, na si kwa Rais pekee (maana huyo Waziri Katika Ofisi ya Rais mwenye jukumu la kuisimamia TISS anakwazwa na mazingira yalivyo, sambamba na 'uoga' wa kawaida). Ifike mahali, watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa Bungeni, kwa mfano, kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu taasisi hiyo.

Kiutendaji, ni muhimu kwa taasisi hiyo kupewa uhuru wa kioperesheni utakaoiwezesha kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa kama tawi la usalama la chama tawala. Sambamba na hilo ni haja ya kuitengenezea mazingira yatayoiwezesha kuhakikisha mapendekezo yake kwa Rais yanafanyiwa kazi hata pale Rais anapoyapuuza. Ikumbukwe kuwa licha ya Rais kuwa 'mkuu halisi wa TISS,' yeye bado ni mwananchi kama wananchi wengine ambao TISS inawajibika kuhakikisha sio tu usalama wao bali hawawi tishio kwa usalama huo. Rais anapopuuza ushauri unaotishia usalama wa taifa basi TISS ijengewe mazingira ya kuhakikisha kuwa ushauri wake unafanyiwa kazi.

Nimalizie kwa kutumaini kuwa 'kelele' hizi zitasikika kwa wahusika. Tujifunze kwa wenzetu waliotatutangulia na wahusika wasione aibu kusikia ushauri wa wenye uelewa hata kama wapo nje ya 'uwanja wa mapambano.'

Endelea kutembelea blogu hii kwa habari mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hizi za ushushushu (bonyeza hapo kwenye menu ya INTELIJENSIA upelekwe moja kwa moja)

bbb The Gatekeeper ni filamu (documentary) inayoeleza kuhusu shirika la ushushusu wa ndani wa Israel, Shin Bet (au Shabak kwa Kiyahudi) kutoka kwa mtizamo wa wakuu sita wa zamani wa shirika hilo (pichani juu) kwa njia ya mahojiano.


 

Endelea kutembelea blogu hii kwa habari mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hizo zinazohusu ushushushu (bonyeza kwenye menu INTELIJENSIA kwenda moja kwa moja). Kuhusu makala ya 'Shushushu ni nani? Anafanya kazi gani?' ninaahidi kuiendeleza katika siku chache zijazo. Ninaomba samahani kwa kuichelewesha.

14 Sept 2014

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kwamba kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislamu (ISIS) kimemchinja kwa kumkata kichwa, David Haines, Mwingereza mfanyakazi wa shirika la misaada, kwa mujibu wa video iliyosambazwa na kikundi hicho.

Video ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.

Tukio hilo limetokea na kurekodia katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa kusoma 'hotuba ya mwisho.'

Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu, "Ninapenda kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia kwa hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair."

Taarifa kamili ya David ni hii

Embedded image permalink

Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha. Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili la leo. Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, "Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu."

3 Sept 2014

Wapiganaji wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao.

Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana. Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley. 

Wapiganaji hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza. 

Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake. Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.

Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq. 

Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani

CHANZO: BBC Swahili

30 Aug 2014

Kikundi cha kigaidi cha Taliban huko Aghanistan kilikuwa kipo tayari kumwachia huru Sajenti wa Jeshi la Marekani Bowe Bergdahl ili kumpata mwanamama huyu. Magaidi wa ISIS nao walikuwa wapo tayari kumwachia mwandishi wa habari wa Marekani waliyemuua kwa kumkata kichwa, James Foley iwapo mwanamama huyo angeachiwa huru. Je kwanini takriban kila kikundi kikubwa cha kigaidi kinamhitaji Aafia Siddiqui?

Miaka miwili iliyopita, maafisa waandamizi wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani walipokea 'ofa' ya kushangaza kutoka Pakistani. Iwapo Marekani wangekubali kumwachia mwanamke mmoja anayetumikia kifungo kirefu huko Texas kwa kosa la jaribio la kuua, basi Sajenti Bowe Bergdahl aliyetekwa na Taliban tangu mwaka 2009 angeachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za kiusalama, Rais Barack Obama na maafisa wake walikataa 'ofa' hiyo. Kumwachia mwanamke huyo, Bowe Bergdahl kunekinzana na msimamo wa Marekani wa kutofiki amakubaliano na magaidi. Kadhalika, kumwachia huru mwanamke huyo kungemrejesha uraiani mtu hatari kwa usalama.

Siddique, mwenye umri wa miaka 42, na anayefahamika kwenye anga za kupmbana na ugaidi kama 'Lady al-Qaeda' ameshahusishwa na mmoja wa magaidi wahusika wa  mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 Khalidi Sheikh Mohammed, na wakati flani alikuwa katika orodha ya magaidi wanaosakwa zaidi (most wanted terrorist list).

Gaidi huyo wa kike alipata elimu yake katika chuo kikuu kinachoheshimika sana duniani cha M.I.T na ana shahada ya uzamifu (PhD). Mwaka 2008, alikamatwa akiwa na kemikali ya Sodium Cyanide, pamoja na nyaraka za jinsi ya kutengeneza silaha za kemikali, mabomu ya kusababisha madhara makubwa (smart bombs) na jinsi ya kuitumia Ebola kama silaha. Maofisa wa Shirika la Upelelezi la FBI walipojaribu kumhoji, mwanamke huyo alichukua silaha na kufyatua risasi.

Japo Marekani haikulipa uzito wazo la kubadilishana mwanamke huyo na 'mateka waliokuwa mikononi mwa magaidi,' Siddique amekuwa turufu muhimu kwa magaidi kila linapokuja suala la 'kubadilishana mateka' mbalimbali wa Marekani na Ulaya walio mikononi mwa magaidi.

Jumanne iliyopita, kikundi cha kigaidi cha ISIS kilidai gaidi huyo wa kike aachiwe huru ili nao wamwachie huru mwanamke mmoja wa Kimarekani aliyetekwa huko Syria alipokuwa akifanya kazi katika shirika la misaada ya kibinadamu. Maafisa wanaamini kuwa ISIS inawashikilia mateka angalau Wamarekani wengine wanne, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa habari Steven Sotloff. Magaidi hao wanataka kulipwa Dola za Marekani milioni 6.6 ili wamwachie huru mwanamke huyo mtumishi wa shirika la misaada ya kibinadamu ambaye ndugu zake wameomba jina lake lihifadhiwe.

Wakati Ikulu ya Marekani imekuwa ikikataa katakata wazo la kumwachia huru mwanamke huyo gaidi ili kuwezesha kuachiwa huru kwa mateka wa nchi hiyo waliopo katika mikono ya magaidi, "Twafahamu kuna wanaotengeneza mazingira katika 'Wizara ya Ulinzi' ya kuangalia uwezekano wa kubadilishana mateka kwa kumtumia Siddique."

Mjadala mkubwa uliibuka baada ya kuchinjwa kwa Foley kuhusu aidha kulipa fedha kwa magaidi au kuwaachia wafungwa kama wanavyodai magaidi hao. Marekani, tofauti na nchi nyingi za Ulaya, huwa hailipi fedha kwa ajili ya kuachiwa huru raia wake waliotekwa. Na inaelezwa kuwa hiyo ni miongoni mwa sababu zinazowavunja moyo magaidi kuwateka nyara Wamarekani kwa minajili ya kudai fidia ili mateka hao waachiwe huru, kwa mujibu wa mtaalam mmoja wa ugaidi.

Siddique ni kama 'celebrity' flani nchini Pakistan, ambapo kifungo chake mwaka 2010 kilipelekea maandamano nchini humo (Pakistan). Matokeo ya kifungo cha Siddique yalikuwa hahabari zilizoongoza katika magazeti yote makubwa.

Hukohuko Pakistan, kikundi kijiitacho 'Brigedia ya Aafia Siddique'kimeshafanya mashambulizi kidhaa dhidi ya serikali ya nchi hiyo kama upinzani na malalamiko yao dhidi ya wanachokiona kama kifungo kisicho cha haki kwa mwanamke huyo hatari.

CHANZO: Jarida la Foreign Policy20 Aug 2014

Nianze makala hii kwa kuomba samahani kutokana na kuchelewesha mfululizo huu wa makala kuhusu taaluma ya ushushushu. Baadhi ya wasomaji wamehoji ukimya huo, huku wengine wakidhani kwamba 'wahusika' wamenizuwia. Ninapenda kurejea nilichokiandika katika sehemu ya kwanza ya makala hii kwamba mfululizo huu unazingatia sheria na maadili na 'wahusika' hawana sababu ya kuuzuwia.

Kwa kukumbushana tu, sehemu ya kwanza iliitambulisha taaluma ya ushushushu kwa ujumla, wakati sehemu ya pili ilielezea jinsi mashushushu wanavyopatikana (recruitment). Katika sehemu hii ya tatu tutaangalia mafunzo ya mashushushu wanafunzi.

Ninakumbuka siku moja niliwahi kuulizwa swali na rafiki yangu flani huko Twitter iwapo walinzi wa viongozi (bodyguards) nao ni mashushushu kwa maana ya kupitia mafunzi kama 'mashushushu wa kawaida.' Jibu langu kwake litatoa mwelekeo wa makala hii, kwamba, kwanza japo taaluma ya ushushushu ina maeneo flani yanayofanana mahala popote pale duniani, vitu kama mazingira, mahitaji ya nchi/taasisi ya kishushushu, na pengine uwezo wa kiuchumi hupelekea tofauti kati ya taasisi moja na nyingine. Nitoe mfano. Kwa nchi kama Marekani, taasisi ya kishushushu inayohusika na ulinzi wa viongozi (US Secret Service) 'inajitegemea' kwa maana ya ajira,mafunzo na utendaji kazi. Wanaojiunga na taasisi hiyo ni lazima wapitie kozi ya awali ya upelelezi wa jinai (Basic Criminal Investigator Training) inayodumu kwa wiki 10, na inayofanyika katika chuo cha Federal Law Enforcement Training Centre kilichopo Glynco, Georgia, na kisha kufanya kozi nyingine ya wiki 17 inayojulikana kama Speicla Agent Basic Training, inayofanyika katika chuo cha James J. Rowley Training Centre, nje kidogo ya jiji la Washington DC.

Kwa minajili ya kuepuka mkanganyiko, nitatumia mfumo unaotumiwa na Idara yetu ya Usalama wa Taifa (TISS) katika maelezo kuhusu mafunzo ya mashushushu. Tofauti na Marekani, Idara yetu ya Usalama ni taasisi moja yenye vitengo mbalimbali. Na katika jibu nililompatia rafiki yangu ailiyeniuliza huko Twitter, maafisa usalama wanaolinda viongozi wetu huajiriwa kama afisa usalama mwingine yeyote yule. Katika mazingira ya kawaida, baada ya Idara ya Usalama wa Taifa kumaliza mchakato wa kuwapata mashushushu watarajiwa (process niliyoieleza kwa undani katika makala iliyopita), hatua inayofuata ni mafunzo. 

Kwa huko nyumbani, kila shushushu mpya hupatiwa mafunzo kupitia kozi ya awali ya uafisa (Junior Basic Course) katika chuo chao kilichopo pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam. Urefu wa kozi hutegemea vigezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya Idara yenyewe. 

Muundo wa mafunzo:

Kimsingi, na katika mazingira ya kawaida, kozi hiyo ya awali hugawanywa katika sehemu kuu tatu: mafunzo ya kijeshi na ukakamavu, mafunzo ya mapambano pasipo silaha (unarmed combat) na mafunzo ya ushushushu 'halisi.'

Mafunzo ya kijeshi na ukakamavu hujumuisha 'kwata' za kijeshi (kama zile wanazofunzwa 'makuruta' katika Jeshi la Kujenga Taifa). Kabla ya kuanza kozi hii, mashushushu watarajiwa hufanyiwa uchunguzi wa kiafya kubaini iwapo wataweza kumudu shuruba zinazoambatana na kozi hiyo. Na kwa hakika ni hatua ngumu mno, ambapo kwa takriban kila 'intake' kuna 'wanafunzi' wanaoamua kuomba ruhusa ya kuondoka baada ya kushindwa kustahilimi ugumu wa mafunzo hayo. 

Haya ni mafunzo ya kijeshi 'halisi' kwa maana ya drills za kijeshi, mafunzo ya msingi ya kivita ikiwa ni pamoja na usomaji ramani katika uwanja wa mapambano, ulengaji shabaha, uelewa kuhusu silaha mbalimbali, nk. Sambamba na mafunzo hayo ni mazoezi makali ya viungo na ukakamavu. Kadhalika, mafunzo hao huambatana na kujenga nidhamu ya kijeshi pamoja na uvumilivu (ni jambo la kwaida kwa 'wanafunzi kupitisha usiku kadhaa bila kulala). Mafunzo haya huendeshwa na wakufunzi wa kijeshi ambao pia ni waajiriwa wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Hatua inayofuata ni kozi ya mapambano bila silaha (unarmed combat). Katika kozi hii, mashushushu watarajiwa hufundishwa jinsi ya kupambana na adui kwa kutumia mwili pekee, yaani bila kuwa na silaha. Walimu wa kozi hii huitwa Sensei na kozi hujanyika katika ukumbi ujulikanao kama dojo. Kadhalika, 'wanafunzi' huvaa ' mavazi maalum' yajulikanayo kama Kimono.

Pasipo kuingia ndani zaidi, kozi hii hufuata mfululizo wa hatua zinazojulikana kama 'kata.' Kwa lugha nyepesi, kata ni movements za mtu mmoja mmoja au zaidi, na kila moja ni mfumo wa mapambano. Kila kata ina jina, na majina hayo yana asili ya Mashariki ya Mbali, ambapo fani ya mapambano bila silaha ni sehemu muhimu ya utamaduni kwa nchi kama China,Japan, Korea, nk. Ili kujifunza kata inayofuata ni lazima kuimudu kata ya awali. Ni kama vile hatua za makuzi ya mtoto, hawezi kuanza kukimbia kabla ya kutamaa.

Kwa minajili ya kurahisisha maelezo, kozi hii hujumuisha karate, judo,ngumi,nk. Kadhalika, japo mafunzo yanaitwa mapambano bila ya silaha, ukweli ni kwamba kuna baadhi ya kata huhusisha matumizi ya/ kujilinda dhidi ya silaha ndogo japo hatari kama vile visu, jambia la mapambano, minyororo, nk. Katika kozi hii, 'wanafunzi' hufunzwa pia kuhusu 'sehemu za udhaifu katika mwili wa binadamu' (weak points) kwa minajili ya kutambua eneo gani la mwili wa adui likidhibitiwa anakuwa 'hana ujanja.'

Hatua ya tatu ni mafunzo 'halisi' ya ushushushu. Kwa ujumla, mafunzo haya humfundisha shushushu mtarajiwa mbinu za kukusanya taarifa za kiusalama kwa siri, kuzichambua na 'kuzifanyia kazi.' Kwa ujumla pia, kozi hii hugawanywa katika makundi mawili: ushushushu ndani ya nchi na ujasusi ushushushu nje ya nchi. Kadhalika, masushushu wanafunzi hufunzwa  kitu kinachoitwa 'shughuli za adui' yaani ujasusi (espionage), uzandiki (subversion), hujuma (sabotage) na ugaidi (terrorism). Vilevile, hufunzwa mbinu za kunasa mawasiliano (bugging), ufuatiliaji wa siri (surveillance), jinsi ya kupata watoa habari (recruitment of sources) na jinsi ya kuwamudu, ikiwa na pamoja na jinsi ya 'kuwamwaga' (kuachana nao) pale wanapopoteza umuhimu. 

Pengine la kuchekesha katika hatua hii ya mafunzo ya ushushushu ni hisia kwamba 'mashushushu hufundishwa kutongoza.' Kuna aina flani ya ukweli katika hilo japo kinachofundishwa sio jinsi ya kutongoza mwanamke bali kutongoza kwa minajili ya kupata taarifa. Na pengine neno 'kutongoza' sio stahili kwani lina connotation na mambo ya ngono. 

Japo mbinu za kukusanya taarifa za kiusalama (methods of elicitation) ni maalum kwa matumizi ya mashushushu, kimsingi zinatumika katika fani nyingine, kwa mfano watafiti wanapofanya mahojiano kwa ajili ya tafiti zao.Tofauti ya msingi ipo kwenye usiri unaoambatana na mbinu husika, kwa mfano mtu kuhojiwa pasi kujua anahojiwa na shushushu. Mfano mmoja wa mbinu hizo ni kinachotwa 'incorrect supposition.' Mbinu hii inatumia udhaifu wa kawaida wa binadamu kutotaka kuelezwa isivyostahili. Kwa mfano, katika kutaka kufahamu kama mtumishi wa kawaida tu ana 'fedha zaidi ya uwezo wake.' shushushu anaweza kumwambia mtu huyu "ah inadaiwa wewe ni masikini tu ambaye hata kodi ya nyumba ya kupanga inakusumbua." Katika mazingira mwafaka, mhusika atakurupuka na kujigamba, "ah wapi bwana. Utawaweza waswahili kwa uzushi? Mie nina nyumba kadhaa hapa mjini, na lile duka la spea pale Kariakoo ni langu..." Kwahiyo wakati mwingine ukiskia mtu anang'ang'ania kusema kitu kisicho sahihi dhidi yako, usikimbilie kudhania anakudhalilisha au hajui ukweli.Yawezekana 'anakulengesha' umpatie ukweli anaohitaji.

Mbinu nyingine ni ya 'nipe nikupe.' Nakupa unachodhani ni taarifa za siri (naam, pengine ni za siri kweli lakini hazina madhara) ili nawe unipe taarifa ninazohitaji. Ni kile wanaita 'Quid Pro Quo.'

Jambo jingine ambalo mashushushu wanafunzi hufundishwa muda wote ni kitu kinachofahamika kama constant vigilance of an officer, yaani afisa usalama wa taifa anapaswa kuwa macho muda wote, huku akitambua kuwa uhai wa taifa lake upo mikononi mwake muda wote. Pengine tafsiri ya kanuni hiyo ni 'kujitambua muda wote.' Kutambua dhamana aliyonayo afisa usalama kwa taifa. Kadhalika, mafunzo huhusisha pia kujenga na kuimarisha matumizi ya 'hisia ya sita.' Kama nilvyoeleza katika makala ya kwanza, binadamu tuna hisia tano: kuona kwa kutumia macho, kusikia kwa kutumia masikio, kunusa kwa kutumia pua, ladha kwa kutumia ulimu na kuguswa (touch) kwa kutumia ngozi. Hisia ya sita ni kitu cha zaida ya hivyo vitano. Ni vigumu kueleza katika mazingira ya kawaida ila labda kwakifupi ni ule uwezo wa kwenda mbali zaidi ya uwezo wa kawaida wa hisia: kuamini au kutoamini pale inapopaswa kuamini au kutoamini, kutambua hatari hata bila ya kupewa tahadhari, nk.

Awali nimetaja kuhusu vitendo vya adui, yaani ujasusi, uzandiki, hujuma na ugaidi. Kimsingi japo hivi ni vitendo vya adui na njia ya kupambana nayo ni kinachojulikana kama counterintelligence au CI kwa kifupi, mashushushu wanafunzi hufunzwa pia mbinu 'za kiadui.' Ni hivi, kuna nyakati serikali au taasisi ya usalama hulazimika kupelekea amshushushu wake nje ya nchi, na kimsingi hawa ndio wanaoitwa spies, na kitendo chenyewe ndio espionage (ujasusi), lengo si 'kutengeneza maadui' bali kuwapatia mashushushu uwezo wa kukusanya taarifa za kiusalama nje ya nchi. Miongoni mwa kanuni anazofundishwa shushushu mwanafunzi ni pamoja na uwezekano wa kukanwa na nchi yake pindi akikamatwa kwenye operesheni za nje ya nchi. Vilevile, mashushushu hufunzwa kuhusu kitu kinachofahamika kama 'kifuniko' (cover ) yaani utambulisho bandia. Kwa mfano, balozi takriban zote duniani huwa na majasusi wanaojipachika vyeo kama 'mwambata wa siasa' au mwabata wa ulinzi.' Ieleweke kuwa japo ushushushu ni fani inayokubalika, serikali rafiki ikitambua shughuli za maafisa usalama wa nchi nyingine rafiki, yaweza kupelekea matatizo makubwa. Na mara nyingi ukisikia serikali imewafukuza maafisa ubalozi flani basi mara nyingi watu hao ni mashushushu 'waliojificha' kama maafisa ubalozi.

Vilevile, katika muda wote wa mafunzo, mashushushu watarajiwa huhamasishwa kuhusu uzalendo, thamani ya nchi yao, umuhimu wa kuilinda muda wote, umuhimu wa taaluma hiyo katika ustawi na mustakabali wa taifa lao,nk. Na siku ya kuhitimua mafunzo, kila shushushu huapa kwa kushika alama muhimu za taifa- katiba/bendera ya taifa, na kuweka kiapo cha kuitumikia nchi yake kwa uwezo wake wote, sambamba na viapo vingine vya kikazi (kwa mfano kamwe kutotoa siri za nchi na za Idara). Japo kuna hisia 'mtaani' kwamba watu walioacha au kuachishwa ushushushu huogopa kutoa siri kwa kuhofia kuadhibiwa, ukweli ni kwamba kiapo wanachokula wakati wa kuhitimu mafunzo ni 'kizito' mno kiasi kwamba katika mazingira ya kawaida, mhusika atajiskia nafsi inamsuta kusaliti kiapo hicho. 

Licha ya mafunzo ya darasani, kuna mafunzo ya nje ya darasa ambapo mashushushu watarajiwa 'humwagwa mtaani' kufanya mafunzo ya vitendo. 

Kubwa zaidi wakati mafunzo yanaendelea ni usiri wa hali ya juu. Katika mazingira ya kawaida, kila shushushu mwanafunzi huwa amefika ukweli kuwa anaenda/ yupo mafunzoni. Na kuficha huko si kwa marafiki tu bali hata wazazi na ndugu wa karibu. Na hapa ni muhimu kueleza kwamba moja ya vitu anavyokumbushwa afisa usalama wa taifa tangu hatua za mwanzo za kujiunga na taaluma hiyo hadi katika maisha yake ya kila siku ni KUWA MAKINI NA IMANI, au kwa lugha nyingine USIMWAMINI MTU YEYOTE. Wanasema TRSUT WILL GET YOU KILLED, yaani IMANI (kwa mtu au kitu)  ITAKUUWA. Kwahiyo si jambo la ajabu kwa shushushu kutomwamini hata mzazi, ndugu au mwenza wake. 

Kwa leo ninaomba kuishia hapa. Endelea kufuatilia mfululizo wa makala hii, ambapo toleo lijalo litaangalia kidogo kuhusu aina nyingine za mafunzo na kuangalia kwa undani kuhusu 'maisha ya shushushu mtaani,' yaani baada ya kuhitimu mafunzo yake. Unaweza kusoma habari za intelijensia kirahisi zaidi kwa kuonyeza INTELIJENSIA hapo kwenye menu ya blogu hii.
Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.