27 Dec 2008


POSTMORTEM NI MUHIMU HASA KWENYE VIFO VYENYE UTATA.LAKINI POSTMORTEM KWENYE MASUALA YA SIASA NI MBINU INAYOTUMIKA AIDHA KUKWEPA LAWAMA NA KUZIELEKEZA MAHALA KWINGINE AU KUPOOZA MAUMIVU YALIYOSABABISHWA NA MAPUNGUFU KWENYE UWAJIBIKAJI.KATIKA HABARI IFUATAYO,MBUNGE WA HANDENI,DKT ABDALLAH KIGODA, AMETOA POSTMORTEM REPORT YA MPANGO WA "MABILIONI YA JK",KWAMBA HAYAKUWANUFAISHA WATU WA VIJIJINI.PENGINE KABLA YA KUANGALIA VIJIJINI,SWALI KUBWA LILIPASWA KUWA "MABILIONI HAYO YAMEWANUFAISHA WATU WANGAPI REGARDLESS YA LOCATIONS ZAO-MIJINI AU VIJIJINI".LAKINI LA MSINGI ZAIDI,JE POSTMORTEM REPORT KAMA HIYO YA KIGODA INA UMUHIMU GANI KWA WANANCHI AMBAO HAWAKUNUFAIKA NA MPANGO HUO ULIOLENGA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA?SOMA KWANZA HABARI YENYEWE KISHA TUENDELEE NA MJADALA:
Na Steven William, Handeni
MBUNGE wa Handeni Dkt Abdallah Kigoda, amesema kuwa dhamira ya Rais Jakaya Kikwete kutenga fedha kwa ajili ya kukopeshwa wajasiriamali wadogo alikuwa na dhamira nzuri, lakini fedha hizo zilivamiwa na 'wajanja' wachache waliozikopa na wananchi hasa wa vijiji hazikuwafikia.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya kata ya Ndolwa wilayani hapa juzi kufuatia wananchi kumbana mbunge huyo kuhusu mikopo hiyo maarufu 'mabilioni ya Kikwete', mbunge huyo alisema kuwa fedha hizo zilitengwa na kupitia benki ambako wananchi wengi hasa wa vijijini hawana uelewa mpana wa kutumia benki zilizopo kukopa.

"Ndugu zangu wananchi dhamira ya Rais ilikuwa nzuri kwani alitenga fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia wenye mitajhi midogo wapandishe mauzo ya bidhaa zao lakini fedha zile zilipitia benki na nyie uwezo wa kuzitumia benki hamjui, hivyo wajanja wakajitokeza wakazichota," alisema Dkt Kigoda.

Aliwapa mfano wa mkoa wa Kagera fedha hizo zilizpopelekwa mkoani humo, ni watu watano tu waliopata fedha hizo kutoka katika benki hizo akiwemo meneja wa benki hiyo hali iliyoleta tafsiri mbaya kwamba waliozichukua ni watu wa mjini waliokuwa na fursa nzuri na uzoefu wa kukopa benki.

Hata hivyo, aliwatoa wasiwasi wananchi hao kwamba serikali itatoa tena fedha lakini walishauri kwamba pindi zikitolewa zishirikishe viongozi wa wilaya husika wachama na serikali ambao wamekuwa wakifahamu vikundi mbalimbali vya wajasiriamali katika maeneo husika hivyo fedha hizo zitafika kwa walengwa.

Kufuatia kuingizwa tena fedha hizo kwenye mabenki hayo, mbunge huyo aliwataka wananchi wa wilaya ya handeni kuhakikisha wanajiunga na vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitatambulika na serikali ili waweze kuomba na kupata mikopo.

CHANZO:Mwananchi

HIVI DKT KIGODA ALIKUWA WAPI WAKATI FEDHA HIZO ZIKIELEKEZWA KUSIKOSTAHILI?NA WAKATI ANATOA TAKWIMU ZA KAGERA,KWANINI HATAJI IDADI YA WALIONUFAIKA AU KUATHIRIKA KATIKA JIMBO LAKE LA HANDENI?PIA ANAPASWA KUWAOMBA RADHI ALIOKUWA AKIWAHUTUBIA KWA KUSEMA "..na nyie uwezo wa kuzitumia benki hamjui".HIVI NI KWELI WANAKIJIJI WOTE ALIOKUWA AKIWAHUTUBIA,NA WENGINEO AMBAO HAWAKUPATA MABILIONI HAYO HAWANA UWEZO WA KUZITUMIA BENKI?JE YEYE KAMA KIONGOZI NA MWAKILISHI WAO AMEFANYA NINI KUWASAIDIA WAPIGA KURA WAKE KUWA NA UWEZO WA KUJUA NAMNA YA KUZITUMIA BENKI?BY THE WAY,NENO "KUZITUMIA" NI CONTRADICTORY KWANI LINAWEZA PIA KUMAANISHA KUZITUMIA BENKI KAMA ILIVYOKUWA KATIKA UFISADI WA EPA.ANYWAY,NADHANI ALIKUWA ANAMAANISHA WANAKIJIJI HAWAJUI KUZITUMIA HUDUMA ZA BENKI.IF SO,HAWAJUI KWA VILE HAKUNA BENKI,BENKI ZIPO LAKINI HAZITOI ELIMU YA NAMNA YA KUTUMIA HUDUMA ZAKE,WANAKIJIJI HAWATAKI KUELEKEZWA NAMNA YA KUTUMIA HUDUMA HIZO,AU...?

TATIZO KUBWA LINALOKWAMISHA MIPANGO MIZURI NI MIPANGO MIBOVU.WAINGEREZA WANA MSEMO POOR PLANNING PRODUCES POOR PERFORMANCE.UBOVU WA MPANGO WA MAMILIONI YA JK ULIKUWA KWENYE USIMAMIZI.NI DHAHIRI KWAMBA UKIPELEKA MAMILIONI,LET ALONE MABILIONI,PASIPO KUHAKIKISHA KUWA WAJANJA (ISOMEKE MAFISADI) HAWATABUNI MBINU ZA KUTAFUNA FEDHA HIZO,ITAKUWA NI MITHILI YA KUTWANGA MAJI KWENYE KINU.

MPANGO WA KUWAPATIA FEDHA WANANCHI WASIO NA UWEZO ILI ZIWASAIDIE KUJIKWAMUA KIUCHUMI ULIKUWA MZURI LAKINI ULIHITAJI UCHAMBUZI MAKINI KATIKA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WAKE.KULIKUWA NA HAJA YA KUANGALIA POWER RELATIONS HUKO ZINAKOPELEKWA FEDHA HIZO,HUSUSAN MAHUSIANO KATI YA WASIMAMIZI NA WALENGWA.UDHAIFU KATIKA HILO NDIO UMEPELEKEA KESI KAMA HIYO YA KAGERA AMBAPO MENEJA WA BENKI NAE AKAJIINGIZA MIONGONI MWA WALENGWA JAPO SIDHANI KAMA ILIPASWA KUWA HIVYO.KILICHOPASWA KUFANYIKA KABLA YA KUPELEKA FEDHA HIZO NI KUTAMBUA WANAOZIHITAJI,KUFAHAMU MIPANGO YAO YA NAMNA WATAKAVYOTUMIA FEDHA HIZO AMBAZO KIMSINGI NI MIKOPO,KUTENGENEZA MAZINGIRA AMBAPO MAFISADI HAWATAZITAFUNA NA MWISHO,KUZIWASILISHA KATIKA WAKATI MWAFAKA.

PENGINE KABLA YA KUFIKIRIA KUTOA AWAMU NYINGINE YA MABILIONI NI MUHIMU KUFANYA TATHMINI YA MAFANIKIO NA FAILURES KATIKA AWAMU ZILIZOTANGULIA.SAMBAMBA NA HILO NI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WOTE WALIOFUJA FEDHA HIZO.PIA NI MUHIMU KUFAHAMU FEDHA HIZO ZITAREJESHWA VIPI ILI BAADAYE WASIJE WAJANJA WAKAPORA ARDHI NA MALI NYINGINE ZA WALALAHOI KWA VISINGIZIO VYA KUDAI MAREJESHO YA FEDHA HIZO.

MWISHO,VIONGOZI KAMA DKT KIGODA WANAWEZA KUWA NA UMUHIMU ZAIDI KATIKA KULETA UFANISI WA MPANGO HUO WA MABILIONI YA JK SIO KWA KUTULETEA POSTMORTEM PINDI MAMBO YAKIENDA MRAMA BALI KWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUHAKIKISHA MAFANIKIO YANAPATIKANA.HILO HALIHITAJI SEMINA ELEKEZI KWANI LIKO NDANI YA UWEZO WETU.KINACHOHITAJIKA NI DHAMIRA NA UWAJIBIKAJI.YES WE CAN!

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.