24 May 2011

Mwangalie kwanza.Hivi abiria watasafiri kwenye hilo lijinembo lisilo na mvuto?Au anamaanisha wapande kwenye mkono wake alioinua?Hovyoooo!!!!

Unajua,baadhi ya viongozi nchini Tanzania wanatuona sie kama machizi vile.How come mtu anayeamua kuondoka katika shirika mfu ajigambe kwa kubadilisha nembo?Huu ni uhuni wa hali ya juu.Lakini uhuni huu unasababishwa na anayeteua wahuni wa aina hii,I mean Rais Jakaya Kikwete.
Hivi Kikwete anajisikiaje kumsikia rafiki yake Mattaka akiwatusi Watanzania kwa kujivunia mafanikio ya nembo mpya ilhali ATC haina ndege hata moja inayoruka?Majuzi tu,Kikwete kaendelezakulialia kuhusu wasaidizi wake anaodai ni mzigo-kana kwamba walimshikia mtutu wa bunduki awateue,na wameendelea kumshikia mtutu wa bunduki asiwatimue.Hii misemina elekezi ya kila kukicha inasaidia nini katika mazingira haya ya mchezo wa kuigiza wa kisiasa ambapo watu wanaosifika kwa tabia zao chafu kuliko ufanisi wao wanaruhusiwa kula fedha za walipa kodi,only kuondoka kwa matusi dhidi ya walipa kodi hao hao?

It's sooo disgusting.Enewei,soma kichekesho hiki kinachoudhi

Mattaka ang'oka ATCL 
Monday, 23 May 2011 21:56

Fredy Azzah

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka ametangaza kustaafu kazi huku akijivunia kubadilisha nembo, ingawa ameliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka.

Mattaka aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa alistaafu rasmi Mei 11, mwaka huu baada ya kufika umri wa miaka 60 na kwamba alishindwa kulifufua shirika hilo la umma kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa menejimenti. Alitaja moja ya sababu hizo kuwa ni mzigo wa madeni.

“Naondoka lakini najivunia kuiondoa ATCL chini ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) waliokuwa wameingia ubia, pia najivunia kuleta nembo mpya ambayo inatumika sasa,” alisema Mattaka.

Desemba 2002, Shirika la Ndege Tanzania (ATC), lilibinafsishwa kwa kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na kubadilisha jina lake kuwa “Air Tanzania Company Limited” (ATCL). “Wanasema najiuzulu.

Hii siyo kweli, nastaafu kwa mujibu wa sheria, ingetakiwa nistaafu kuanzia Mei 11, lakini ni barua tu ndiyo ilichelewa kuja, nimeomba kustaafu na nimekubaliwa,” alisema Mattaka. Mattaka alisema tangu kuteuliwa kwake kuliendesha shirika hilo mwaka 2007, walikuwa na nia ya kulifufua lakini sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao zilikuwa kikwazo.

“Shirika lolote la ndege linahitaji mtaji ili liweze kujiendesha, sisi tumechukua shirika likiwa na mtaji hasi wa Sh43 bilioni na madeni yaliyofikia Sh23 bilioni,” alisema Mattaka.

Alisema katika kujitahidi kulifufua shirika hilo, kuanzia mwaka 2007 mpaka mwishoni mwa 2008, walifanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kununua ndege moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50 na kukodi nyingine aina ya Air Bus, shughuli ambayo alisema waliifanya katika mazingira magumu.

Alisema baada ya mwaka huo, mafuta ya ndege yalipanda kwa zaidi ya asilimia 50, jambo lililoyafanya mashirika mengi ya ndege yaliyokuwa yakiendeshwa bila ruzuku ya serikali kuanguka.

“Mwishoni mwa 2009 ndipo serikali ikaanza kutoa fedha kidogo kidogo ambazo hata hivyo, ilizielekeza kwenye kulipa madeni. Napenda tu kusema kuwa sasa serikali inatakiwa kuwa na shirika lake la ndege,” alisema Mattaka na kuongeza: “Unapokuwa katika shirika la umma ukastaafu bila matatizo ni jambo la kumshukuru Mungu, kwa hiyo kwa sasa napenda tu kumshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa.”

Amlaumu Mkapa
Awali, Mattaka alisema katika uongozi wake ndani ya mashirika ya umma, kamwe hatamsahau Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alimsimamisha alipokuwa Mkurugunzi wa Mfuko wa Jamii wa (PPF) kutokana na kashfa mbalimbali, ikiwamo ya rushwa na ubadhirifu wa fedha.

Anasema kitendo cha kusimamishwa kwake ghafla kilimuumiza sana, ingawa anadai kuwa baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa kuchunguza, walibaini kuwa hapakuwa na ukweli wowote wa kashfa zilizomfanya asimamishwe kazi.

“Unajua bwana siku zote mti wenye matunda ndiyo hurushiwa mawe, waliona majengo yanaibuka tu, mara PPF House, PPF Tower na kile Kijiji cha PPF kule Arusha, wakasema lazima hizi ni 10 percent.” “Walichunguza wakakuta yote yale hayana ukweli wowote na wakanilipa stahili zangu ambazo ndizo zilinifanya nikae takribani miaka ninne mpaka nilivyokuja tena huku ATCL.”

Alisema ameondoka ATCL na kuliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka akidokeza kwamba moja ipo Afrika Kusini ikifanyiwa matengenezo ambayo anasema yamekamilika na kinachosubiriwa ni Serikali kulipa fedha za matengenezo.

Alisema ndege nyingine ipo nchini lakini haifanyi kazi kutokana na kuhitaji matengenezo ya lazima. Mattaka alisema, serikali imemteua William Haji, kukaimu nafasi anayoiacha.

CHANZO: Mwananchi

1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.