18 Mar 2008

Gazeti la Los Angeles Times lina habari kwamba rapa tajiri na maarufu,Sean "P.Diddy" Combs alikuwa na taarifa za ndani kuhusu mpango wa mauaji ya Tupac Shakur aliyepigwa risasi na hatimaye kufariki Novemba mwaka 1994.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi za gazeti hilo,watu mbalimbali wamethibitisha tuhuma hizo ambazo zimekanushwa vikali na P.Diddy.Itakumbukwa kwamba kifo cha Tupac kinahusishwa pia na mauaji ya rapa mwingine maarufu Christopher Wallace a.k.a. Notorious B.IG. ambacho kinadhaniwa kuwa ni kisasi cha washirika wa Tupac.


                
              Uchunguzi huo wa L.A.Times unadai kwamba sababu kubwa iliyopelekea kuuawa kwa Tupac ni "adhabu" kwa nguli huyo wa rap kukataa kuwa mshirika wa kibiashara wa lebo ya Bad Boy inayomilikiwa na P.Diddy.

Kwa habari zaidi soma habari hiyo ya kusisimua kwa KUBONYEZA HAPA.Hapo chini ni clip ya B.I.G katika track Mo Money Mo Problems akimshirikisha Puff Daddy na Mase


Pia waweza kuangalia track hii hapo chini ya Tupac  f/t The Outlawz (Caution: Very Explicit Lyrics) Hit Em Up ambapo rapa huyo na vijana wake wanatupa "madongo" makali kwa P.Diddy (enzi hizo akijulikana kama Puff Daddy),B.I.G,Lil' Kim,Lil' Cease,Mobb Deep na lebo nzima ya Bad Boy.Ni dhahiri kuwa track hii ilichangia sana kukuza beef kati ya mahasimu hao wa Pwani ya Mashariki na ya Magharibi huko Marekani.2 comments:

  1. Lol! What is Diddy doing up there?...Is that mgongo mgongo dance style or?..Lol

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2020

Powered by Blogger.

Nisapoti

Podcast

Chaneli Ya YouTube