28 Feb 2010

bu
MBUNGE wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) juzi jioni alimuacha hoi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, pale alipowapa salamu ya shikamoo watoto ili pamoja na wazazi wao wamchague tena kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.

Tukio hilo lilitokea wakati Waziri Mkuu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Sikonge katika mfululizo wa ziara yake ya kuutembelea Mkoa wa Tabora.Kabla ya Waziri Mkuu kuanza kutoa hotuba yake, Nkumba alipewa nafasi ya kuwasalimia wapiga kura wake, ndipo alipoitumia nafasi hiyo kutangaza nia ya kugombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakati ulipokuwa ukiahirisha kikao cha Bunge kilichopita ulisema sasa ni wakati muafaka kwetu kurudi kwa wapiga kura wetu ili kuwapa shikamoo.

“Leo ni siku ya bahati kwani watu wengi wamejitokeza katika mkutano wako huu na mimi naomba kuitumia nafasi hii kutoa shikamoo. “Kwa heshima na taadhima shikamoooni watoto wote mliopo hapa kuanzia mnaonyonya, watoto wa halaiki, watoto mliopo shuleni na shikamooni vijana na wazee wote mliopo hapa,” alisema Nkumba.

“Napenda sasa kutumia nafasi hii kutangaza nia kwamba nitagombea tena ubunge katika Jimbo la Sikonge na naomba wote mniunge mkono,” alisema Nkumba.
Tukio hilo lilimfanya Waziri Mkuu aliyekuwa amekaa jukwaani na viongozi wengine wa kitaifa, mkoa na wilaya, kuvunjika mbavu kwa kicheko.

CHANZO: Habari Leo

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.