27 Apr 2010

Tarehe 6 ya mwezi ujao,Waingereza watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu.Kura za maoni zinaonyesha kuwa hakuna chama kitakachopata ushindi wa kutosha kuunda serikali peke yake (hung parliament).Vyovyote itakavyokuwa,kuna mambo kadhaa mbayo Watanzania wanaweza kujifunza katika uchaguzi huu hasa kwa vile nasi tutakuwa na uchaguzi hapo Oktoba mwaka huu. 


Kubwa zaidi ni namna wagombea wanavyohangaika kuwabembeleza wapiga kura.Unajua kuna kijitabia cha baadhi ya wanasiasa huko nyumbani ambao sijui ni ulevi wa madaraka au dharau kwa wapiga kura,hawajihangaishi hata kidogo kuwaonyesha wapiga kura kuwa ajira zao zinategemea ridhaa za wapiga kura hao.Pengine ni jeuri ya uwezo wao wa kununua kura katika jina la takrima au kudumisha chama.

Yani hapa ukiangalia kwenye runinga namna Waziri Mkuu wa sasa,Gordon Brown,anavyopelekeshwa na wapiga kura kwa maswali mazito kana kwamba utawala wake ulikuwa mbovu kupindukia,unapata picha kuwa kwa hawa wenzetu GOOD IS NOT ENOUGH,THEY WANT EVEN BETTER (Ubora tu hautoshi,wanataka ubora zaidi).Na si kwamba Brown na Labour yake hawajafanya mambo ya maana kwa Waingereza bali watu hawa hawapendi 'kuangushwa' kwa aina yoyote ile.

Na jingine linalovutia katika kampeni hizi ni namna wapiga kura wanavyozipa manifesto za vyama umuhimu mkubwa na pengine mwelekeo wa nani watampigia kura.Kwetu,manifesto ni sawa na waraka unaokumbukwa wakati wa chaguzi na 'kinga' ya kujitetea pale mambo yanapokwenda mrama.Wengi tunafahamu namna akina Makamba wanavyotumia manifesto ya CCM kujibu shutuma mbalimbali zinazoelekezwa kwa chama hicho tawala.Hilo sio kosa bali tatizo ni kwamba utetezi huo mara nyingi hauendani na hali halisi.Kwa mfano haitoshi kusema manifesto ya CCM inatamka bayana kuhusu 'chuki' yake dhidi ya rushwa huku in practice hadi leo hatufahamu Kagoda ni mdudu gani.Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno,so Waswahili say.

Manifesto ya CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 iliweka bayana dhamira yake ya kupata ufumbuzi wa suala la mahakama ya kadhi lakini hadi leo suala hilo linapigwa danadana.Utafiti wangu wa shahada ya uzamili kuhusu harakati za vikundi vya waislam nchini Tanzania (unaoelekea ukingoni) ambao umegusia kwa undani suala hilo unaashiria kuwa 'kupuuzia' kero (grievances) kama hiyo ya mahakama ya kadhi na suala la OIC yana potential ya kusababisha matatizo huko mbeleni.Tatizo haliwezi kutatuliwa kwa kuliepuka bali kulikabili.We have to solve difficulties before they become problems (tunapaswa kutatua ugumu kabla haujawa tatizo).

Ni matumaini ya wapiga kura wa Tanzania kuwa watatumia haki zao za kidemokrasia kwa busara zaidi kuchagua wagombea wanaoweza kuwatumikia kwa dhati.Zama za ushabiki wa vyama zimepitwa na wakati hasa kwa vile kitakachowakomboa Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini na ufisadi sio ushabiki bali ufanisi wa chama.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.