12 Sept 2008

Nani kasema vibaka na wezi wanaenda likizo mwezi wa toba?Hebu cheki kituko hiki kilichojiri ndani ya msikiti.Kwa mujibu wa gazeti la Dar Leo,JESHI la Polisi (huko nyumbaniTanzania) linamsaka mwanaume mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja kwa tuhuma za kumpa Baraka Rwambow (22), futari yenye dawa za kulevya kisha kumpora pikipiki yake katika msikiti wa Tambaza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Jamal Rwambow amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni, msikiti wa Tambaza. 
Amesema kijana huyo alikodiwa Kimara Temboni na mtu anayemfahamu kwa sura ili ampeleke msikiti wa Tambaza kwa ajili ya kuswali swala ya magharibi. Amesema kuwa baada ya kufika msikitini hapo mtu huyo aliingia ndani kuswali na baada ya kutoka alimpa dereva wa pikipiki futari hiyo ambapo alikataa na alimbembeleza akaamua kula. Baada ya kula mtu huyo alianza kulegea na mwishowe alimuomba mteja wake huyo amuendeshe ili waweze kurejea nyumbani ambapo mteja huyo aling'oa pikipiki na kwenda moja kwa moja Salender Club na kumtupa kijana huyo akiwa hajitambui. 

Walinzi waliokuwepo jirani walimuokota mtu huyo na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.Polisi wanaendelea kumsaka mtu huyo na pikipiki hiyo aina ya Royck.

Ama kweli dunia haijaishiwa vituko.Hebu tumwangalie na huyu nae.Jana dunia iliungana na Wamarekani kuadhimisha mwaka wa saba wa mashambulizi ya kigaidi ya September 11,2001.Licha ya kusababisha majonzi na kubadili mwenendo wa mambo ulimwenguni,tukio hilo lilizaa mashujaa kadhaa:kwa mfano watu waliojitolea mhanga kuokoa maisha ya wenzao na wale walionusurika kufa katika majengo yaliyoshambuliwa.Kumbe kuna "wasanii" walioona nafasi ya kujichukulia ujiko wa kuwa mashujaa wa September 11 hata kama hawakuwepo mahala pa tukio.Mfano ni HUYU SHUJAA FEKI WA 9/11.

0 comments:

Post a comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2020

Powered by Blogger.

Nisapoti

Podcast

Chaneli Ya YouTube