26 Feb 2009


MKUU wa wilaya ya Maswa, James Yamungu, amempongeza aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Albert Mnali, akimwita kuwa ni shujaa kutokana na kitendo chake cha kuchapa viboko walimu wa shule tatu za msingi na kusababisha atimuliwe kazi na Rais Jakaya Kikwete.

Mnali, ambaye hakujutia kitendo chake cha kuchapa walimu akisema alikuwa tayari kwa uamuzi wowote toka juu, aliwachapa viboko walimu wa shule za Kansenene, Katerero na Kanazi kwa madai ya utoro kazini, kuchelewa na uzembe na kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu kwenye wilaya hiyo. Kitendo chake kililaaniwa na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali na kufuatiwa na uamuzi wa Rais Kikwete kumvua ukuu wa wilaya.

Lakini jana, mkuu wa wilaya ya Maswa alionekana kuchukulia kitendo hicho kuwa sahihi na kumuita Mnali kuwa ni shujaa. Akizungumza wakati akifungua mkutano mkuu wa tatu wa chama cha kuweka na kukopa cha Nyalikungu uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo, kapteni huyo mstaafu wa jeshi alisema kuwa Mnali ni shujaa ambaye alikuwa akiwatetea Watanzania licha ya kitendo chake kusababisha atimuliwe. ..
ENDELEA


CHANZO: Mwananchi


YAYUMKINIKA KUAMINI KWAMBA KUNA TATIZO KATIKA UTEUZI WA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI HASA KATIKA NGAZI ZA MIKOA NA WILAYA.SIJUI NI KUJISAHAU,SIJUI NI KULEWA MADARAKA,AU SIJUI NDIO ILE "MIE NDIO RAIS WA WILAYA,KIJIJI,NK" INAYOWAPA BAADHI YA MA-RC,MA-DC,NA VIONGOZI WENGINEO KATIKA NGAZI MBALIMBALI KUJIONA WAKO JUU YA SHERIA,WAKO SAHIHI KATIKA KILA WAFANYACHO,NA PENGINE KUJIONA WAKO SAHIHI KULIKO HUYO ALIYEWATEUA (RAIS).HIVI HUYU DC ANAYEMWITA MWENZIE ALIEFUKUZWA NA RAIS KUWA NI SHUJAA HAFANYI DHIHAKA KWA RAIS?SI VIGUMU KUJUA WANAPATA WAPI JEURI HII....

1 comment:

  1. Nchini Bongo kuna mambo.

    Nakubaliana na wewe Kaka Chahali kwamba inawezekana kwamba kuna tatizo la kimsingi katika uteuzi wa hawa wnaojiita watawala.

    Kwa nini usiwepo utaratibu wa hawa wanaoitwa wateule wa Rais kuchaguliwa na wananchi wenyewe?

    Kinachofanyika hivi sasa ni matokeo ya wingi wa wateule kiasi kwamba inaonekana kwamba wateule wengine hata hawafahamiki kwa mteuzi wao.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.