30 Mar 2010

Your blog-Kulikoni Ughaibuni-is always striving to come up with spanking new ideas,the latest being an introduction of "THE WEEK IN BULLSHIT".It's all about the weirdest,craziest and even funniest stuffs that happened during a given week. Siku zote Blogu yako ya Kulikoni Ughaibuni imekuwa ikijitahidi kuja na mawazo mapya,na lililojiri sasa ni UPUUZI/UBABAISHAJI KATIKA WIKI.Hii itahusu habari za vimbembe,uzushi na vichekesho vilivyojiri katika wiki husika.

Kimbembe cha kwanza katika safu hii ni taarifa kwamba mwanamama mmoja aliyetinga nyumbani kwa Inspekta Jenerali mstaafu wa Polisi (IGP),Omari Mahita,"kujitambulisha" kuwa ni mtoto wa afannde huyo,ameishia kuswekwa lupango kwa kosa la "kuingia kwa jinai".

Wakati blogu hii haina mamlaka ya kuhukumu iwapo ni kweli mwanamama huyo,Sophia Mahita (45) ni mtoto halali wa Afande Omari,kitendo cha jeshi la polisi kumswekwa rumande mwanamke huyo ni cha uonevu usiposwa kulelewa.Kwanini,kwa mfano,badala ya kumsweka ndani wasingefikia uamuzi wa kuitisha vipimo vya DNA?Ikumbukwe kuwa Afande Mahita ana historia ya kuwa na mtoto nje,na kukana,kama ilivyothibitika kwenye kesi ya mwaka 2006 iliyofunguliwa na ex-mtumishi wa ndani wa Mahita,Rehema Shabani .Katika kesi hiyo Rehema alidai alitungwa ujauzito na Mahita na alikuwa anahitaji msaada katika matunzo ya kijana wao.Afande alikanusha 'mzigo' huo,lakini hatimaye mahakama ilitoa hukumu kuwa 'ngunguli' huyo ni baba halisi wa mtoto husika.

Jeshi letu la polisi ni miongoni mwa taasisi zinazoongoza kwa ubabe na ukiukaji wa haki za binadamu.Lakini jeuri walioyonayo inachangiwa zaidi na udhaifu mkubwa katika taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zinazohusika na uangalizi na kuhakikisha haki za binadamu nchini.Ni katika mazingira hayo ndipo tunakuta wanyonge wakihofia kuwaripoti vigogo au wenye nazo kwa vile si ajabu wanyonge hao wakaishia kugeuziwa vibao.

A mini-bullshit of the week ni uamuzi wa CCM kumteua Zakia Menghji kuongoza kamati ya usimamizi wa fedha na vifaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.Hivi huyo mama si ndiye aliyeingizwa mkenge na mafisadi wa EPA na kuidhinisha mabilioni yaliyokwibwa na majambazi hao?Labda,nasisitiza LABDA,uteuzi huo umezingatia uzoefu wake katika namna ya kudili na mafisadi kutoa chochote kwa chama hicho tawala.

See you next time

1 comment:

  1. Tanzania is like HEARTACHEDEPOT.
    Haki za mwananchi ni utashi wa viongozi.Nakikaribisha kipengele hiki ambacho kitaongeza uchaji wa maswali tunayostahili kujiuliza kuhusu mengi "ya ajabu" yatendekayo.
    Panaburudisha huku pakitafakarisha

    Kwangu kipengele kifananacho na hiki nakiita WALIWAZA NINI? (http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Waliwaza%20nini%3F%3F)

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.