5 Jan 2011


Lowassa awaonya vigogo wanaojali matumbo yao

na Violet Tillya, Arusha

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametoa wito kwa wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo kubadilisha hali ya maisha ya wananchi wao kiuchumi.
Kadhalika amewataka viongozi hao kuweka kipaumbele katika kujali matumbo ya wapigakura wao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwakopesha ili waweze kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi hapa nchini.

Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Manyire, Kata ya Mlangarini, wilayani Arumeru alipokuwa akizungumza katika sherehe za kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua diwani wao Mathias Manga (CCM).

"Wakati umefika kwa viongozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kubadilika na kuacha tabia na mazoea ya kujinufaisha wao wenyewe na familia na jamaa zao na kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi kuwatumikia wananchi hususan kujali wanakula nini" alisema Lowassa.

Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uamuzi wake wa kukubali mabadiliko ya Katiba na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wakati ukifika wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao.


MBONA MAMBO!YAANI MPAKA KUFIKIA 2015 TUTASIKIA MENGI

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.