23 Jun 2009


Pengine siendi na wakati.Pengine mgumu wa kuelewa.Pengine....well,pengine sina hoja bali naibua tu cha kuropoka.All in all,mie ni miongoni mwa sijui wengi au wachache ambao hizi SIKU MAALUM hazina umuhimu kihivyo.Tuanze na siku ya kuzaliwa (BIRTHDAY).Mie nilizaliwa tarehe inayofanana na siku ya Uhuru na Jamhuri,yaani 9 Desemba (mwaka sabini na kitu).Excuse yangu kubwa ya "kuipuuza" birthday yangu huwa "tayari taifa linasherehekea pamoja nami".Si unajua 9 Desemba huwa ni mapumziko huko home?Halafu maswala ya gwaride na vikorombwezo vingine.Well,inatosha kuwa kiji-excuse cha namna flani.La muhimu kwangu katika kila 9 Desemba ni kumshukuru Mungu kwa kunifikisha siku hiyo,kisha kuongea na wazazi.Baba na marehemu mama walijenga utaratibu wa kutuimbia wimbo wa hepi bethdei to yuuu...That's it.Sala,wimbo na dua za wazazi,siku imekamilika.Hizo habari za birthday parties ni msamiati ambao haujaingia kwenye kamusi yangu.


Kuna kitu inaitwa MAHAFALI.Well,sikumbuki vyema kuhusu mahafali ya kumaliza darasa la saba lakini natambua kuwa ilikuwa mbinde hapo Ifakara.Uchumi wa familia haukuruhusu anasa zisizo na msingi,na wakati huo (1985) taifa nalo lilikuwa katika wakati mgumu vilevile.Si zamani kihivyo.lakini mengi ya yanayoonekana leo hayakuwepo zama hizo.

Nadhani kitu pekee nachokumbuka kuhusu mahafali ya kumaliza kidato cha nne ni uamuzi nilokuja kuujutia baadaye wa kuonja kilevi cha kiwandani.Nilijaribu bia aina ya Safari Lager kwa mara ya kwanza maishani.Of course,kabla ya hapo nilishawahi kujaribu kilevi cha asili cha pombe ya mpunga.Ili nisije sahau,ni vema nikujulishe kidogo kuhusu pombe hii inayonukia kama wali.Kwa kifupi,ukiinywa saa 10 jioni basi inakuwa kichwani hadi kesho saa 10 jioni.Well,at least kwa "vichwa panzi" kama nilivyokuwa siku hizo.

Basi hiyo Safari Lager ilinipelekesha kupita maelezo.Nadhani nilifanya vituko kadhaa lakini kumbukumbu zaidi niliyonayo ni kuugua kwa takriban wiki hivi.Ungetegemea kuwa hiyo ndio ingekuwa mara yangu ya kwanza na ya mwisho kugusa kilauri.Wapi!Ukiniuliza namna gani niliweza kuji-transform kutoa mnywaji anayeugua wiki nzima baada ya kunywa bia moja hadi kufikia hatua kummudu John Mtembezi (John Walker),sidhani kama nitakuwa na jibu sahihi.

Anyway,mahafali ya kidato cha sita hata sikumbuki yalikuwaje.Shule yenyewe ilikuwa ya kijeshi (Tabora Boys) halafu nilikuwa miles away from home.Mahafali kwa maana ya mahafali yalikuwa ya kuhitimu Mlimani (UDSM).Kuna waungwana walishauri nitengeneze kadi za mchango wa sherehe ya mahafali.Well,it worked.Watu wakapiga donation,likapatikana fungu la kufanya sherehe ya maana mtaa wa Isisi,Kinondoni.Na kuna mahala flani walinisaidia bia za bei nafuu.

Hapa Aberdeen nilijichukulia tu vyeti vyangu hapo 2003 na 2004.Ila nikikamilisha libeneke hili la sasa,huenda nikajumuika na watu wawili watatu maana hii ya sasaa ni shughuli nzito kwa kiasi kikubwa.

Back to the topic.Sijui Father's Day ni leo au kesho au ishapita.Honestly,muda huu naoandika post hii sina hakika,na sitaki kuhakikisha kwa ku-google.Kwangu,siku ya Baba yangu (na kama ilivyokuwa kwa Mama yangu) ni kila siku.Najua kwanini kuna siku moja maalumu,lakini kwa mie kila siku ni maalum.Yaleyale ya siku ya Wapendanao.Nikimpenda mwandani wangu basi ni suala la kila siku na Ferbuari 14 inakuwa siku kama siku nyingine tu.Of course,nimeshawahi kuonekana kichekesho huko nyuma lakini hainisumbui.

Vipi,huu mtazamo wangu unaouonaje?Ukale,uzembe wa kwenda na wakati,sahihi au you dont even care?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube