30 Apr 2010

Mtakatifu au mzushi?

Raia mmoja wa India amegusa hisia za jeshi la nchi hiyo kutokana na madai yake kwamba haitaji chakula wala maji kumudu kuishi.Prahlad Jani anadai yeye ni 'breatharia',yaani mtu anayeweza kuishi kwa kutumia nguvu za asili za kiimani.Anadai anapata nguvu hizo za asili kutoka kwa 'mungu wa kike' anayemmwagia kimiminika (elixir)cha miujiza katika paa la chini la mdomo wake (palate),kwa mujibu wa gazeti la Telegraph la London. 


Wakati baadhi ya watu wanamwona kama 'mzushi' flani,taasisi ya maendeleo ya utafiti wa ulinzi inasema Prahlad anaweza kutoa mwangaza katika kuwasaidia wanajeshi kumudu kukaa muda mrefu bila kula,au hata wahanga wa majanga mbalimbali.Hadi sasa amekaa siku sita bila kula au kunywa chochote katika hospitali iliyopo Hyderabad,na madaktari wanasema haonyeshi dalili yoyote ya kuathiriwa na njaa.

"Ikithibitika kuwa madai yakni sahihi,basi itakuwa hatua kubwa sana kwenye sayansi ya tiba",anasema Dkt G.Ilavazhagan,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulinzi ya Fiziolojia na Stadi Shiriki."Itatuwezesha kuokoa maisha ya wanadamu katika nyakati za majanga,kimo cha juu,safari za majini,na mazingira mengine magumu ya kibinadamu na ya asili.Tutaweza kuwaelimisha watu kuhusu namna ya kustahimili (surviving) mazingira magumu pasipo chakula na maji au chochote kile".

Madaktari wataendelea kumchunguza kwa siku 15 kipindi ambacho wanataraji kuona misuli yake ikisinyaa,upungufu mkubwa wa maji mwilini,kupungua uzito wa mwili na baadhi ya viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi.

Binadamu wengi hawawezi kustahimili zaidi ya siku 3 hadi 5 pasipo kunywa maji.

Imetafsiriwa kutoka gazeti la Daily News la India.

3 comments:

  1. Ni mtu wa kipekee kabisa. Tusubiri tuone.

    ReplyDelete
  2. Du hiyo kali. Siju wana UTAMBUZI wanatueleza nini kuhusu jambo hilo.

    ReplyDelete
  3. India wanazo Tabia nasikia sa madaktari kuwapa pesa watu ili ifanyike documentary tu wapate umaarufu hospital ni wazushi mtu anaweza kukaa week mbili bila kula ila week ya tatu ataona mambo kuhusu maji na wanampa tu hao maji.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.