25 Sept 2011


Mchungaji aliyetibuana na kanisa lake ameanzisha kanisa la Facebook.Mchungaji Mark Townsend (44),ameanzisha kanisa analoliita The Hedge-Church baada ya kuhitilafiana na wazee wa Church of England.

Katika kuchangisha fedha,mchungaji huyo  pia anamiliki tovuti ya kukodisha mchungaji,ijulikanayo kama Rent-a-Rev ambayo inachaji kati ya pauni 40 (Shs 102,029.40) na 150 (shs 382,610.25) kwa ajili ya kufungisha ndoa za wandandoa wa jinsia moja au wa jinsia tofauti,ibada za mazishi na ubatizo,shughuli ambazo zinafanyikia aidha msituni,majumbani au hata kwenye baa.

Kanisa hilo tayari lina waumini 416 na inaaminika kuwa ni la aina yek duniani.Misa na huduma za maombi zinafanyikia mtandaoni na waumini wanatumia ujmumbe wa baraka kila siku kutoka kwa Mchungaji Townsend.

Mwezi ujao,Mchungaji huyo ataendesha ibada ya komunio itakayoonyeshwa moja kwa moja mtandaoni (live streaming).Mark,kutoka eneo la Leominster,Herefordshire,anasema: "Niliamua mwaka jana kuachana na Church of England.Kwa miaka 10 iliyopita nimelitumikia kanisa hilo katika mahusiano ya upendo-chuki (love-hate relationship).Nililazimika kufanya mambo ambayo nilikuwa siyaamini na nilitamani sana mabadiliko.Imechukua mwongo mzima  (kipindi cha miaka 10) kwa dhamira yangu kutimia."

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa kutoka gazeti la Daily Recond la hapa Scotland toleo la jana (Jumamosi,Oktoba 24,2011)

1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube