31 Dec 2010


Wanasema ukitaka kumjua Mswahili ni mtu wa aina gani subiri apate madaraka.Muda mfupi uliopita nikiwa Facebook nilikutana mtandaoni na Mheshimiwa flani aliyebahatika kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa wana nchi (Mbunge) katika uchaguzi mkuu uliopita.Kwa vile sikuwahi kumpatia pongezi zangu kwa ushindi wake wa kishindo dhidi ya mgombea wa chama tawala,nikaonelea si vibaya kutumia fursa hiyo kumwambia maneno haya (nanukuu)

MHESHIMIWA,NAOMBA KUKUPA HONGERA KWA USHINDI.KILA LA HERI KATIKA UJENZI WA TAIFA LETU.HAPPY NEW YEAR 2011.

Kwa vile ujumbe wangu huo ulishaashiria kuwa lengo langu ni pongezi na heri ya mwaka mpya tu,na sio kurefusha maongezi,nilitarajia japo "Thanks" au "Poa".Lakini,kama ilivyo kawaida kwa Waheshimiwa wengi,Mheshimiwa huyo ambaye nilijaribu kumsapoti yeye na chama chake wakati wa kampeni,akahisi labda nataka "kumpiga mzinga/kirungu" ( kuomba msaada).Hakujali pongezi za mie mwananchi (na sapota wake), "akauchuna",kisha akatoka nje ya chumba cha kuchati logged out of the chatroom).Nilifadhaika hasa kwa vile namchukulia mwanasiasa huyu kijana kama role model kwa makundi mbalimbali ya vijana katika jamii yetu (safari yake hadi kuwa Mheshimiwa is truly inspirational na inaweza kuzalisha changamoto na tumaini jipya kwa vijana mbalimbali).Zaidi,dadangu mmoja anayemfahamu fika Mheshimiwa huyo aliwahi kuniambia kuwa mwanasiasa huyo mpya ni mtu humble (poa) sana.Very down to earth licha ya umaarufu aliokuwa nao kabla ya kujitosa kwenye ulingo wa siasa.Na kilichonisukuma "kujikomba" kutoa salamu na pongezi ni ukweli kwamba ni nadra kukutana na kigogo kwenye chatroom ya Facebook,na uwepo wake niliutafsiri (wrongly?) kuwa dalili ya utu poa (humility) wake.How wrong!

Lakini kwa ujumla nadhani ni dharau tu,na kasumba iliyobobea miongoni mwa Waswahili waliokwaa madaraka kuwapuuza "wat wa kawaida (yaani tusio na umuhimu).Ila nachopata shida kuelewa ni je Waheshimiwa kama huyu ninayemzungumzia hapa wanapungukiwa na kitu gani wakiamua kuonyesha kuwa uheshimiwa wao hauondoi ubinadamu wao?Watavuliwa madaraka?Wataamvukizwa maradhi flani?Vitambi vyao vitasinyaa (na vitambi vyao vinatafsiriwa nao kama part and parcel of uheshimiwa wao just like kipara-au ualaza- na wasomi njaa).Yah,Uswahili unaambatana na imani za ajabu kabisa.Hakuna uthibitisho wa kisayansi kuwa upungufu wa nywele kichwani unamaanisha ufanisi wa ubongo.Na kwa namna hiyohiyo,ukubwa wa tumbo-ambao pengine ni matokeo ya kuelemewa na pombe kama sio dalili za kwashakoo- haupaswi kuwa kigezo cha uheshimiwa hususan pale Mheshimiwa anapokuwa mtovu wa heshima.

Pengine msomaji mpendwa unaweza kunishutumu kuwa nafanya ishu hii kuwa big deal.Well,nimekuwa mfuasi mzuri sana wa dadangu mmoja,bloga maarufu Dinahicious,ambaye huko Twitter anatoa elimu ya bure kwa mtindo wa "wape vidonge vyao".Mdada huyu ni kama mtambo wa kurekebisha tabia zinazokera,hususan za hao wanaojiona watu maarufu.Kwani mtu ukiwa maarufu-hata kama hisia hizo za umaarufu ni za ndotoni tu-kisha ukawa-treat wanadamu wenzio kama watu hai na sio mawe,umaarufu huo utadidimia?

Natumaini Mheshimiwa huyu nayemzungumzia atasoma makala hii (kama ana muda.Si unajua sifa mojawapo ya uheshimiwa wa Kiswahili ni kuwa bize?).Madaraka ni kitu cha kupita,ilhali utu wa mtu ni kitu cha kudumu.Waheshimiwa wetu wanapaswa kujifunza kwa kwa watu kama Nyerere,Mandela,Martin Luther King,Jr,Mahatma Ghandi,Mama Theresa na hata Mitume ambao waliishi maisha ya unyenyekevu huku wakitambua kuwa uongozi wao ni matokeo ya imani kutoka kwa wanaowaongoza.

Kuisha kwa uchaguzi na kukwaa madaraka kusiwe sababu ya kususa hata salamu za pongezi kutoka kwa watu wa kawaida kama sie.Biblia inatuasa kuwa wajikwezao watashushwa na wajishushao watakweza.

Naamini ujumbe umefika,loud and clear!

1 comment:

  1. Pole sana kwa maswahaibu hayo yaliyokukuta. Ushauri wa bure kumfahamu mtu binafsi kwa mawasiliano siyo tatizo ni mtu unayetaka kufahamia naye.

    Ni mtu wa namna gani kwa tabia yake binafsi Nadhani ilo ndilo la msingi hapo. Achana kutaka kufahamiana na mtu kwa ukaribu hasa wanasiasa isipokuwa piam huduma yake kwa jamii na maendeleo na huo ndiyo ubaki uhusiano wako na yeye.

    Iwapo anashindwa kusaidia jamii na maendeleo basi mlete hapa blogini kama ulivyofanya sasa na sisi tutamjadili na kumpa vidonge vyake au sifa anazostahili

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.