23 Jul 2009Hiyo sio sanamu,bali "msanii" mmoja ambaye kila wikiendi anavizia mtaa ulio bize na "kuganda kama sanamu" kisha kutoa vijishara vya kuvunja mbavu.Hulazimishwi kutoa asante bali "mchango wako utathaminiwa".Ni mchanganyiko wa ubunifu na "usanii" (i.e. ujanja-ujanja wa kuishi mjini)

Huyu nae ni mtaalam wa cover versions,or sort of off.Ukiskia muziki wake pasipo kumtia machoni unaweza kudhani The Killers,Coldplay,au rockers flani wanafanya concert mtaani minus makelele ya kawaida ya rock stars.Kipaji?Usanii? Well,katika zama hizi za recession,credit crunch na vitu kama hivyo,si serikali na taasisi za fedha pekee zinazohitaji kuwa na mikakati ya kujinusuru.Nahisi "wasanii" hawa wanatumia vipaji-au ujanja ujanja-kukabiliana na hali hiyo.At the end of the day,kinacho-matter ni kono kwenda kinywani.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Philemon Chahali 2006-2018

JUMUIKA NAMI TUMBLR

  Sehemu Ninahifadhi Nyaraka Zangu!

Powered by Blogger.

Download "Chahali Blog ANDROID App"

UNGANA NAMI FACEBOOK