22 Mar 2008

Jana nilishuhudia kituko cha mwaka.Mwanzoni nilidhani ni porojo tu lakini asubuhi hii nimeona tukio hilo limekuwa gumzo mtandaoni.Ilikuwa takriban saa 6 mchana za hapa (hapa saa zitabadilika mwishoni mwa mwezi huu),nikaamua kupoteza muda kwa kuangalia kipindi cha Fox&Friends.Nasema kupoteza muda kwa vile waendesha kipindi hicho huwa wananikera sana kutokana na kauli zao za upendeleo wa wazi kwa wahafidhina na upinzani wao mkubwa dhidi ya Democrats na liberals.Sikujutia uamuzi wa "kupoteza muda" kwani huku watangazaji Steve Doocy na Gretchen Carlson wakishikia bango kauli ya Obama kwamba grandmom wake ni like typical White person,mwenzao Brian Kilmeade aliamua kuondoka kwa muda studioni kutokana na kukerwa na namna wenzie walivyokuwa wakimsakama Obama.Kama hiyo haitoshi,muda mfupi baadaye,mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho,Chris Wallace,alionekana hewani wakati Fox&Friends inaendelea ambapo alielezea waziwazi kwamba alikuwa akiangalia kipindi hicho na hakupendezwa na namna kauli ya Obama kuhusu bibi yake ilivyokuwa ikipotoshwa.Wallace alieleza wazi kwamba yeye si msemaji wa kambi ya Obama lakini angependa kuona kipindi hicho kinazungumzia suala hilo ndani ya context,na kwenda mbali zaidi kwa kuwashauri wana-Fox&Friends kuangalia pia habari nyingine za muhimu kuhusu Obama kama vile endorsement ya Bill Richardson na hotuba zake mbili kuhusu uchumi na vita ya Irak.

0 comments:

Post a comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2020

Powered by Blogger.

Nisapoti

Podcast

Chaneli Ya YouTube