Showing posts with label Duniani kuna Mambo. Show all posts
Showing posts with label Duniani kuna Mambo. Show all posts

25 Sept 2011


Mchungaji aliyetibuana na kanisa lake ameanzisha kanisa la Facebook.Mchungaji Mark Townsend (44),ameanzisha kanisa analoliita The Hedge-Church baada ya kuhitilafiana na wazee wa Church of England.

Katika kuchangisha fedha,mchungaji huyo  pia anamiliki tovuti ya kukodisha mchungaji,ijulikanayo kama Rent-a-Rev ambayo inachaji kati ya pauni 40 (Shs 102,029.40) na 150 (shs 382,610.25) kwa ajili ya kufungisha ndoa za wandandoa wa jinsia moja au wa jinsia tofauti,ibada za mazishi na ubatizo,shughuli ambazo zinafanyikia aidha msituni,majumbani au hata kwenye baa.

Kanisa hilo tayari lina waumini 416 na inaaminika kuwa ni la aina yek duniani.Misa na huduma za maombi zinafanyikia mtandaoni na waumini wanatumia ujmumbe wa baraka kila siku kutoka kwa Mchungaji Townsend.

Mwezi ujao,Mchungaji huyo ataendesha ibada ya komunio itakayoonyeshwa moja kwa moja mtandaoni (live streaming).Mark,kutoka eneo la Leominster,Herefordshire,anasema: "Niliamua mwaka jana kuachana na Church of England.Kwa miaka 10 iliyopita nimelitumikia kanisa hilo katika mahusiano ya upendo-chuki (love-hate relationship).Nililazimika kufanya mambo ambayo nilikuwa siyaamini na nilitamani sana mabadiliko.Imechukua mwongo mzima  (kipindi cha miaka 10) kwa dhamira yangu kutimia."

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa kutoka gazeti la Daily Recond la hapa Scotland toleo la jana (Jumamosi,Oktoba 24,2011)

1 Aug 2011


Familia yenye furaha: Kushoto ni Baba mtoto Jordan (15),akifuatiwa na  mama mtoto Tia (14) na kichanga  Gracie,na nyuma ni babu kijana  Shem (29) na kulia ni bibi kijana  Kelly (30)

Kwa namna ilivyozoeleka,unaposikia "babu" au "bibi" unadhani pasi wasi kuwa mtajwa ni aliyekula chumvi nyingi,na huenda umri wake upo kwenye miaka ya 50 na kuendelea.Na sia ajbu ana mvi lukuki.

Hali si hivyo kwa Shem Davies,kijana mwenye umri wa miaka 29 ambaye wiki hii amekuwa "Babu Kijana Zaidi nchini Uingereza."Davies,ambaye hana kazi (unemployed),amefanikiwa kupata mjukuu baada ya bintiye wa kike aitwaye Tia (umri miaka 14!!) kujifungua mtoto aitwaye Gracie.
Baba na mwana:  Shem na mwanaye Tia na kijukuu Gracie

Kuzaliwa kwa Tia (miaka 14 iliyopita) ni matokeo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Shem na mwandani wake wa zamani aitwaye Kelly John mwenye umri wa miaka 30 sasa.

Kuchanganya madawa zaidi,kijana aliyezaa na Tia (mama mtoto mwenye miaka 14) naye ni serengeri boy wa miaka 15 tu!Kwa jina anaitwa Jordan Williams (pichani chini akiwa na mzazi mwenzie na kichanga chao)

Kwahiyo mjukuu amepatikana kwa mama mwenye miaka 14 na baba mwenye miaka 15,na ana babu wa miaka 29 na bibi wa miaka 30!

Lakini ukiangalia kwenye picha zinazoambatana na habari hii itakuwia vigumu kutambua umri wa wahusika wa Isidingo hii.Tatizo ni kwamba ni vigumu sana kukadiria umri wa hawa "wazungu."

Uingereza ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mabinti wanaojifungua kabla ya kutimiza miaka 18.

CHANZO: Daily Mail

22 Jul 2011



Mwanamama mmoja na mumewe huko Aberdeen,Scotland walikumbwa na kiwewe baada ya kukumbana na bonge la dude kwenye ufukwe wa Bahari ya Kaskazini.Well,dude hilo halikuwa hai bali kiufasaha ni masalia ya "sea monster" (sijaui tafsiri yake kwa Kiswahili ni ipi)?Pata picha ndio ungekuwa wewe peke yako...Hadi sasa haijafahamiaka masalia hayo ni ya kiumbe gani wa baharini lakini wataalam wanabashiri kuwa inawezekana ni ya papa muuaji (killer whale) au papa rubani (pilot whale)

Papa muuaji  

Papa rubani

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.